Kulea kabinti ni mtihani mkubwa . . .

Kulea kabinti ni mtihani mkubwa . . .

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,914
Imepita kama miezi kama mi 2 hivi tangu haka kabinti kaanze vituko vyake.
'
Ni katoto kadogo tu,kamezaliwa mwaka 2000!
'
Kalikua kananiheshimu sana,kila nikikutana nako au nikienda kwao kwaajili ya kuonana na baba yake ili kuzungumza mambo mbalimbali kalikua kananiamkia kwa adabu mpaka niliwahi kumpongeza baba wa haka kabinti kwa kukalea vizuri.
'
Lakini nikaanza kuona salam hakuna,nikienda kwao nikikakuta hakaningopi tena.
'
Nikikaita kukauliza kama baba yake yupo,nikiwa nazungumza nako hakapepesi macho wala kuangalia pembeni kama nilivyokazoea,kananiangalia moja kwa moja machoni.
'
Nilikua sitaki kuamini nilichokua nafiria mpaka jana usiku nilipopita nyumbani kwao na kukuta kanapewa kichapo na mama yake eti amekakuta na fedha taslim sh 160,000!
'
Kichapo kilipozidi kakasema kana mahusiano na jamaa mmoja kaliemtaja jina na kakasema uhusiano wao una miezi 2 sasa na huyo jamaa ndo amekua akikapa fedha hizo.
'
Mama yake kidogo azimie!
'
Nikagundua ndo maana haka kabinti kalikua kamebadilika.Tena huyo jamaa ana hela hivyo hakakuona faida ya kuniheshimu tena.
'
Sasa hii ni laana kabisa,huwezi kuamini ukikaona kalivyo,sijui huyu mwendawazimu alivutiwa nini kwa haka katoto!
'
Inaonekana katika mambo magumu siku hizi ni kulea mtoto wa kike!
 
Mlezi wa Kweli ni MUNGU tu, sisi wengine wasindikizaji bytheway huyo ni mkubwa mwenzio huyo Mpwa, shauri yako....
 
Pasua kichwa hiyo...!! Watakatifu wote mtuombee....!!!
 
Inataka moyo, sala, na strictness!...
Bila hivyo unawalelea walimwengu, na utakuja kuwa discouraged, na haya magonjwa ya presha ndo yanaweka kambi miilini mwa wazazi!!
 
swali la kizushi.....

Unataka kabinti kaangalie pembeni aka kapepese macho ili iweje? Jamaa kapepesewa macho kaishia kumhonga 160k shaurilo.


Anyway....
Malezi ya miaka hii ni magumu si wa kike wala wa kiume. Tena ukiwa na wakiume hulali kihofia kasiharibiwe na mabazazi.

Mungu atulindie wanetu
na wazazi tuwe karibu nao kuwaongoza kwa hekima za Mungu
 
Yani sikuizi mungu atustiri na hawa ma binti zetu lakini ....
 
Mlezi wa Kweli ni MUNGU tu, sisi wengine wasindikizaji bytheway huyo ni mkubwa mwenzio huyo Mpwa, shauri yako....

Khaaaaaaaaa!!!!
 
malezi na maadili ya watoto wa kike ni magumu mno! tuko zama za digitali na dot.com! ukiona katoto ka kike hakakusalimii tena ujue bikira haipo tena! wakati wewe unakaogopa kuwa ni katoto kuna zee zima kuzidi umri wako wewe linakasaula! tena kabinti kakiona huna mpango nako kanakuona huna mpango na umepitwa na wakati!
zaidi sana wazazi tuzidishe bidii ya malezi kulingana na mafundisho ya kiroho na kuwaombea watoto wetu!
 
Sasa hii ni laana kabisa,huwezi kuamini ukikaona kalivyo,sijui huyu mwendawazimu alivutiwa nini kwa haka katoto!
'
Inaonekana katika mambo magumu siku hizi ni kulea mtoto wa kike!

Ni kweli Eiyer, lakini nafikiria jambo gumu zaidi ni sisi wanaume kubadilisha tabia za kuwatokea mpaka watoto wetu, lol!
 
Last edited by a moderator:
Ukiwa na mtoto wa kike mzuri! Nunua gobore halafu fanya test kwa kunguru au paka! Heshima mazima mwanao atakuwa vizuri kabisa!
 
swali la kizushi.....

Unataka kabinti kaangalie pembeni aka kapepese macho ili iweje? Jamaa kapepesewa macho kaishia kumhonga 160k shaurilo.


Anyway....
Malezi ya miaka hii ni magumu si wa kike wala wa kiume. Tena ukiwa na wakiume hulali kihofia kasiharibiwe na mabazazi.

Mungu atulindie wanetu
na wazazi tuwe karibu nao kuwaongoza kwa hekima za Mungu
mwali umenifanya moo udundie kulia na ushoto kama ule wa jerry.

malezi ni magumu sana sio kwa watoto wa kike tu bali hata wa kiume.

jana kuna mtu nilikuwa naongea nae kumsimulia kisa cha mwanangu aliniambia
'''ivi hujui kwamba kwasasa mwanao uyo wa kiume ndo rjali kweli kweli??'' hakuishia apo akasema tena usisangae anaweza akazini ata na waalim wake manake anayo (huyo mtu) experience ya kutembea na waalim wake toka yuko primary, sec na chuo kikuu. na hawa wote ndio walikuwa wakimtengenezea mazingira yaani walimtega mwanaume.
 
Huenda anapewa free yakutosha hivyo yupo katika stage ya kujaribu kila kitu, bila mzazi kumkemea yawezakana akapotelea huko mazima.

Tuje kwako sasa; Ulitaka apepese macho halafu itokee nini?? Uje kutuambiaa "ooh, mtoto kabadilika nikiongea nae anarembulia, sijua kafunzwa na nani tabia za ajabu namna hii".
 
Nimeshtuka hapa utadhani mimi ndio mama wa huyo binti masikini, kabinti kangu kamezaliwa 2001 Mungu tuepushe nilianza kuzembea kusali sasa namrudia Mungu kwa kishindo maana hii ni hatari
 
Ni kazi, ila kazi kubwa siku hizi ni watoto wa kiume kwa haya mambo ya kishetani wanayoiga.....(Ushoga)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom