Mkuu nakupa sayansi kidogo.
Dawa ya typhoid unayomeza ni wazi ni mojawapo ya antibiotics. Sasa kazi ya antibioitics ni kuua bacteria wanaosabibisha huo ugonjwa. Bahati mbaya ni kwamba mara nyingi dawa hizi hazichagui aina ya bacteria wa kuua. Hivyo wakati ikishambulia bacteria wa ugonjwa huua na kupunguza wale bacteria rafiki wanaohusika na mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na usafirishaji hadi kwenye utumbo mpana. Kwa mantiki hiyo, kuna kuwa na mlundikano wa kinyesi katika utumbo mpana. Kadri kinavyozidi kukaa kwenye utumbo mpana ndivyo ambavyo majimaji huendelea kufyonzwa zaidi na kukifanya kuwa kikavu na hivyo kuwa vigumu kusafiri hadi sehemu ya kutolea haja kubwa.
Kupunguza hali hiyo. Kula vyakula vya majimaji zaidi, mfano; matunda (hasa mapapai na parachichi) na mboga za majani. Pia unashauriwa kunywa maji mengi mara kwa mara. Kama hali haitengemai nenda duga la madawa wakupe dawa za kulainisha choo. Dawa hizo ni group la probiotics. Hizi husaidia kuongeza wale bacteria rafiki wanaohusika na umeng'enyaji wa chakula katika utumbo mwembaba na mpana. Nadhani nimekusaidia kiasi kuelewa chanzo cha tatizo lako.