'Kulala Kitanda Kimoja na Mpenzi Wako ni Hatari Kwa Afya Yako' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Kulala Kitanda Kimoja na Mpenzi Wako ni Hatari Kwa Afya Yako'

Discussion in 'JF Doctor' started by Mbonea, Sep 24, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Thursday,
  Watu wengi hujihisi kupata usingizi bora wanapolala kitanda kimoja na wapenzi wao lakini wanasayansi wanaonya kwamba kulala kitanda kimoja na mpenzi wako ni hatari kwa afya na huweza pia kusababisha uhusiano usambaratike.


  Wanasayansi wa nchini Uingereza wameonya kwamba kitendo cha wapenzi kulala kitanda kimoja ni cha hatari kwa afya zao na pia huweza kuhatarisha uhusiano wao.

  Wanasayansi hao wamesema kuwa kitendo cha kulala kitanda kimoja humsababishia mtu kupata usingizi duni na hali hiyo inaweza kusababisha magonjwa mbali mbali yanayotokana na ukosefu wa usingizi kama vile magonjwa ya moyo na dipresheni.

  Wanasayansi hao walisema kuwa kwa wastani wapenzi wanapolala pamoja huwa na usingizi duni kwa asilimia 50 kwasababu ya kuamshana amshana na hali hiyo huwa tofauti wakati wanapolala peke yao.

  Watu kukoroma, kugonga gonga meno na kujigeuza geuza kitandani, kuamka usiku kwenda ****** ni miongoni mwa sababu zinazowanyima wapenzi usingizi bora.

  Wanasayansi hao walisema kuwa wapenzi kulala kitanda kimoja huchukuliwa kitamaduni kuwa ni kuonyesha mapenzi na upendo wakati kitendo cha wapenzi kulala vitanda tofauti huonekana si jambo sahihi katika tamaduni.

  Wakiongea katika tamasha la sayansi la Uingereza, wanasayansi hao waliwashauri watu wachukue hatua mapema kabla ya afya zao kutetereka au uhusiano kuvunjika.

  Dr Neil Stanley, mtaalamu wa mambo ya usingizi toka hospitali ya chuo kikuu cha Norfolk and Norwich University ambaye hulala kitanda tofauti na mkewe alisema " Usingizi ni kitu chenye uchoyo, hakuna mtu anayeweza kushea usingizi".

  Akiongelea majaribio ya kisayansi waliyoyafanya kwa pea 40 za wapenzi Dr Stanley alisema "Watu hujihisi wanapata usingizi bora wakilala pamoja lakini ushahidi wa kisayansi unaonyesha tofauti".

  Kama haiwezekani kulala vitanda tofauti, Dr Stanley alitoa ushauri wa kununua kitanda kikubwa zaidi na kila mtu atumie shuka yake.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kila unachoposti Mbonea kiliishajadiliwa hapa JF.....unachokifanya ni kama self masturbation...unajiridhisha weye mwenyewe!
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,476
  Trophy Points: 280
  Inaongeza idadi ya posts mkuu. Ushasahau kuna kumtafuta mwanaJF wa mwezi?
   
 4. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ha ha ha...self service sio..he he he I love JF
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  eeeh wewe unakatisha tamaa jamani
   
Loading...