Kukosa elimu ya darasani isiwe kichaka cha kuficha uwezo wa kufikiri

Gamba la Mbu

Senior Member
Jun 28, 2020
160
417
Salaam!

Imekuwa ni desturi ya Watu wengi kulalamika kuwa kukosa Elimu ya darasani kumewafanya kushindwa kufikia mafanikio fulani fulani hususani ya kiuchumi.

Kwa upande wangu sioni mantiki ya kukwamishwa kuendelea kiuchumi kisa elimu ya kuta nne.

Hebu kwanza tujiulize ni nini kinamfanya mtu afanikiwe kati ya #Elimu na #Maarifa?

Iko wazi kuwa maarifa yanahitajika zaidi ili mtu yeyote atoboe kiuchumi ukiongeza juhudi na nia madhubuti.

Kuna tofauti ndogo sana kati ya Elimu na Maarifa lakini impact yake ni kubwa katika maisha ya kila siku. Hebu tupate hiyo tofauti:

Maarifa:

Hupatikana kupitia mfumo halisi wa maisha ya kila siku ya mwanadamu ( Real life experience) na huongezeka au huzidiana kulingana na muda. Hii ni njia ya utambuzi wa mambo kupitia kufanya kwa vitendo kwa muda fulani na uelewa huongezeka kadri muda unavyozidi kwenda.

Ndio maana huwezi kuwa Mfanyabiashara mwenye mafanikio kama hujawahi kufanya biashara. Vivyo hivyo kwa kada zingine nyingi.

Elimu:

Ni utambuzi wa mambo kwa njia iliyorasimishwa ya kupata maarifa kupitia taasisi rasmi za kielimu ( Formal process of gaining knowledge)

Hivyo tukirudi kwenye mada kuu hapo juu:

Ili mtu ufanikiwe unahitaji knowledge tu kukusogeza kutoka sehemu moja hadi nyingine. Kukosa elimu ya darasani kisiwe chanzo cha kufifisha uwezo wako na kujiona dhaifu mbele ya cheti.

Kuna watu wana maarifa makubwa kuhusu ufundi wa vitu mbalimbali lakini hawajakaa darasani.

Experience huzidisha knowledge.

Kuna hitajika uelewa zaidi kwenye hili. Tafadhali ongezea nyama.

images (14).jpeg
 
Back
Top Bottom