Wadau naomba kuuliza kwa wale ambao wamewahi kukopa Fanikiwa Microfinance,
Afisa Mikopo wao kaja kunitembelea na kunishawishi kukopa kwao. Akanieleza kuwa ukikopa mfano milioni 5 kwa miaka miwili unaweza ukakatwa 393,250 kwa mwezi. Lakini kama nitaweza kurudisha mkopo baada ya miezi sita kabla ya muda wenyewe wa mkopo ina maana nitatakiwa kurejesha (393,250 X 6) Jumlisha (5,000,000 - (393,250x6)). Yaani utalipa ile ile amount ya milioni tano hivyo utaepuka ile riba uliyotakiwa kulipa ndani ya miaka 2.
Je hii ni kweli au kauli za kushawishi tu?