Kulikoni magazeti ya Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulikoni magazeti ya Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chama, Feb 2, 2011.

 1. c

  chama JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wakati dunia nzima ikifuatilia matukio na ghasia za kisiasa zilizoanzia Tunisia na sasa Misri, inashangaza kuona magazeti Tanzania yasivyotoa kipaumbele kwa habari za matukio ya kisiasa yanayoendelea Misri, ninachojiuliza wahariri wa magazeti hawaoni umuhimu wa matukio ya Misri ama watanzania hatuna haki ya kupashwa habari za kimataifa? Tukumbuke chanzo cha ghasia hizi ni mwanachi wa kawaida mfanyabiashara ndogondogo kujiwasha moto Tunisia akipinga vitendo vya kidhalimu alivyotendewa na askari, matukio kama haya ni mengi Tanzania kila kukicha utaona askari na mgambo wa halmashauri wakidhalilisha wananchi wanapojitafutia riziki, magazeti yetu yanapaswa kuwa huru kwenye utoaji wa habari kwa maslahi ya jamii nzima.
   
 2. m

  mukamba New Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  baadhi magazeti na vyombo vingine vya habari vinamilikiwa na mafisadi. hivyo wahariri wavyombo hivi hawako huru. wanabana kutoa habari ambazo zinaweza kuchochea mageuzi ya kisiasa. hili ni tatizo kubwa. Hongera mwanahalisi na raia mwema - YOU ARE DOING ALOT KULETA MAGEUZI!!!
   
Loading...