Aaanh asee wapo bhana wanaokaliwa wake kwa waume!!! Mie natoka jamii ya mfumo dume lakini nashukuru nimepita madarasani kiasi kwa hiyo naona jinsi mifumo invyofanya kazi ingawa hatutopata definition moja ya concept hii ila kama "Gender studie" ipo na inakubalika basi kukaliwa pia kupo!!! 1. We mwanaume na sharubu aamke kumi na nusu, deki, vyombo, fua, pika chai, oga nenda job jua na mvua na mkewe mama wa nyumbani hii ni nini kwa mfano??!!! 2. Mama anaamka anaandaa watoto, waende shule aandae chai ya mumewe, atoke mpaka sokoni na beseni anachukua matango, machungwa na mihogo huyo mpaka magerejini anazunguka kuuza na mtoto mdogo mgongoni mume kalala tuu akitoka hapo kucheza bao na karata, abishanie Simba na Yanga tu jioni amarudisha suruali home na anataka wali syenzi type!!! Asee wapo wanaokaliwa wengine kwa mabavu wengine kisaikolojia na wengine vyote kwa pamoja