Kukohoa sana kwenye baridi na mafua makali kwenye joto

Barakaeli174

Senior Member
Aug 2, 2015
171
142
Wataalamu wa Afya naomba msaada,

huwa nikilala nikipigwa na baridi ile inaanza tu basi nakohoa sana ila nikijifunika basi sikohoi tena, hata nikikaa nje na baridi ikianza kuwa kali nakohoa hadi ntakapokuwa nimejifunika vizuri, nikikaa ndani kwenye chumba ambacho hakina hewa ya kutosha nashikwa na mafua makali sana nikitoka nje basi yanaisha hilo hunifanya nilale dirisha wazi. Naomba kujua kama nahitaji dawa au nimekuwa mbovu kwenye mapafu maana wengine hawakohoi kama mm pamoja na kuwa wote tupo sehem moja. Swali lingine je umri wangu wa miaka 38 pia ni rahisi kupatwa na tatizo kama hili. Naomba msaada wakujua kwanini hili linanitokea, na dawa ni ipi ili kumaliza tatizo hili.

Asanteni.
 
Hospital za wezakuwa dalili za pumu

Au kupungua Kwa kinga ya mwili
 
Mkuu Barakaeli174 kwa maelezo uliyotoa hapa, kuna uwezekano mkubwa ukawa na tatizo la pumu.
Tuwasiliane nikutumie dawa ndugu yangu.
Nimesaidia wengi hapa JF, tafuta ule uzi wa asthima hapa utakutana na shuhuda za waliopona kupitia mimi.
 
Sawa lakini hewa nzito maana yake hakuna hewa kabisa ndo maana mafua yanakuwa makali nikikaa sehem kuna hewa kidogo basi yanatoweka nikipigwa na baridi ubavuni nakohoa unafikiri ni dalili za athma kweli
 
Ndiyo mkuu hizo ni dalili zenyewe.
Ukiwa mgonjwa wa asthma huzi kuhimili kukaa sehemu yenye mgandamizo wa hewa, pia baridi kali ikipenya unaisikilizia kifuani so ili kujiweka katika hali ya msawazo inakulazimu ukohoe mfululizo.
Makohozi ya mtu mwenye asthma ni membamba yenye mchanganyiko wa utelezi.
Na siku zote, attacks za asthma huambatana na mafua mepesi na wakati mwingine ukilala unapumua kwa tabu na kunaambatana na miluzi.
Kama ndo unavyote teseka hivi basi wewe ni mgonjwa wa pumu.
 
Mrejesho mkuu

Back
Top Bottom