Kukataa hisia za mtu au za kwako mwenyewe

MAMESHO

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
1,366
1,622
Kuna wakati ambapo unakataa hisia za mtu kwa sababu hujavaa viatu vyake. Hii inasababisha azidi kuchanganyikiwa zaidi hata kama ana akili njema.

Wakati mwingine unaweza kujifanyia jambo hilo mwenyewe. Yaani wewe kukataa hisia zako mwenyewe

Jambo hili linachukuliwa kama kawaida lakini sio lenye afya. Na huwa linatokea mara nyingi

Haya ni baadhi ya maneno yanayoweza kutumika mtu anapokwambia jambo au pale unapokuwa na mawazo kichwani

"Sio jambo kubwa sana"
"Hivi unajua kuna wenye hali mbaya zaidi"
"Hii kitu ni kawaida"
"Mbona wanaume wote wako hivyo"
"Yaani ingeweza kuwa mbaya zaidi"
"Dah inatokeaga lakini"
"Endelea kupambana"
"Hapo bado hujaona"
"Subiri yapo makubwa zaidi"
"Kila mtu ana shida"
" chagua kuwa na furaha"
"Acha utoto"
"Samehe na sahau"

Karibu uongezee maneno mengine.

Nilichojifunza mtu anapokueleza jambo heshimu hisia zake usihukumu hisia zake wala za kwako wewe mwenyewe.
Mtu anakuja na shida unambandika shida mpaka anaona afadhali shida yake arudi nayo 😂😂😂😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom