Kukojoa mkojo mweupe {usio na rangi} kwa mienzi 2 mfululizo. Je, ni ugonjwa!

kamwendo

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
897
1,913
Habari za siku Wakuu,


Hope mu wazima na mnaendelea vyema na mihangaiko yenu ya kila siku.

Leo nimekuja kwenu nina tatizo ambalo linanitia wasiwasi kama si shaka kabisa.

Wote tunaelewa kuwa tunakunywa maji ili kuleta uwiano wa ufanyaji kazi mzuri mwilini. Na moja ya kazi ya maji mwilini ni kuondoa na kuchuja sumu na taka nyinginezo.


Imezoeleka kutokana na kazi hiyo moja wapo ya maji mwilini mara nyingi mkojo tunaokojoa huwa na rangi ya njano kutuonesha kuwa maji tuliokunywa yametumika ipasavyo kwa kusafisha figo na tishu nyingine.

Mimi binafsi nimekuwa na wasiwasi juu ya hali yangu ya kukojoa mkojo mweupe kama maji ambao hauna rangi kabisa tena kwa muda mrefu mbaya zaidi hata ukiamka asubuhi, Ambapo kiutaalamu mkojo wa asubuhi ni lazima uwe na rangi.

Ebu niwekeni sawa ndugu zangu , Je nahitaji kumuona daktari haraka iwezekanavyo au ni hali ya kawaida tu!!

By the way sijawahi kuhisi maumivu ya aina yoyote na kwa jinsia mimi ni Me.

Always Be Open to learning.
 
Mkuu Rangi ya mkojo hubadilika kutokana na kiasi cha maji mwilini.
Fuatilia hapa chini
Rangi%2Bya%2Bmkojo.png

1. Mweupe kabisa (Usio na Rangi):
Unakunywa maji mengi kupita kiasi. Ikiwezekana unashauriwa upunguze kidogo

2. Manjano iliyochanganyika na Kijani kidogo: Ni kawaida, una afya na Mwili wako una maji ya kutosha.

3. Manjano iliyo pauka: Upo kawaida tu. Endelea kunywa maji ya kutosha

4. Njano iliyo kolea: Upo kawaida lakini unashauriwa kunywa maji ya kutosha.

5. Njano inayokaribia kufanana na Kahawia au Rangi kama ya Asali: Mwili wako hauna maji ya kutosha. Kunywa maji kwa wingi sana sasa.

6. Rangi ya Kahawia: Huwenda una Matatizo kwenye Ini lako au Upungufu mkubwa wa Maji mwilini. Kunywa maji ya kutosha na umwone daktari kama hali hii ikiendelea kujitokeza.

7. Rangi ya Pinki inayokaribia kuwa kama Nyekundu:
Kama hujala matunda yoyote yenye asili ya uwekundu, basi huwenda una Damu kwenye kibofu chako cha mkojo. Inaweza ikawa sio ishara mbaya. Lakini inaweza ikawa ishara ya ugojwa wa Figo, uvimbe, matatizo kwenye njia ya mkojo, au matatizo kwenye kibofu. Muone daktari haraka iwezekanavyo.
 
Mkuu Engineer2014, Shukran sana maana umeelezea vyema.

Natumaini kuna wengine pia waliofaidika.

All the best Mkuu.
 
Nlichogundua kutokana na maelezo yako ni mimi kunywa maji mengi kupita kiasi kinachohitajika mwilini mwangu.

The Safety Solution ni kupunguza kidogo unywaji wa maji mengi sana.

May God bless you.
 
Unakunya maji mengi recently? U ajiskia kiu mara kwa mara ? Vp kuhusu frequencies za kukojoa?? ...kama frequencies za kukojoa zimeongezeka na unajskia kiubmara kwa mara, its better ikachek sukar...
 
pia mkojo ukiwa wa njano sana, bs ujue unakula sana maembe wew, punguza
 
Unakunya maji mengi recently? U ajiskia kiu mara kwa mara ? Vp kuhusu frequencies za kukojoa?? ...kama frequencies za kukojoa zimeongezeka na unajskia kiubmara kwa mara, its better ikachek sukar...
Ni ushauri mzuri Mkuu, Nitaenda kupima kisukari.

Mara nyingi nakojoa kila baada ya masaa 3 au 4 na maji nakunywa kama lita 2 kwa siku.

Natumaini nimekujibu ipasavyo mkuu.
 
Back
Top Bottom