sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,687
- 1,111
Watanzania kwa nini tunalumbana kwa kukosa maarifa,tunapigania haki ya mchanga je haki ya madini haituhusu,madege yana beba madini yetu kila kukicha bila udhibiti hatuoni ila mchanga tunatolea mapovu.
Kwa nini tusipitie upya mikataba iliyofanywa ki Karl peters tukaona wapi tumekosea,kuzuia michanga ndiyo tija ikiwa mikataba ina ruhusu,turudi kwenye mikataba tuangalie tena na tena wapi tulikosea.
Tuna gas inayoendelea kuvunwa huko,tumejiridhisha mikataba ya uchakataji gas ina maslahi kwa taifa au tuna utazama mchanga kwanza.
Tumefanya uchunguzi kupitia kamati ya prof. Mruma,tabia ya uchunguzi ni kugusa sehemu zote mbili,upande wa mtuhumiwa na upande wa anayetuhumu,je kamati iliwafikia watuhumiwa kuwachunguza,na kama haikuwafikia ni kwa nini?
Rais kateua kamati mbili,kamati moja imethibitisha yanayosemwa,kamati ya pili inaendelea na uchunguzi,kamati ya pili ikija na taarifa tofauti na kamati ya kwanza ilihali tumeshatoleana mapovu,tutaiamini taarifa hiyo?
Tumekuwa wepesi wa kukurupuka bila kuvuta subira kwa kuainisha taarifa zote mbili za kamati ndipo tufanye maamuzi,maamuzi ya kukurupuka yanaweza kuligharimu taifa na kuvunja mahusiano ya kibiashara.
Tulikuwa tuna kimbilia nini ikiwa hatujajiridhisha kwa taarifa ya kamati nyingine.
Kamati ya jaji Bomani ilianisha mambo mengi sana kuhusu mustakabali wa madini yetu na kutoa mapendekezo kama ifuatavyo;
1.Kuwapo mfumo imara wa sheria utakaofanya uwekezaji katika shughuli za madini ufanyike kufuatana na sheria za nchi zinazosimamia uwekezaji kwa ujumla badala ya mikataba maalumu na mwekezaji mmoja mmoja
2. Mikataba binafsi iruhusiwe pale tu ambapo uwekezaji ni wa kiwango cha dola za Marekani milioni 200 au zaidi
3. Mikataba itakayoingiwa ni lazima ipelekwe bungeni kwa taarifa; Sheria ya madini ifanyiwe marekebisho ili iweke vipengele vyote muhimu vinavyohusu uwekezaji katika sekta ya madini ili kuwa na sheria inayojitosheleza
4. Mikataba iwe wazi kwa wananchi na ipatikane katika ofisi za mikoa, wilaya na halmashauri ambako migodi ipo
5.Mikataba yote haifanani. Mikataba yote ifanane na kuwe na model agreement ambayo itakuwa sehemu ya sheria ya madini
6.Msamaha wa ushuru wa mafuta isipokuwa kwa mafuta yatakayotumika kwa uzalishaji wa umeme unaotumika migodini tu; Gavana aachiwe nafasi ya kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria
7.Asilimia 60 ya fedha inayotokana na mauzo ya madini irejeshwe nchini kwa ajili ya matumizi ya ndani
Pamoja na mapendekezo hayo serikali haikuona umuhimu wa kuileta mikataba ile,leo serikali inakuja kienyeji kuzuia bila kuangalia uwezekano wa kulisimamia jambo hili kisheria kisha kama kuna ukweli wowote tuzuie kisheria.
Tumekuwa wepesi sana wa kukurupuka katika dhana nzima ya rasilimali za nchi bila tafakuri ya kina,mathalani mchakato wa uchakataji gas ulianzishwa kabla ya nchi haijatengeneza sera ya gas,mikataba ya gas tusipokuwa makini nayo itatuingiza kwenye wimbi la sakata la madini,kwa kuwa mikataba hii ilizingatia sera ya madini ambayo ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo.
Kuna haja sasa kupitia upya mapendekezo ya jaji Bomani kwa kuipeleka mikataba yote bungeni ili mgawanyo wa rasilimali za taifa uweze kuinufaisha nchi yetu.