Kuku, Kunguru na Tai

mushijcob

Senior Member
May 20, 2015
104
69
Ukiona tai na kuku wapo pamoja wanatafuta chakula ujue tayari tai ameshapoteza mwelekeo. Mwanamafanikio mwenzangu ni kwamba kuku hana msaada wowote kwako juu ya kupaa kwako juu ya kwenda juu zaidi.

Wewe kama mtu unaetaka kufika mbali unaetaka kupaa juu kama tai tafuta tai wenzako kuku atafundisha mbinu za kukaa hapa hapa chini, kuku atakufundisha jinsi ya kufukua chini. Hana cha kukusaidia juu ya safari yako ya mafanikio. Kua makini na jaribu kutambua kuku ni yupi na tai ni yupi.

Wakati unatafuta tai wenzako usisahau kuna kunguru pia kunguru wanatamani kufika juu lakini wanavutwa na vitu vilivyopo huku chini jaribu pia kua makini maana unaweza kumkimbia kuku ukajikuta umetua kwa kunguru. Kunguru tabia zake zinafahamika anapenda kula majalalani.

Unaweza ukawa unajidanganya kwamba unaweza kuwabadilisha wakawa kama wewe ila ukweli ni kwamba wewe ndio utakaebadilishwa jitahidi kukaa mbali nao haijalishi utakua na mpweke kiasi gani ndio mafanikio yalivyo.

Pia wanasema ndege wafananao wanaruka pamoja, tukikuona na kuku tunajua wewe ni kuku, tukikuona na kunguru tutajua wewe ni kunguru, tukikuona na tai tutajua na wewe ni tai mwenzetu.

Tai hakati tamaa kirahisi hata kama kuna upepo mkali na mawingu havimfanyi arudi chini.

Changamoto kubwa tuliyonayo ni kwamba kipindi hiki tuna tai wengi ambao bado hawajajitambua kama wao ni tai. Ni imani yangu kwamba kama umeweza kusoma hapa uko kwenye kundi la Tai hongera sana na endelea kupambana safari bado ni ndefu.
Asante sana na Karibu
©Jacob Mushi
 
Ila kunguru anaishi maisha marefu sana kuliko hao ndege wengine, yaani ukiangalia lifespan ya kunguru ni mara mia ukilinganisha na kuku na ni mara hamsini zaidi ukilinganisha na tai sasa hapo nani mjanja zaidi
 
Asante mtoa mada, wengi wetu tunaishi chini ya viwango,tunaishia kufukuafukua chini kama kuku wakati ni tai...

Tunatoa mpenyo kuruhusu wengine kuona sifa nzuri ndani yetu ambazo sisi wenyewe hatuzioni kwasababu tu ya hofu/kutojiamini. Mambo mengi tunayoyatamani kwa wenzetu yako ndani ya uwezo wetu iwapo tutathubutu na kuondoa hofu....

Shida iliyotuzunguka wengi ni hofu ya kukosea,ni bora mtu aliethubutu kuingia ulingoni akapigwa kuliko yule muoga mana yule amejifunza tayari japo amepigwa.... Kwenye ulingo kupigwa ngumi na kudondoka chini sio fedheha ni sehemu ya mchezo,fedheha ni kuendelea kubaki pale chini.

Wanasaikolojia wanamsemo wao "The best way to avoid mistake is to gain experience and the best way to gain experience is to make mistakes"
 
Asante sana Valentina
 
Asante Kwa ujumbe mzuri mkuu, bahati mbaya watakuja shallow thinkers na kuanza kuleta habari za njiwa, bata nk wakati mada imelenga binadamu wapambanaji.!!!
Utawaona tu.
 
well said mkuu. Nimeongeza kitu kichwani. Naambatana na Tai wenzangu kuanzia sasa
 
Asante mtoa mada, wengi wetu tunaishi chini ya viwango,tunaishia kufukuafukua chini kama kuku wakati ni tai...

Tunatoa mpenyo kuruhusu wengine kuona sifa nzuri ndani yetu ambazo sisi wenyewe hatuzioni kwasababu tu ya hofu/kutojiamini. Mambo mengi tunayoyatamani kwa wenzetu yako ndani ya uwezo wetu iwapo tutathubutu na kuondoa hofu....

Shida iliyotuzunguka wengi ni hofu ya kukosea,ni bora mtu aliethubutu kuingia ulingoni akapigwa kuliko yule muoga mana yule amejifunza tayari japo amepigwa.... Kwenye ulingo kupigwa ngumi na kudondoka chini sio fedheha ni sehemu ya mchezo,fedheha ni kuendelea kubaki pale chini.

Wanasaikolojia wanamsemo wao "The best way to avoid mistake is to gain experience and the best way to gain experience is to make mistakes"

Sio lazima kuji associate na waliofanikiwa tu ili nawe uwe na mafanikio,wakati mwingine tunatakiwa kukaa chini na walio fail ili kujua ni wapi walipoanguka ili kutufanya tusipitie mapito yao...
 
Upo sawa ndugu...

Muhimu ni kuangalia tumezungukwa na watu wa aina gani
 
Sio lazima kuji associate na waliofanikiwa tu ili nawe uwe na mafanikio,wakati mwingine tunatakiwa kukaa chini na walio fail ili kujua ni wapi walipoanguka ili kutufanya tusipitie mapito yao...
To be a millionaire, you must burn the bridges of mediocrity. This means that you're ready to erase the average people, places, and things, even if they are family or friends. However, this can only happen when you start to align yourself with experts. When you get closer to industry leaders, these average people will automatically dissipate in your life.
 
Kama ilivyo kwa hisabati,kwamba uwezzo wa kutunga swali unatakiwa kuwa wa kiwango cha juu kuliko namna ya kulikokotoa kupata jibu ndivyo ilivyo pia mbinu za kujikwamua kutoka umasikini zinatakiwa kuwa za kiwango cha juu kuliko namna ya kuendelea kuogelea kwenye umasikini...

Yapasa kufahamu pia umasikini na utajiri ni swala la akili na namna tunavyoi tune,kama mtu hana nidhamu ya maisha hata angeji associate na benki kuu iwe role model wake bado ataendelea kuwa kapuku tu!
 
Ni kweli utajiri unaletwa na tabia na umaskini hvyo hivyo ukikaa na matajiri utaiga tabia zao
 
Nina jamaa yangu mmoja alisoma mambo ya Procurement na supply kwa kiwango cha Shahada ya kwanza, kapata ajira Mantrack ngozi pale Nyerere road kwa Wahindi sijui na kwa aina ile ya biashara seem alikutana na watu wenye exposure na wenye ukwasi wa kueleweka but guess what! Dogo alipiga mzigo pale kapata mshahara wa say miezi nane kaacha kazi kaenda mkuranga huko kununua mashamba na kuanza kilimo, leo huyu dogo anaitwa mzee,si kwa umri, bali kwa uwezo wake alionao kupitia kilimo! Hapa ndipo napoamini kwamba maisha ni Doctrine na falsafa yake tunapishana nayo kwenye jamii tunayoishi kila siku muhimu ni kuwa na utambuzi na kuwa na nidhamu ya ya maisha!
 
Back
Top Bottom