Kukipenda CCM si kukubaliana na Matusi ya wana CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukipenda CCM si kukubaliana na Matusi ya wana CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Meitinyiku L. Robinson, Apr 3, 2012.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua nimekuwa nikisikia na kusoma juu ya habari za Lusinde viz a viz matusi aliyokuwa akiyaporomosha ila sikutilia maanani nikiamini kuwa yaweza kuwa maneno ya kisiasa ama ushabiki. Ila nikiri leo nimebahatika kusikiliza mwenyewe kwa masikio yangu pamoja na UanaCCM wangu hili la Lusinde kwa kweli halikubaliki hata kidogo.

  Haiwezekeni hata kama kusingekuwa na watoto hayo maneno hayakustahili kabisa kutolewa kwa namna ile; Lusinde kama ana Familia hivi kweli wakisikiliza hayo maneno ataiambiaje Familia yake?? Lusinde kama anakwenda Kanisani ama Msikitini atawaambiaje waumini wenzie ama Paroko, ama Padre ama Shehe??? Hili si Arumeru tu ni jamii nzima ya Watanzania.

  WanaCCM sawa tunaweza thibitisha ama kwa kuweka clip au vyovyote vile ambavyo
  huyo Lema ama Mdee nao wamekuwa wakitukana katika Kampeni lakini je kuthibitisha huko ndiko kutakako sawazisha matusi ya Lusinge??? Mungu tusaidie hivi tunakoelekea ni wapi wazee ni nini hiki jamani????

  Sikuwahi ama kufikiria au kujua kuna siku nitasikia maneno kama haya niliwahi kusikia lugha chafu Arusha Mjini lakini hii imepitiliza......... Khaaaa yani jamaa anafloo kama vile anazungumza peke yake chumbani kwake, hell no tafadhali Livingstone afanywe kila anachostahili thats not fair si tu kwa hao aliokuwa akiwarushia makombora ama akiwajibu bali ni fedheha kwa Chama (Mwenyekiti), Wanachama, Taifa na hilo Bunge letu.....

  Lusinde hustahili hiyo salutation, Lusinde hustahili kuitwa baba, Lusinde hustahili muumini, Lusinde hustahili kuwawakilisha watu wa Mtera!

  Ni mwanaCCM ila wa hoja kuntu na si matusi ya namna ile....
   
Loading...