kulikoni kisiwa cha Mafia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kulikoni kisiwa cha Mafia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by wa hapahapa, Oct 7, 2012.

 1. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,550
  Likes Received: 1,601
  Trophy Points: 280
  Mafia ni kisiwa ambacho kipo kusini mwa Tz.
  nipo hapa kwa muda usiopungua mwezi sasa ...
  shughuri kubwa hapa ni uvuvi wa samaki mbalimbali wapoambao ni hotcake
  yaani wanavuliwa kamba koch,pweza nk.

  Pia zipo shughuri za kitalii maana lipo eneo limetengwa maalum kwa Hifadhi ya Bahari likiwa
  chini ya Marine Park ambalo watalii huwa wanafanya michezo ya baharini .
  pamoja na utalii ni mategemeo ya watu wa hapa baaba ya muda kutakuwa na uzalishaji wa mafuta na gesi
  kwa maisha ya baadae (haijulikani mradi hutakamilika lini)

  KULIKONI MAFIA
  Tokea nifike hapa nilikuta lipo tatizo la mgao wa umeme...
  nilipouliza wenyeji wangu wakaniambia ni kawaida kwa mgao huo hasa ikitokea
  1. mafuta ya kuwasha mitambo (generators) ya umeme ikiwa ndio ipo katika taratibu za kuagizwa au kuletwa
  hapa kisiwani...... maana yanatoka DSM kwa kuletwa na meli ya mafuta
  2. kukiwa na tatizo la kiufundi pia itabidi kuwepo na mgao kwa muda hadi vifaa (Spares) vitakapo agizwa
  kutoka DSM... nayo hii itachukua hadi siku tatu ndio mambo yatakua sawia(c mnajua tena safari + posho)

  hizo ndio sababu zinazochelewesha maendeleo lakini cha kushangaza umeme huo unawaka ktk vitongoji
  vitatu tu (kilindoni, kulungeni na kigamboni) ambavyo ni sawa na eneo la Sinza ya Dar ki ukubwa.

  labda kosa c la management ya tanesco ya mafia, labda kosa ni kampuni na viongozi wake wa dar, labda c kampuni wala viongozi wake.. kosa litakuwa la wizara husika lakini huwezi kujua moja kwa moja tatizo ni nini.....au nani.

  yapo mambo mengi sana nimeyaona katika kipindi cha mwezi mmoja niliokaa huku... nitawajulisha moja hadi jingine
  wana jf ............ watu wa huku ni wakarimu sana na khs samaki wapo wa kila aina .
   
 2. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Vipi Maji yanapatikana kama pale jumba jeupe ,magogoni au?
   
 3. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,550
  Likes Received: 1,601
  Trophy Points: 280
  si sawa na pale jengo jeupe....
  huku maji yanatoka kwa mgao ni asubuhi na jioni..... pengine wakijisahau kufunga ndio tunapata muda wote

  pia Mafia ni kisiwa mama chenye visiwa vidogo nane hivi wanavyokaa watu. . vingine ni Juani,Jojo, Chole,
  Jibondo, Bwejuu,Banja,Shungimbili na Nyororo.

  kali zaidi ni maisha ya hapo Nyororo... kisiwa ambacho wanaishi wanaume tupu hamna hata dalili ya kwepo
  mwanamke hapo... inavyosemekana wapo wanaume wasiopungua 500.
   
 4. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,550
  Likes Received: 1,601
  Trophy Points: 280
  pia na wasiwai maji yenyewe hayajakuwa treated na dawa..

  wakati mwingine nahisi Mola anaipenda tz kuliko nchi zingine
  maana ni watu wachache sana wenye health or lyfe assurance lakini tunaishi kwa matumaini japo
  probability of death occurance ni 70-95% depend on place or where you are regards causes
   
Loading...