Kulea kabinti ni mtihani mkubwa . . .

Kulea kabinti ni mtihani mkubwa . . .

mmh,pole inasikitisha,na hawa wanaume hawa,huwa hawana huruma kwa kweli.huyo ni mdogo bado kwa kujiingiza katika mahusiano.wa kukomeshwa ni huyo kijana
 
Dah kwl hatari itabidi tutafute sayari nyingine kwa ajili ya malezi ya watoto wetu
 
....hahah...kama usingehitimisha na hicho kichapo cha 160,00/- nami nilikuwa nakusoma tu unyuzi huu unataka kuupeleka wapi na hako kabinti ka 13yrs!...

Nawe 'kemea' huyo pepo mchafu anayekufanya uangaliane nako hako kabinti macho kwa macho na hasa ukikatazamia kakuogope....'kemea!' hiyo curiosity na utemee mate chini...astaghafirullah...



Imepita kama miezi kama mi 2 hivi tangu haka kabinti kaanze vituko vyake.
'
Ni katoto kadogo tu,kamezaliwa mwaka 2000!
'
Kalikua kananiheshimu sana,kila nikikutana nako au nikienda kwao kwaajili ya kuonana na baba yake ili kuzungumza mambo mbalimbali kalikua kananiamkia kwa adabu mpaka niliwahi kumpongeza baba wa haka kabinti kwa kukalea vizuri.
'
Lakini nikaanza kuona salam hakuna,nikienda kwao nikikakuta hakaningopi tena.
'
Nikikaita kukauliza kama baba yake yupo,nikiwa nazungumza nako hakapepesi macho wala kuangalia pembeni kama nilivyokazoea,kananiangalia moja kwa moja machoni.
'
Nilikua sitaki kuamini nilichokua nafiria mpaka jana usiku nilipopita nyumbani kwao na kukuta kanapewa kichapo na mama yake eti amekakuta na fedha taslim sh 160,000!
'
Kichapo kilipozidi kakasema kana mahusiano na jamaa mmoja kaliemtaja jina na kakasema uhusiano wao una miezi 2 sasa na huyo jamaa ndo amekua akikapa fedha hizo.
'
Mama yake kidogo azimie!
'
Nikagundua ndo maana haka kabinti kalikua kamebadilika.Tena huyo jamaa ana hela hivyo hakakuona faida ya kuniheshimu tena.
'
Sasa hii ni laana kabisa,huwezi kuamini ukikaona kalivyo,sijui huyu mwendawazimu alivutiwa nini kwa haka katoto!
'
Inaonekana katika mambo magumu siku hizi ni kulea mtoto wa kike!
 
Ni muhimu sana kwa wazazi kujitahidi kuwa karibu na watoto wenu. Malezi yanaanzia nyumbani, usiwape jukumu la kukulelea mtoto wako watu wengine.
Ongea nae, mpe nafasi ya kumsikiliza, jua changamoto zake zinazomkabili, mshilikishe Mwenyezi Mungu na inshaallah utafanikiwa!
 
Tusali na kufunga kwa ajili ya watoto wetu...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom