KUKIMBIA USHINDANI

TAECOLTD

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
1,051
1,835
Habari za muda huu wanajamvi?! Ni matumaini yangu kwamba mpo vyema na mnaendelea kupambana kuzivuka changamoto za kila kukicha.
Nimefuatilia taarifa mbalimbali kuhusu muenendo wa baadhi ya vitu ndani ya Tanzania yetu kuna niliyoafikiana nayo na mengine sikuyaafiki kabisa. Si suala la kuficha sote tunafahamu biashara bila ushindani ni kazi bure ama ushindani wa ndani au ushindani wa nje. Kampuni inaweza kupimwa ipasavyo kulingana na changamoto za ushindani inayokumbana nazo, mfano viwanda vya cement Tanzania vipo vingi tu vya ndani na nje ya nchi kama Twiga, Tanga, Rhino, Dangote, Simba na kadha wa kadha ambapo ushindani huo ndio hupelekea kampuni kukomaa zaidi na kama kamsemo kasemacho "only the strong one will survive" hivyo ushindani ndio hupelekea biashara kujitadhmini zaidi na kupambana ili kulinda wateja wake.
Kuna sheria kadhaa zimenishangaza ambazo zimepelekea sekta kadhaa kukimbia ushindani na kubaki wenyewe sokoni
1) Sukari Tanzania
2) Filamu Tanzania
Kinachonishangaza ni pale movie za nje kupigwa marufuku ili kuinua wasanii wa ndani, kwa jicho la haraka haraka unaweza dhani unasaidia lakini uhalisia ni pigo kubwa sana. Movie za nje kupendwa zaidi inaonesha ni kwa namna gani waigizaji wa ndani wana kasoro nyingi ambazo wameshindwa kuzirekebisha na kushindwa kuwashawishi wananchi kuwapenda. Kupiga marufu uingizwaji wa movie hizi sio kutatua tatizo bali ni kukimbia tatizo ambapo sokoni watakuwa wenyewe wametawala hivyo hawawezi kujirekebisha kwakuwa hawana mshindani yeyote sokoni zaidi yao.
Ingekuwa vyema kukawa na soko huru ambalo lingewapa uchungu hawa wasanii wapambane kutanua kazi zao na kupambana na makosa wanayoyarudia mara kwa mara. Vivyo hivyo kwa kampuni zetu za Sukari, kulipokuwa na Soko huria viwanda vyetu bado vililala na kushindwa kupambana na washindani kutoka nje. Sasa sokoni wamebaki wenyewe pasipo ushindani hivyo itapelekea kushindwa mapema sana kwani binafsi naamini pasipo ushindani kila kitu huaribika.
Hivyo binafsi naona kabisa mambo haya hayajatatua matatizo bali ni kukimbia ushindani jambo ambalo kibiashara sio zuri kabisa.
Asante kwa kusoma makala hii,
Mtenga Gerald
TAECO LTD
TANZANIA
www.facebook.com/TAECO2012
 
Back
Top Bottom