Kulifunga Kanisa Si Sawa

CONTROLA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2019
Posts
7,087
Reaction score
23,867
Yawezekana amekosea, Yawezekana hayuko Sawa,Yawezekana kuna mahali kamkasirisha Yeyote katika Watawala

INapaswa atafutwe yeye,muhojiane nae mkitaka Mfanyeni mtakavyo

Lakini kulifunga Kanisa/Nyumba ya IBADA si sawa

Lile si KANISA tu ile ni sehemu watu wanaenda kukusanyika kuongea na Mungu wao, ni eneo la kiroho na wala sio nyumba ya mtu binafsi.

Haki Hamna katika Hili, kuzuia watu kufanya ibada kisa mtu mwingine hii sio Sawa.

Sidhani kaam ingekua ni Msikiti pangekua kimya hivi, ila kwakua wakristo hawana Kauli wamenyamaza.

Kanisa ni Mali ya Washarika na wala sio mali ya Mchungaji ndio maana tunatoa sadaka zetu zifanye kazi ya Mungu.

Mchungaji ni Msimamizi Tu lakini si mmiliki wa KANISA, kulizunguka kanisa kwa magari na askari na bunduki ni kuwanyima HAKI ya kufanya IBADA wananchi.

wananchi hawa hawatendewi haki mnawakosea.

Fungueni KANISA ondokeni eneo la kanisa

Mtafuteni Mtu wenu huko nnje ya Kanisa, nendeni kawekeni kambi nyumbani kwake si mnapajua ila ONDOKENI kanisani

Watu tunataka KUABUDU, tunataka Uhuru wa ibada.

Mnavunja Sheria.
 
CCM kawaida huwa wana panic haraka sana, ni sisi tu watanzania tumeregea kupindukia
 
Kwa pesa wanazoiba acha wawe wakali na wauawaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…