Leo nilienda Ofisi ya Air Tanzania ofisi ya Mwanza kwa ajili ya kufanya booking ya safari yangu kwenda Dar es salaam tarehe 4.3.2018 saa za mchana. Nilichoambiwa sijaamini mpaka sasa. Niliambiwa kwa tarehe hiyo na muda huo kwa safari moja tu (one way) kwenda Dar es Salaam ni Tshs.410,000 nikamuuliza mara mbli mbili Je ni kweli akaniambia ndo gharama yenyewe na kama nikitaka nilipe Tshs. 350,000 kama safari yangu itakuwa muda wa jioni. Mwanzoni tulielezwa kuwa Mwanza to Dar kwa safari moja ni kati ya Tshs.160,000 - 180,000. Tuliaminishwa kuwa ATCL itakuwa na gharama nafuu leo hii toka Mwanza kwenda Dar ni Tshs.410,000. Hii inatisha na kama ndo mwendo utakuwa hivyo Fastjet itazidi kutawala anga ya Tanzania. ATCL jirekebisheni.