Kukosekana kwa chanjo ya Gumboro

Mrlee

Member
Aug 31, 2017
5
3
Mimi ni mfugaji wa kuku na kuna tatizo la kukosekana kwa chanjo ya Gumboro sokoni, wafugaji wenzangu nyie mnalimudu vipi swala hili?
 
Ni changamoto kweli... mi safari hii imebidi tu niwape dawa za mafua na kuharisha lakini nawaona kabisa hawajakua na vizuri na muda wa kuuzwa umefika... soko safari hii sio zuri kabisa kuku wako wengi sana
 
Hizo dawa za mafua ni mbadala wa gumboro au uliwapa tu,Nina vifaranga 400 ila nimekosa hiyo chanjo, soko lipo kaka muhimu wewe kulitafuta kwa bidii.
 
Hizo dawa za mafua ni mbadala wa gumboro au uliwapa tu,Nina vifaranga 400 ila nimekosa hiyo chanjo, soko lipo kaka muhimu wewe kulitafuta kwa bidii.
Hakuna mbadala kwa duka nililoulizia mimi... ila jaribu kuulizia maduka tofaut tofauti unaweza kuwapa nini badala ya gomboro
 
Nilivyo ambiwa Kwa kawaida hiz chanjo hazina mbadala hiyo kama hawajapata huo ugonjwa nishukuru, wakipata ndy hasara tena.
Ni kweli kabisa mi hapa naunga unga wateja niwatoe hawa maana nawaona kabisa hawako strong sana wasije kunifia
 
Chanjo hii imeadika maeneo mengi, mimi wana week ya tatu sijawapa, nasali watoke salama...
Masoko yapo japo kwa tabu kidogo, tusiache kufuga.
 
Wakuu hivi ni booster gani iko vizuri zaidi kwa broiler... maana kuna mama mmoja kuku wake wakifika wiki tatu tu wako vizuri kuliko kawaida sijui hata anatumia nini
 
Kw
Twanga Jani LA alovera unga wao changanya na maji wape hakika hutajutia sharti maji yasichacbe yani yasilale ukiwa wanakunywa Siku hiyohiyo kwa muda wa week moja kila Siku asubuhi na jioni hutojutia
Asante sana... vp ushawahi kusikia kuhusu kiwachanganyia na mlonge ?
Pia kwa maji ya lita kumi ni kiwango gani cha aloe vera
 
Chukua hata majani makubwa matatu yanatosha ,pia mlonge unasaidia kama kiti yake inapatikana maeneo hayo unaweza tumia
Asante kwa ushauri... sema changamoto hapo ni upimaji wa majani hayo... sasa hivi nna vifaranga 700 j3 vinatimiza wiki yakwanza nikipata source ya mlonge wa kutosha na aloe vera ntavianzishia wiki ya pili
 
Back
Top Bottom