Habarini za usiku huu wapendwa?. Poleni kwa mihangaiko na majukumu ya weekend ya leo, yote kheri tumshukuru Mungu.
Bila kupoteza muda basi niende moja kwa moja kwenye kipengele taja hapo juu.
Ni kwamba mm ni mtoto wa kwanza kwa wazazi wangu(baba na mama) na umri wangu uko kwenye 20's. Baba na mama walikutana shule na wakati huo mama akiwa na umri wa miaka 15 tu na wakati huo akiwa std 7 na mzee wangu alikuwa ameshamaliza std 7 miaka 2 mbele ya mama means mama alipata ujauzito akiwa ana miezi kadhaa tangu aingie std 7, miaka ya 90 hiyo.
Kulingana na mzee wangu mazingira ya kwao kutoruhusu means baba yake kuwa mkali kupita maelezo, alimwambia mama amsakazie mhuni mmoja hv huo ujauzito(Nilihadithiwa na mama mkubwa japo mama hajaniambia). Mama naye alifanya hivyo bila kujua madhara yake baadaye. Huyu baba wa kuuziwa mbuzi kwenye gunia hakujua hivyo alikubali bila pingamizi na akalea ujauzito hadi nilipozaliwa.
Miaka alisonga mbele kwa kasi na ilipofika 1998 huyu mzee wangu wa kufikia alifariki nami nikiwa najua ndo baba yangu.
Mwaka 2002 nilipoanza std 1 ndipo nilipomjua baba yangu mzazi, nilikuwa mtoto lkn sikuweza kumwamini hata aliponifuata shule akiwa na zawadi kedekede, nilikuwa nachukua zawadi zake na kumpelekea mama na kumwambia kuhusu huyo mtu aliyenifuata na kujitambulisha kuwa ni baba yangu, mama aliishia kutabasamu tu.
Ilipofika 2005 ndipo nilipozoea kuwa huyo ndo baba yangu baada ya mama kunithibitishia kwa kinywa chake sababu pia mm na huyu baba yangu tunafanana sana.
Maisha ya upande wa mama hayakuwa mazuri sana sababu km ni kulala njaa, kutembea peku nikiwa naenda shule, kunyeshewa mvua nyumba inavuja, nk. vilikuwa vitu vya kawaida sana.
Upande wa baba maisha yalikuwa vzr yy na familia yake(mke na watoto).
Siku zingine mambo yalipokuwa magumu sana, nilikuwa naenda kwa baba kuomba msaada nakuwa najihisi km ombaomba hasa nikijilinganisha maisha ninayoishi mm na wale madogo wa pale, najisikia vibaya sana na kujumlisha na mishauo ya mama(mke wa baba) hapo ndo nilikuwa nahisi kufa siku si zangu
. Hadi nilikuwa nahisi tu labda baba alikuwa anahitaji nimjue lkn hakuhitaji anisaidie kwa chochote sababu niliweza hata mkuta yy halafu akanionesha dharau waziwazi na wale madogo wakiwepo hivyo nao wakiona hivyo heshima inashuka kwangu.
Baada ya kumaliza std niliamua nihamie kwa mzee wangu baada ya yy kuniambia ili aweze nilipia ada form 1, nilikaa miaka 2 kwa maumivu lkn baada ya hapo nilipata hifadhi kwa msamalia mwema aliyekuwa karibu na shule sababu shule ilikuwa mbali na kwa baba hivyo ilinilazimu nitembee umbali mrefu ili kufuata masomo na nikirudi home jioni napo hamna kupumzika naingia shamba hivyo usiku hakuna hata muda wa kujisomea sababu nakuwa nimechoka sana.
Baada ya kupata hifadhi nilikomaa na shule ingawa baada ya necta matokeo yalikuwa mazuri kiasi ingawa si sana.
Baadaye nilipata mfadhili wa kuja kwenye jiji letu maarufu la Makonda kufanya kazi ambapo kwa sasa niko na maisha yangu angalau si sana najitegemea na kurudi mkoani kwetu huwa naenda mara moja moja kusalimia.
TATIZO;
Kwa sasa shida inakuja yaani nakuwa napretend kuwa niko sawa na mzee lkn roho yangu haipo hivyo, kuongea sawa hata kwenye simu tena tunaweza ongea story za wapi na wapi na kucheka nn na nn lkn huwa nahisi naidanganya nafsi yangu. Na kuongea kwenye simu hadi baba anitafute yeye na kuna muda huwa anajishtukia kwa kuniambia niwe karibu na mkewe(mama wa kufikia) akiamini labda ukimya wangu yy(mkewe) ndo chanzo wakati si kweli.
Kitu kingine nakuwa mpweke kupitiliza means napenda kukaa peke yangu sana hadi muda mwingine sipendi hata kupiga story na watu, naweza nikajifungia ndani nikiwa nipo home bila hata kutoka hata nje na ikitokea akaja mtu kupiga labda story, nitatafuta sababu yeyote hata kujifanya natakiwa nifike mahali ili mradi tu aondoke. Lkn nakuwa na huruma na matatizo ya watu means naweza kulia hata kimoyo moyo sababu ya matatizo ya mtu
Kwa ufupi pia, ni mcheshi sana kwa watu(hadi huwa nasifiwa) lkn nafsi yangu nahisi inakuwa imebeba vitu vizito kuliko capacity yake.
Na napenda utani sana hasa nikiwa maeneo ya kazi na hii ndo maana ya watu kunisifia ucheshi na naamini hiyo hali inaficha maumivu niliyo nayo moyoni.
Ningependa sana kuondokana na hayo matatizo lkn nakuwa nashindwa hivyo msaada wako hasa wa kimawazo unahitajika sana.
Pia hata wale wa matusi karibuni sana.
N.B; Nilichogundua, malezi ya mtoto yanafaa kuhusisha wazazi wote wawili na km kuna tofauti kati ya wazazi bora zikamalizwa haraka sana ili kuweza kumlea mtoto ktk maadili mema.
Asante.
Wako ktk ujenzi wa Tanzania ya viwanda;
DON YRN.
Sent using
Jamii Forums mobile app