Kukosa Hedhi (Amenorrhea) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukosa Hedhi (Amenorrhea)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Sep 18, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Tatizo la kukosa hedhi ni jambo ambalo linawakumba wanawake wengi waliovunja ungo. Aidha suala hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbana nalo.


  Tatizo la kukosa hedhi au amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa (primary) au baadaye kabisa maishani (secondary).


  Primary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo na ambayo huweza kuendana na hali ya kukosa mabadiliko ya kubalehe kama vile kuota matiti au nywele za kinena; au msichana anaweza kuwa na mabadiliko ya kubalehe lakini asipate hedhi.


  Secondary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito, hanyonyeshi, na ambaye hajavuka umri wa kukosa hedhi (menopause) na wala hatumii njia za uzazi wa mpango kama vile sindano au vidonge, na ambaye hapo awali alikuwa akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama kwa miezi mitatu au zaidi.


  Mwanamke hupataje hedhi?


  Ili mwanamke aweze kuwa na mzunguko ulio sahihi wa hedhi, ni lazima matezi yake ya hypothalamus na pituitary pamoja na kiwanda cha kutengeneza mayai ya kike (ovaries) na mji wa mimba (uterus) vifanye kazi zake sawasawa.


  Hypothalamus huchochea tezi la pituitary kuzalisha hormone chochezi ya follicle au follicle-stimulating hormone (FSH) pamoja na homoni ya luteinizing (LH). Hizi FSH na LH kwa pamoja huchochea ovaries kuzalisha homoni za estrogen pamoja na progesterone. Kazi za estrogen na progesterone ni kusababisha mabadiliko katika ukuta wa uterus yaani endometrium ikiwepo kupata hedhi. Ili damu ya hedhi iweze kutoka nje, njia ya uzazi ya mwanamke haina budi kuwa huru yaani isiyo na matatizo yeyote yale.


  Amenorrhea husababishwa na nini?


  Visababishi vya amenorrhea vyaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu, vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi ya mwanamke na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke.


  Matatizo katika mfumo wa homoni: Matatizo katika mfumo wa homoni yanaweza kuwa katika tezi za hypothalamus, pituitary au ovary.

  Matatizo katika Hypothalamus: Matatizo katika hypothalamus yanayoweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi ni pamoja na

  Uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitary

  Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi. Ugonjwa huu

  hujulikana kama Kallmann syndrome
  Lishe duni na utapia mlo

  Uzito mdogo kuliko kawaida (kukonda kwa kupitiliza)

  Matatizo katika tezi ya Pituitary: Vyanzo vinavyohusisha tezi ya pituitary ni pamoja na
  Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu au kwa kitaalamu Prolactinemia. Prolactin

  ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha. Hali ya kuwa na prolactin nyingi katika damu inaweza kutokea iwapo kuna uvimbe unaoitwa (prolactinoma) katika tezi ya pituitary.

  Kuwepo kwa uvimbe mwingine wowote katika tezi ya pituitary.

  Pituitary kushindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa, hususani iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

  Kuharibika kwa tezi ya pituitary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili.
  Kuwa na historia ya kupata tiba ya mionzi inayohusisha tezi ya pituitary.

  Matatizo katika ovary: Vyanzo vinavyohusisha matatizo katika viwanda vya kuzalisha mayai ya kike yaani ovaries ni pamoja na

  Kutozalishwa kabisa kwa mayai (Anovulation)

  Kuwepo kwa kiwango kingi cha homoni za kiume katika damu (Hyperandrogenemia)

  Ovary kuwa na vifukovifuko (Polycystic ovarian syndrome) na kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Haya ni matatizo ya homoni ambayo huwapata baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa

  Kufa na kushindwa kufanya kazi kwa ovary kabla ya muda wake
  Ugonjwa wa kuzaliwa unaoitwa Turner syndrome ambao humbatana na kukosekana kwa ovary au ovary kuwa changa kuliko kawaida, msichana kushindwa kuvunja ungo na msichana kuwa na kimo kifupi kuliko kawaida.

  Ugonjwa huu hutokana na matatizo ya kijenitikia (genetic disease)
  Ukosefu wa kimaumbile wa ovary ambao hutokea wakati wa ukuaji

  Kufa kwa ovary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili
  Historia ya kuwahi kupata tiba ya mionzi au madawa yanaathiri ovary

  Ugonjwa wa kurithi wa Galactosemia unaoambatana na kuwa na kiwango cha juu cha sukari aina ya galactose katika damu

  Matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi: Matatizo ya kimaumbile katika njia ya mfumo wa uzazi wa mwanamke yanayoweza kusababisha ukosefu wa hedhi ni pamoja na

  Mwanamke/msichana kuzaliwa bila kuwa na uke, shingo ya uzazi au mji wa mimba (uterus)
  Kuta za uterus zinazotazamana kujishikiza pamoja

  Utando unaozunguka uke (hymen) kuziba kabisa na kukosekana kwa tundu la kupitishia damu ya hedhi (imperforate hymen)

  Kuwepo kwa utando unaokatiza katika uke unaozuia damu ya hedhi kushindwa kutoka
  Mabadiliko katika mwili wa mwanamke: Mambo yanayoweza kuathiri mwili wa mwanamke na kumfanya ashindwe kupata hedhi ni pamoja na

  Kula kiasi kidogo sana cha chakula kuliko kawaida au kula kupita kiasi
  Unene uliopitiliza au kupungua uzito/kukonda isivyo kawaida
  Uwepo wa magonjwa sugu kama kifua kikuu
  Utapiamlo
  Msongo wa mawazo
  Matumizi ya madawa ya kulevya

  Matumizi ya baadhi ya madawa hususani baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya akili
  Kuwa na hofu iliyopitiliza
  Kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi

  Dalili za Amenorrhea ni zipi?


  Kukosa hedhi siyo ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo kwa tatizo au ugonjwa fulani katika mwili. Kulingana na ugonjwa unaosababisha tatizo hili, kukosa hedhi kunaweza kuambatana pia na


  Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito na wala hanyonyeshi, maumivu ya kichwa na matatizo katika kuona vitu ambavyo kwa pamoja vinaweza kuashiria uwepo wa uvimbe katika ubongo

  Mwanamke kuwa na nywele na vinyweleo vingi mwilini na kuota ndevu kama mwanaume hali inayoashiria kuwepo kwa wingi kwa homoni za kiume za androgen

  Ukavu katika uke, kutoka jasho sana wakati wa usiku, au mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria matatizo katika ovary
  Kuongezeka uzito kupita kiasi au kupungua kwa uzito isivyo kawaida
  Mwanamke kuwa na mhemko kuliko kawaida yaweza kuashiria kuwepo kwa matatizo ya kiakili na kisaikolojia
  Uchunguzi na vipimo


  Msichana yeyote aliyefikia umri wa kubalehe na kuvunja ungo na ambaye bado hajaanza kupata mabadiliko yeyote ya kubalehe katika mwili wake hana budi kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Aidha msichana aliyefikia umri wa miaka 16 na ambaye bado hajaanza kupata hedhi anatakiwa pia kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.


  Kwa wanawake waliokuwa wakipata hedhi kama kawaida lakini ghafla wakaacha kupata kwa muda wa miezi mitatu mfululizo au zaidi nao pia hawana budi kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo hili.


  Vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa kuchunguza sababu za kukosa hedhi kwa mwanamke:


  Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha homoni za FSH, LH, TSH na prolactin ambazo uzalishwaji wake unachochewa na tezi ya pituitary, na pia kupima kiwango cha homoni ya estrogen inayozalishwa na ovary.

  Kipimo cha ultrasound ya nyonga kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo katika njia ya uzazi na pia kuchunguza hali ya ovary.

  CT scan au MRI ya kichwa kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo kwenye tezi ya pituitary au hypothalamus.

  Vipimo vya kufahamu ufanyaji kazi wa tezi ya thyroid

  Kupima damu ili kufahamu kiwango cha homoni ya prolactin katika damu
  Kuchunguza uterus kwa kutumia aina ya X-ray inayoitwa Hysterosalpingogram na kipimo kingine kiitwacho Hysteroscopy ambacho huchunguza chumba cha uterus.
  Matibabu ya kukosa hedhi


  Matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kufanyika nyumbani bila kuhitaji dawa, ingawa pia, kutegemeana na chanzo cha tatizo, yanaweza kuhitaji dawa na hata upasuaji wakati mwingine.

  Matibabu yasiyohitaji dawa


  Baadhi ya wanawake wanaopata tatizo la kukosa hedhi kwa sababu ya kujinyima kula (wanaofanya dieting) na hivyo kupata upungufu wa virutubisho mwilini, wanashauriwa kula lishe bora.

  Baadhi ya wanawake wanaopata tatizo hili la kukosa hedhi kwa sababu ya kuongezeka uzito kupitiliza, wanashauriwa kuwa makini katika aina ya vyakula wanavyokula ili kuwa na uzito unaotakiwa.

  Wanawake wanaokosa hedhi kwa sababu ya kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi wanashauriwa kujiwekea kiasi katika ufanyaji wao wa mazoezi.

  Iwapo kukosa hedhi kumesababishwa na msongo wa mawazo, ni jambo jema kutafuta njia za kushughulikia matatizo hayo na kuyatatua ili kuondoa msongo wa mawazo

  Inashauriwa kutokuvuta sigara na kuacha kunywa kunywa pombe.

  Matibabu yanayohitaji dawa: Matibabu ya kukosa hedhi hutegemea chanzo cha tatizo. Matibabu huelekezwa katika kutibu chanzo, na iwapo chanzo cha tatizo ni matatizo ya kimaumbile, upasuaji unaweza kufanyika. Kwa

  wanawake wenye matatizo ya kuwa na kiwango kingi cha prolactin, daktari anaweza kushauri matumizi ya dawa aina ya bromocriptine au pergolide. Kwa wanawake wenye upungufu wa homoni ya estrogen au wale

  wenye matatizo katika ovary zao, dawa zenye kurejesha homoni hiyo zaweza pia kutumika. Wakati mwingine dawa za uzazi wa mpango zaweza kutumika kurejesha mzunguko wa hedhi na pia kusaidia kuongeza kiwango cha homoni ya estrogen mwilini.

  Upasuaji: Upasuaji unaweza kufanywa iwapo kuna

  Uvimbe katika ubongo unaoathiri tezi ya pituitary na hypothalamus

  Matatizo katika njia ya uzazi ya mwanamke

  Je kukosa hedhi kunaweza kusababisha nisipate mtoto?


  Ikumbukwe kuwa, kukosa hedhi si ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo tatizo hivyo basi iwapo tatizo hilo lina uhusiano na kutunga mimba na kupata mtoto, uwezekano wa kupata mtoto utakuwa mdogo ikiwa tatizo hilo

  halitashughulikiwa. Matatizo kwenye tezi za pituitary, hypothalamus pamoja na ovary ambayo yana uhusiano

  mkubwa na kukosa hedhi, husababisha pia tatizo la ugumba. Iwapo matatizo hayo yatashughulikiwa ipasavyo, uwezekano wa kupata kupata hedhi na hatimaye kupata mimba huwa mkubwa.Kukosa Hedhi (Amenorrhea)
   
 2. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  MziziMkavu, kuna wadada baada ya kujifungua na kumaliza damu ya uzazi ile damu huwa inapotea kwa miezi mpaka mwaka. Wengine wanakuja shtukia wamebeba mimba eventhough hakuwa wanapata hedhi, tatizo ni nini?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Inatokea mabadiliko ya mwili wa mtu tangu alipojifunguwa na kukaa muda mwingi wa kutopotea Damu ya uzazi ikitokea hivyo itabidi amuone Daktari apate kumpa dawa na ushauri mzuri wa kufanya MadameX
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  duu thanks for the use thread maana hapa kuna mmoja huyo alisumbuka sana na hili tatizo kumbe sio ugonjwa bwana..
   
 5. s

  sikati tamaa Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 12, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Na inakuaje mtu akifanya mapenz wengne wanapitsha cku zao yan badala ya kupata hedh tareh 24 unaaenda mpaka tarehe 7 mwez mwingne na asiposex mzunguko unakua kawaida bla kubadilika
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Ni kweli inatokea hivyo kutokana na tendo la sex ndilo linalo msababisha Mwanamke kubadilika kwa siku zake na sio mbaya bora iwe hivyo na awe anafanya tendo hilo la ndoa sex kuliko kutofanya tendo la ndoa kutamletea matatizo mengine kama vile Stress na kuwa na hasira bila ya sababu na mengineyo mengi tu sikati tamaa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. E

  Eselo Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  oh vp kuhsu mwanamke ambaye mzunguko wae wa hedhi ni siku 18'je huyo anaweza kuwa na matatizo,,maana nina rafk yangu ana ilo tatizo,,maana kuconcive kwake imekuwa shida sana,,amepewa dawa ziitizwo pre molut kukomaza mayai lkn hakufanikiwa,,ushauri plz
   
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,952
  Likes Received: 1,825
  Trophy Points: 280
  mkuu huyu rafiki yako anawezekana ana tatizo jingine labda ukomavu wa mayai nk ama pia mwenzie nae ana tatizo ila hajui. mzunguko kuwa mdogo haimaanish kwamba hana fertile period na istoshe dawa hzi primoult-N ni aina ya hormones ambazo mwanamke hupewa ili kuweza kurectify dysifunctional bleeding. na inawezekana kwake ikaanguka kwenye aina hii ya bleed.

  all its all amuone gyn wa ukweli ili amwangalie kwa makini nini tatizo. waweza kukuta ana shida kwenye ovaries pasi yeye kujua.
   
 9. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mimi miss yu bana!
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,952
  Likes Received: 1,825
  Trophy Points: 280
  nipo ma dearest kuna mahali niliteleza kwenye ulezi wa ndoa so nikawa nafeel ma gap sasa yamekaa sawa. si unajua kungwi mzuri huona makosa yake na kuyarekebisha haraka ili wanafunzi wasome ukweli? hahahahahah,

  miss you too.
   
 11. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  thats my girl!unagundua na kuweka sawa fasta!na kila kitu kinarudi on track!kila la kheri mwaya!
   
 12. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,952
  Likes Received: 1,825
  Trophy Points: 280

  thanks ma swthrt. hapa hakuna kulala bana unailinda na kutete ndoa kwa gharama yeyote ile.
   
 13. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  This thread is useful!
   
 14. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280

  NAomba niongezee MziziMkavu, hii mara nyingine hutokea mtu anaponyonyesha, na ni katika mabadiliko ya hormones hizo hizo, na pale mama anapoacha tu kunyonyesha basi na hedhi hurejea tena. inawatokea wazazi wengi sana na sidhani kama ni tatizo, ila inaporudi damu huja kwa wingi sana.
   
 15. jamiif

  jamiif JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 2,417
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  mzizimkavu MUNGU akubariki sana kwa kutoa somo hili muhimu...endelea na moyo huo huo wa kutusaidia Inshaallah!
   
 16. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Na inakuwaje mtu anapata damu nyepesi sana , kidogo na kwa siku chache labda 2 hivi?
   
 17. E

  Eselo Member

  #17
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thank mkuu,,but yye amefanya vipimo vyoote hana tatizo shida nii hiyo tu mzunguko,,atajuaje fertile day maana haelewi cku za fertile kwa huo mzunguko wake,,mwenzi nae hana shida,,msaada ndugu
   
 18. g

  getrude furahia Member

  #18
  Jun 12, 2015
  Joined: Nov 26, 2014
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nimepitiliza siku zangu ilitakiwa nianze tar 9 june lkn hadi leo sijapata na nina uhakika sina mimba, maana nilikutana na mme wangu bila kinga siku ya sita na mzunguko wangu ni siku 26.naombeni msaana jaman kwa anayejua nini tatizo maana sina raha kabisa.na ninanyonyesha bado lkn sijawahi kupitiliza.
   
 19. g

  getrude furahia Member

  #19
  Jun 12, 2015
  Joined: Nov 26, 2014
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nina shida nimepitiliza siku zangu ilitakiwa nipate tar 9 june hadi leo sijapata nimechanganikiwa, japo nina uhakika sina mimba maana nilikutana na mme wangu siku ya sita na mzunguko wangu ni siku 26.sasa sijajua nn tatizo nahitataji msaada wenu. nanyonyesha lkn haijawahi kutokea kupitiliza siku zote hizi
   
 20. kigori one

  kigori one Senior Member

  #20
  Jun 13, 2015
  Joined: Apr 14, 2014
  Messages: 170
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  asante sn mzizi mkavu.. nna tatz hilo kw mwezi Wa pl sasa..nmepma nmeambiwa nna left ovarian cysty kidogo.... lkn tatz hili nlpatw Miez mi4 nyuma nkarudia ultra sound Wakasema lmekwisha..ch ajabu nmepma tn nmeambiwa hvo na kukosa hedh..kabla nilikua nikipata..na niko ktk kipnd cha kutafta mtoto..safar hii inajrudia huku nikpatwa na MAUMVU SANA CHN YA KITOVU....
   
Loading...