Kulalamika mno bila kijiongeza humpoteza uliyenaye/unayemtarajia

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
Kwenye mahusiano ni haki kila mpenzi kuzungumza aonacho hakipo sawa katika upande wa mwenziye. Wapo wasiojua kuzungumza badala yake huwa ni watu kulalamika, kila siku ni watu wakulalamikiana juu ya hili na lile.

Sauti ya mwanamke au mwanaume huwa ni ya malalamiko kuona, kuhisi na kuishi kama mtu asiye na furaha katika ulimwengu wa mapenzi.

Ni jambo jema kuonyesha unaumia na kupaza sauti lakini ni mbaya sana katika mapenzi usipojiongeza, uweza kumpoteza uliyenaye au unayemtarajia kwa haya:

Uonyesha wewe siyo mtu muelewa. Malalamiko yanapozidi ikiwa kila mara unarudia na katika mazingira yale yale na katika jambo lile lile.

Hii uonyesha siyo mwenye uwezo wa kumsoma uliyenaye na kuishi kwa mazingira yake au kusubiria mpaka pale atapokuwa katika muda sahihi na utayari wa mwenzio. Mfano: wapo wanaopenda muda mwingi kuwasiliana kwa simu au sms bila kujali nafasi ya mwenziye, wivu kuzidi nk.

Huwezi kujitoa kwake. Malalamiko yanapozidi na ikiwa hali halisi unaiona, na juhudi za mwenzio unaziona, lakini unalalamika juu ya jambo fulani halijakamilika. Mfano, anatoa huduma zote lakini hana muda nawe, ahadi azitimii, umegundua mapungufu lakini uachi kulalamika. Anayelalamika hawezi kujitoa kifedha, kimali, kinguvu na kimawazo.

Hauna ndoto naye kimaisha. Anayekutambua na kuwa na ndoto moja nawe, kila siku utazama hatua zako, kulalamika kupo lakini katika njia ya mazungumzo yenye kujenga.

Malalamiko ya wenza kuona mwenziye anachelewa kufika au amezidi kufika,kinyume na matakwa, uonyesha huna malengo sawa naye. Kwenye ndoto moja changamoto zote huwa ni zenu na siyo kulaumiana. Unakosa subira na umuoga wa maisha.

Muongo. Unapolalamika sana pia uashiria wewe ni muongo na umezoea kitonga, kama vile kila muda huna, kwa wengine unatoa pesa ila kwa mwenzio unalia huna, unamali nyingi ila kila muda huna, huna bikra ila utaki kukutana na mpenzio. Huku pia uweza onekana ni kuigiza.

Mzigo kwake. Huwezi kufanya kitu, huwezi kubadilika nk. Unapokuwa ni wa kulalamika sana, inafika muda mtu anakuchoka na kuona wewe ni mzigo kwake. Wewe ni mzigo kwamba uishi kulalamika huna shukrani.

Wewe ni mbinafsi. Kila muda unataka yako tu yaende, yako yasikilizwe, yako tu yatimizwe, hata kama ni tatizo limetokea na mume au mke akajali kulitatua bado ukija utalalamika, japo lina wahusu wote. Kusaidia familia ya mke au mume tayari unalalamika.

Mvivu wa fikra. Huwezi kufanya mpaka usukumwe kwa kulalamikiwa kama punda uchapwe fimbo ndio uelewe, kila siku unapoteza, una tia hasara nk.

Ni haki yako kulalamika ila unapaswa kutafakari na kuwa na mipaka kwa unacholalamika, kuna vitu unapaswa kuvitambua kuacha kulalamika kama

*Hulka ya mwenzio

*Hali yake

*Urefu wa mkono wake

*Mahusiano yake na watu na nduguzo

*Hali yake ya afya

*Majukumu aliyonayo

Usipoweza kuvitambua hivi, kulalamika kwako kutakuwa ni kelele, huna tofauti na ndege aina ya Kanga, anapolia hakuna wa kujua hali yake iwe njaa au kuna hatari ni bora lalamika kama kuku, hana tabia ya sauti ya ovyo akilia walio pembeni watashtuka siyo bure.

Lazima atumbue mengine unapaswa kujiongeza, anayekupenda anakutambua na kukupa roho kile inapenda ni wajibu wake. Hata wewe unayelalamikiwa usipojiongeza hayo hapo juu yatakuhusu tena haswa, kuishi kama roboti usiyejali hisia na maisha mwenza wako ni upumbavu.

Na mwandishi mmmuhumba
@ tiktok mmmuhumba

IMG_20221228_141118_298.jpg
 
Back
Top Bottom