Kulikoni bodi ya kahawa Moshi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulikoni bodi ya kahawa Moshi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by staff, Jul 23, 2011.

 1. s

  staff New Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]WAFUATAO WANATAFUTIWA MAKOSA ILI WAFUKUZWE KAZI BODI YA KAHAWA.
  [/FONT]
  [FONT=&quot]
  Wafuatao wanatafutiwa au kuundiwa makosa ili wafukuzwe kazi na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania yenye makao yake makuu Moshi.

  1. Kilian Massawe - Huyu alishafukuzwa kazi mapema kabisa KOSA LAKE inasemekana lilikuwa kutokurudisha masurufu ya safari,2.Kuchakachua mishahara ya wafanya kazi wakati akiwa Mkurugenzi wa fedha. Kesi yake inaendelea mahakamani mjini Moshi.

  2. Leopard Taso Mukebezi – KOSA LAKE – 1.Alihoji kwa nini fedha zinahamishwa toka kwenye matawi ya Tanga na Dar wakati matawi hayo yanajitegemea. 2. Kujihusisha na michezo Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Tanzania halafu anaacha kufanya kazi za shirika.

  4. Desdery Mboya – KOSA LA 1.Alimshauri Mkurugenzi Mkuu kuwa asitoe waraka wa kuuza kahawa za wakulima bila kujali reserve zao Mkurugenzi Mkuu akakataa akalazimisha ziuzwe matokeo yake zilipata bei ya chini sana na wakulima walikataa kuachia kahawa zao na ndipo ikabidi ziuzwe upya kwenye mnada uliofuata. Moto huo ulikuwa mkali sana kati ya wakulima na Bodi ya kahawa. Kumburu akapeleka swala hilo kwenye bodi ya wakurugenzi na Mwenyekiti ambaye ni Bw Pius Ngeze wa kikao hicho aliwaambia wakurugenzi kuwa makosa hayo yalifanywa na Muuzaji mkuu wa kahawa na kusababisha bw Kumburu kukatisha safari yake nchi za nje UK. Akaamuru aliyefanya makosa hayo Bw Mboya apewe barua ya onyo kali.Bw Mboya ambaye pia alikuwa kwenye kikao hicho akasimama na kuelezea wajumbe wa bodi kuwa huo ulikuwa uongo mtupu na kwamba Bw Kumburu hakuwepo safarini alikuwa ofisini na ndiye aliyeandika waraka huo. Mwenyekiti akaikaushia na kwenda kwenye hoja nyingine haraka. Kosa lake la 2. Ni kongea ukweli kwenye vikao kuhusu maswala yahusuyo masoko ya kahawa ndani na nje ya nchi pia alishawahi kukaimu mkurugenzi wa masoko kwa miaka kama nane hivi na kabla mkurugenzi mkuu Bw L.D.Omar Kusitaafu alikuwa anamwachia ofisi kukaimu kwa muda mrefu.Pia kwa sasa anaonekana kuwa tishio kwa mkurugenzi wa masoko wa sasa bw Primus Kimaryo ambaye ni swahiba mkubwa sana wa bw Kumburu kwa kuwa walitokea wote Kilicafe.Alisha jengewa mazingira ya kuitwa mwizi kutokana na mashine ya kukaanga kahawa iliyokuwa imeazimwa na kampuni ya kuuza kahawa ya DORMAN akituhumiwa kuwa alikuwa amewauzia kinyemela huku mashine hiyo ilikuwa imeazimwa kwa DORMA kwa kibali cha mkurugenzi mkuu wakati huo bw Omar. Cha kushangaza ni kwamba kwenye mafaili yote copy ya barua hiyo hakukutwa lakini kwa kuwa Mungu anajua kulinda watu wake Bw Mboya alikuwa na copy yake na ndicho kilichomsaidia.Sasa hivi anahusishwa na kutoa kahawa malipo yakaenda kwa kikundi kingine kimakosa ingawa waliopelekewa fedha hizo wameshakiri kimaandishi kuwa walipokea na wamekubali kuzirudisha.[/FONT]


  [FONT=&quot]
  4. Goodluck Sipira – Mwonekano wake (Personality), kwa umma na Elimu ya juu (M.Sc ukilinganisha na B.SC aliyo nayo Mkurugenzi Mkuu) inampa tabu sana pamoja na kumweleza ukweli bila kumwogopa ndio kunakomponza mpaka kufikia kutaka kumtimua. Alishamsingizia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kudai kuwa Sipira ndio kikwazo cha kukataa kutoa leseni za Cherry kumbe sio kweli ni yeye Kumburu ndio alimwambia asizitoe.

  5. Kaberwa Rutachweka – KOSA LAKE LA 1.Huyu bwana alipogundua kuwa mshahara wake umechakachuliwa alipohoji ndio ikawa kosa lake ingawa alirudishiwa mshahara wake halali ulioidhinishwa na wizara kuanzia hapo ndio ikawa kosa lake. KOSA LAKE LINGINE NI Kuongea ukweli kwa mambo yanayoendelea bodi. Amekuwa akibadilishiwa vyeo ambavyo havieleweki ni msomi mzuri sana na masters 2 za kilimo.
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Kosa ni kuandika barua ya kutaka kujua wadhifa na wajibu wake ndani ya Bodi baada ya kuhamishiwa Makao makuu akitokea Bukoba ambako alikuwa ameajiriwa kama Reginal Manager na kuteremshwa cheo kinyemela bila ya kuidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi Kosa la 3 ni kuulizia sababu za kubaguliwa kimaslahi kwa kulipwa posho ya mafuta tofauti na cheo kilichoidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi.Baada ya Mkurugenzi mkuu kuona wanamnyima haki ndipo akarubuni Bodi ya Wakurugenzi wakaidhinisha hicho cheo kwa kuback date ili aendelee kumnyima haki Bw. Rutachweka. [/FONT]
  [FONT=&quot]
  6. Melikiadi Massawe - Mahusiano yake na wizara kutokana na kukahimu nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Kahawa kwa miaka 6 ndio kosa lake kubwa, na utumiaji wa gari nzuri ndio vilivyompelekea kutafutiwa visa ili amfukuze kazi. Bw kumburu alipoona hampati akaamua kumhamishia Tarime tawi ambalo kisheria na kikanuni halipo na ukizingatia uzalishaji wa kahawa kwenye wilaya hii ni mdogo sana kiasi cha tani 1200 kwa mwaka ili aache kazi mwenyewe.Sasa hivi amewekea mtu wa kumchunguza ambaye ni dereva wake na hivi sasa yuko hatiani kutiwa hatiani.

  7. Alex Peter[/FONT]
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Mahusihano yake ya karibu aliyokuwa nayo na mkurugenzi wa fedha aliye fukuzwa kazi ndicho chanzo cha kumtafutia visa vya kumwandikia barua nyingi za maonyo ili ajenge msingi wa kumuwinda amfukukuze kazi.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  8. Edwin Hamaro[/FONT]

  [FONT=&quot]Mahusihano yake ya karibu aliyokuwa nayo na mkurugenzi wa fedha aliye mfukuza kazi ndicho chanzo cha kumtafutia visa vya kumwandikia barua nyingi za maonyo ili ajenge msingi wa kumuwinda amfukukuze kazi.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  9. Rogatus Meela – KOSA LAKE LA KWANZA NI – Inasemakana ana Mahusiano na Kampuni kubwa ya ununuzi wa kahawa ya Rogers and Mann kampuni ambayo ilipeleka ushindani mkubwa wa kununua kahawa wilayani Tarime na kusababisha wakulima wa kahawa wilayani humo kufaidika sana mpaka hivi leo ndio iliyompelekea bwana huyu kutafutiwa visa vya kutaka kufukuzwa kazi kwa kuwa kampuni hiyo imekuwa kwa muda mrefu ikituhumiwa na washindani waliokuwa wilayani huko kwa muda mrefu kudai kuwa kampuni hiyo inaharibu utaratibu wa ununuzi wa kahawa wilayani kitu ambacho sio cha kweli.. Pia kiongozi wa idara aliyokuwepo ya masoko Kimaryo alishawahi kusikika kua hataweza kuiiongoza idara hiyo kama huyu bw ataendelea kuwepo kwa kuwa hatawaliki Baada ya kusingiziwa vitu vya uongo vingi alihamishiwa idara ya Masoko na kupelekwa idara ya operation na hapohapo kuhamishiwa mkoani Kigoma na kupewa cheo cha Kukaimu afisa uendelezaji wa zao la kahawa mkoa wa Kigoma mkoa ambao uzalishaji wake wa kahawa kwa mwaka ni tani 1200 kama Tarime. Uhamisho wake mpaka leo haujaeleweka maana haukupitishwa kwenye menejiment ya shirika.Hayo yote ni ili aache kazi mwenyewe Inasemakana sasa bado anawindwa vibaya sana.

  10. Elia Mkwawa[/FONT]

  [FONT=&quot]Uzoefu kazini unampoza kwani bwana Kumburu baada ya kuamua kuleta watu wake toka Technoserve inabidi amtafutie kisingizio cha kumbadilisha. Makosa kidogo yaliyofanywa na karani yakapelekea kuwalipa zaidi wakulima tofauti na kiasi cha kahawa waliyouza amewatwisha mzigo na ameisha wafikisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi ili awafukuze kazi.Kama ni makosa hata Mkurgenzi anatakiwa kuwajibika kwa kuidhinisha malipo.

  11. Elias Temu
  Uzoefu kazini pamoja na kuwa kiongozi wa wafanyakazi ambapo amekuwa akimwambia Bw. Kumburu ukweli ndivyo vinampoza kwani bwana Kumburu baada ya kuamua kuleta watu wake toka Technoserve huyu bwana alionekana kuongelea swala hilo kwa kuhoji inabidi naye amtafutie kisingizio cha kumbadilisha. Makosa kidogo yaliyofanywa na karani na wao wakashindwa kuona hii hitilafu yakapelekea kuwalipa zaidi wakulima tofauti na kiasi cha kahawa waliyouza amewatwisha mzigo na ameisha wafikisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi ili awafukuze kazi. Hata hivyo hatua zilichukuliwa kurekebisha hitilafu hii Idara ya fedha ikazembea kuchukua hatua. Kama ni makosa ya uwajibikaji hata Bw. Kumburu naye pia angetakiwa kuwajibika kwa kuidhinisha malipo.Usemaji ukweli wake ndio unaomponza kwa kuwaeleza ukweli wawapo vikaoni ila inasemakana hatima yake iko karibusana[/FONT]

  [FONT=&quot]
  12. Frank Mrema[/FONT]

  [FONT=&quot]Alituhumiwa kwa kosa la kuambiwa na kukubali kumpa mkubwa wake wa kazi bwana Daudi Kiangi LPO ili aijaze ( Bw. Kiangi ni mjumbe wa Menejimenti na ndiye alikuwa na details za hiyo LPO). Huyu naye alikuwa karibu na Mkurugenzi wa fedha aliyemfukuza.Na pia kwenda kudai malipo ya jingo toka CRDB Bank ya Dola takribani 75,000 sasa sijui ilitakiwa akachukue mwenyewe Kumburu au sijui alitaka kitu gani.

  13.
  [/FONT][FONT=&quot]Esther Mlay.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Alituhumiwa kwa kosa la kuwalipa wajumbe wa Bodi kwenye hati ambayo wachapaji hawakuandika jina. Hata hivyo malipo yenyewe hakulipa yeye binafsi. Kinachomponza ni kuvuja kwa taarifa za uchakachuaji wa pesa za shirika anatuhumiwa kwamba yeye ndiye anayezivujisha.Hivi sasa yuko hatarini kufukuzwa kazi saa yoyote[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kumekuwa na matukio mengi katika bodi ya wafanyakazi kunyayaswa na kuonewa pale utakapoonekana unaufahamu wa kazi au jambo lolote lile.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Wafanyakazi hata wakifanya kosa kidogo yeye hajui taratibu anachojua yeye ni kufukuza na alishasikika akisema hata wakienda mahakamani mpaka hizo kesi ziishe yeye atakuwa ameshaondoka kwenye Bodi hiyo.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Ila anachotaka hasa nikuhakikisha watu aliowakuta bila kujali familia zao au muda wa mtu aliokaa kazini anataka kuwafukuza na kuwaharibia maisha yao bila kujali.(inawezekana sio mwanadamu ni mnyama fulani hivi)[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Alipopata cheo hicho wale aliyokuwa akifanya nao kazi huko MCCCo LTD NA Kilicafe walianza kuwaeleza wafanyakazi wa bodi kuwa mmekwisha huku wao wakisherekea kuondoka kwake huko kilicafe[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Mara kwa mara ameshasikika akisema yeye haogopi mtu hata waziri kwake hamjali kwa kuwa waziri na yeye wote ni wateuliwa na Raisi.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Akishirikiana na Mwenyekiti walimpa Waziri wa kilimo taarifa za uongo kwenye mkutano wa wadau wa kahawa uliofanyika Mkoani Morogoro mwezi May 2011 na waziri kujikuta akitoa hutuba ambayo baadae ilibidi isitangazwe kwenye vyombo vya habari vyote kwa kuwa ingeweza kumuharibia kazi,na hayo waliyafanya kwa manufaa yao wenyewe na manufaa ya Kilicafe na Techno serve.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Alishawahi kukaa kwenye kikao cha wafanya kazi akasikika akimwambia Mwenye kiti Bw Piusi Ngeze hawa hata siku moja hawaninyimi usingizi analala kwa raha kabisa hata kwa ni wajinga mno.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kutokana na aliyomfanyia waziri sasa hivi anahaha kutafuta utaratibu wa watu kumwombea msamaha kwa waziri na hivi sasa akijua kuna kikao ambacho waziri atakuwepo anajishauri jinsi kwenda kwenye kikao hicho kule kwenye mkutano Bukoba hakwenda kwa kuwa kulikuwa na maofisa wa wizarani akamtuma DCDO mkutano huo. [/FONT]
  [FONT=&quot]SASA UKITENDA SI LAZIMA UTENDWE?[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kama hujawahi kukutana na mtu muongo kwenye maisha toka uzaliwe karibiana na huyu mtu utatapika au utakimbia [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Barua alizoandikiwa toka wizarani tunaomba waziri zifanyie kazi vizuri maana zitakuwa na uongo mwingi sana usiamini alichokujibu .[/FONT]
  [FONT=&quot]Na pia tunaomba kujua je Mwenyekiti wa bodi Bw Pius Ngeze ni mtendaji mkuu au ni mwenyekiti wa vikao,maana tunashangaa wakati wote yuko Moshi na ofisi amepewa ghorofa ya pili na awapo Moshi hulipwa per diem zake kama kawaida.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Tunamuomba Waziri wa Kilimo, chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe aingilie kati na kurudisha morali ya wafanyakazi wa bodi vinginevyo wafanyakazi wataingia katika mgomo baridi ambao utaathiri sekta ya kahawa nchini.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  k
   
 2. m

  matengo Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli nami na support Wizara ya Kilimo iingilie kati kwani huyu bwana anajicussion nyuma ya Mwenyekiti ili amlinde kwa kutumia mahusihano yake. Hana lolote analolifanya zaidi ya Kutangaza tenda, kuajiri kila kukicha( wengi wao wakikimbia baada ya kuona ubabaishaji wake) kupaka majumba rangi , kuwazungusha Wakurugenzi wa Bodi ulaya na kuandika mikakati mizuri bila utekelezaji.
  Watendaji amewapack ofisini kuandika taarifa na hao aliowapeleka kwenye Guantenamo alizozifungua hawafacilitate wafanye kazi. Wakuu wa Idara amewafanya mizuka kwani amewatia woga hawana maamuzi yoyote bila yeye. Anajitia kujua kila kitu wakati hajui kitu, akisaidiwa kuambiwa ukweli anaaza bifu.
  Mh. Waziri tunaomba uingilie kati, tuma watu wako wachunguze kwani Bodi ya Kahawa inaonekana kama amebinafsiwa Kumburu. Serikali ikichelewa yatakuja tokea kama yaliyotokea mpaka jengo la Bodi likawekwa rehani kwenye benki ya Exhim.
   
 3. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,754
  Trophy Points: 280
  Im from moshi im aware of that board and some board members,one of them is rogath meelaa,i knew something fishy was going on at that board and now here we are! Loool
   
 4. H

  HakiMoja Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  My friends. Mr Kamburu is another Jairo. He is abusing his own profession and responsibilities. The prime minister may face a question related to this scandle by thursday in the instant question session. What is special to this guy? Kiburi cha kuwanyanyasa watanzania ametoa wapi? Asome Katiba ya nchi ajue kwamba kila mtanzania anastahili kufanya kazi na kulipwa ajira stahili. Ninawasiwasi pia na huyo mwenyekiti wake labda ananjaa sana. Kwanini anajidhalililisha kufanya kazi ambazo hastahili. Naunga mkono aundiwe tume huru.
   
 5. M

  Mama yoyo New Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kupitia hii post nimegundua tatizo kuwa ni kwanza, uzoefu na elimu ndogo aliyo nayo mkurugenzi wa Bodi ya kahawa ukilinganisha na majukumu yanayomkabili. Cha kujiuliza alipataje nafasi hiyo wakati sera ya Wizara ya Kilimo hata maafisa kilimo wa wilaya sharti wawe na Masters. Anawaogopa wataalam wazoefu na au wanaomzidi elimu, hivyo anawabughudhi ili wakimbie. Pili hata Mwenyekiti atakuwa anachangia kwani inaonekana ameshindwa kusimamia na kutoa maamuzi yasiyokuwa ya upendeleo ili kulinda maslahi yake matokeo yake wafanyakazi imebidi wakimbilie wizarani kuomba msaada. Ushauri wa bure kwa serikali ni kuwa makini wakati wa kuteua watendaji wakuu wa mashirika makubwa kama hili linalochangia kiasi kikubwa katika uchumi wa taifa.
   
 6. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Peleka Majungu Street karibu na Kiusa, mwaandishi wa makala haya ni huyu hapa 4. Goodluck Sipira – Mwonekano wake (Personality), kwa umma na Elimu ya juu (M.Sc ukilinganisha na B.SC aliyo nayo Mkurugenzi Mkuu) inampa tabu sana pamoja na kumweleza ukweli bila kumwogopa ndio kunakomponza mpaka kufikia kutaka kumtimua. Alishamsingizia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kudai kuwa Sipira ndio kikwazo cha kukataa kutoa leseni za Cherry kumbe sio kweli ni yeye Kumburu ndio alimwambia asizitoe.
   
 7. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  he we ndo Kumburu nn?
   
Loading...