G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Ukweli ni kuwa kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Mwanza Dr. Faisal kumeambatana na ukiukwaji mkubwa wa maadili ya utumishi wa umma! Dr. Faisal amefukuzwa kazi kwa kuegemea ushahidi wa upande mmoja huku chanzo cha kufukuzwa kwake kikiwa hakijawekwa bayana! Hili ni tatizo kubwa!
Tunaambiwa kuwa Rais Magufuli alichukuwa uamuzi wa kumfukuza kazi mtumishi huyo wa umma muda mfupi sana baada ya kupokea simu kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza ndugu Magesa Mulongo!
Kimsingi Rais alitakiwa kupima kwa kina aina ya mtu anayempa maelezo! Magesa Mulongo siyo siri amekuwa kiongozi wa "hovyo hovyo" kwa jamii hivyo mashitaka yake kwa Rais yalitakiwa kupimwa kwa umakini mkubwa! Kulitakiwa subira na uchunguzi wa kina hasa ikizingatiwa historia mbaya aliyo nayo ndugu Mulongo!
Tunathubutu kusema kuwa huenda kulikuwa na uonevu mkubwa dhidi ya hili! Tutamsaidia Dr. Faisal kutinga mahakamani ili kuweka heshima kwa jamii! Kulinda utu na heshima ya kila mmoja wetu!
Tungependa kuona haki inatendeka na utu unalindwa dhidi ya hili!