Wakati dunia nzima ikifuatilia matukio na ghasia za kisiasa zilizoanzia Tunisia na sasa Misri, inashangaza kuona magazeti Tanzania yasivyotoa kipaumbele kwa habari za matukio ya kisiasa yanayoendelea Misri, ninachojiuliza wahariri wa magazeti hawaoni umuhimu wa matukio ya Misri ama watanzania hatuna haki ya kupashwa habari za kimataifa? Tukumbuke chanzo cha ghasia hizi ni mwanachi wa kawaida mfanyabiashara ndogondogo kujiwasha moto Tunisia akipinga vitendo vya kidhalimu alivyotendewa na askari, matukio kama haya ni mengi Tanzania kila kukicha utaona askari na mgambo wa halmashauri wakidhalilisha wananchi wanapojitafutia riziki, magazeti yetu yanapaswa kuwa huru kwenye utoaji wa habari kwa maslahi ya jamii nzima.