Kukaa muda mrefu kunasababisha kufa mapema

Kukaa muda mrefu kunasababisha kufa mapema

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842

e, unaketi chini muda mrefu? Hiki ndio unapaswa kufanya.​


ILO

7-8 minutes



Makala hii inaangazia ushauri uliotolewa na Dk. Keith Diaz, Profesa Msaidizi wa tiba ya tabia katika Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Columbia kilichoko nchini Marekani baada ya kufanya utafiki kwa kuangalia hatari za kukaa muda mrefu wakati wa kufanya kazi.
Katika mahojiana na mafunzo kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa yaliyoongozwa na Daktari Mwandamizi wa UN (Afya ya Umma) Dk.Esther Tan , Dkt. Diaz amesema kutokana na uwepo wa janga la Corona au COVID-19 duniani, kufanyia kazi nyumbani kumekuwa jambo la kawaida na kuvuruga mpangilio wote wa maisha. “Hivi sasa kumekuwa na upungufu mkubwa katika viwango vya shughuli za mwili na kumekuwa na ongezeko lisilo la kawaida katika wakati unaotumika kukaa.”

Mwili unavyofanya kazi​

Akielezea namna mwili unavyofanya kazi Dkt. Diaz amesema, ili mwili wote uweze kufanya kazi inahitajika mishipa ya damu kubana na kutanuka ili kuruhusu damu kupita vyema kwenda kwenye ubongo na hii inampa mtu hewa safi na uwezo mzuri wa kushiriki katik shughuli zake, lakini kukaa kwenye kiti kuna punguza hali hiyo.
Amesema mtu akiketi chini muda mrefu kwenye kiti mishipa inashinda kazi kwa ufanisi na hivyo kupunguza kiwango cha damu inayozunguka na pia kuathiri damu inayokwenda kwenye ubongo, pia amesema kwa kawaida tuu namna mtu anavyokaa ni vigumu kwa damu kuzunguka kwa urahisi kutoka miguuni mpaka kwenye moyo na kwenye ubongo. Na hali hii ikiendelea kwa muda mrefu uwezekano ni mkubwa wa mtu kupata magonjwa.
Mazoezi ya Yoga  katika ukumbi wa Baraza kuu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani

Permanent Mission of India
Mazoezi ya Yoga katika ukumbi wa Baraza kuu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani

Kila hatua ina umuhimu​

Shirika la afya ulimwenguni linapendekeza dakika 150 za mazoezi kwa wiki kwa mtu mzima na mtoto dakika 75 kwa wiki. Na pia shirika hilo limesisitiza watu kuangalia namna bora ya kupunguza muda mrefu wa kuketi chini.
Mazoezi yoyote yatakayo sababisha mapigo ya moyo kuongezeka kwa muda fulani ni mazuri kwa afya ya mwanadamu (Cardio exercise), mazoezi hayo yanaweza kuwa kutembea, kuendesha baiskeli, kuogelea, kucheza mpira wa kikapu, soka, au hata kucheza muziki.
Dkt. Keith Diaz amesema shughuli yoyote ya kawaida inayoweza kufanyika kwa kuruhusu viungo kuzungusha damu kwa urahisi ni muhimu “Ukiwa unafanya kazi unaweza kunyanyuka kwenda kuchukua maji, unaweza kupika huku umesimama, kutoka upande mmoja wa nyumba kwenda mwingine hivi vypte vinamchango mkubwa vikijumlishwa kwenye muda wa kufanya mazoezi kwa wiki.”
“Wakati utafiti unaonesha kufanya aina yoyote ya mazoezi kwa dakika 30 kunapunguza hatari ya kufa kwa asilimia 35, aina yoyote ya kuhakikisha mwili unazunguka hatakama ni kufanya shughuli za kawaida za kilasiku za nyumbani kwa muda huo huo kunapunguza hatari ya kufa kwa asilimia 17.”
Hii inamanisha kuwa jinsi mtu anavyoketi chini muda mrefu wakati akifanya kazi, ndio namna anavyokuwa kwenye hatari kubwa ya kufa haraka ikilinganishwa na yule anayekaa muda mfupi.
Shughuli zozote zinazofanywa wakati mtu ameketi chini zina hatari kubwa kwa afya, shughuli hizo ni kama kukaa wakati wakufanya kazi, kukaa kuendesha gari, kukaa kucheza michezo ya kwenye compyuta, au kuangalia runinga muda mrefu.
Watoto wakifanya mazoezi nchini Uzbekistan

Photo: UNICEF/Giacomo Pirozzi
Watoto wakifanya mazoezi nchini Uzbekistan

Ufanye nini ukiwa ofisini na kazi yako ni ya kuketi chini muda mrefu?​

Usipige simu nenda – Badala ya kutumia mitandao ya kisasa ya mawasiliano au simu za mezani inashauriwa baina ya wafanyakazi ni vema kunyanyuka na kwenda kumfata alipo na kuzungumza naye na kurudi katika eneo lako la kazi hii itasaidia kufanya misuli kuzunguka na hivyo damu itatembea vizuri na insulini ndani ya mwili itaunguzwa na kuboresha afya.
Simama wima kwenye vikao - ni vyema kuhamasisha kuwa na tabia yakusimama wima katika mikutano ya majadiliano kazini badala ya kukaa chini muda wote.
Kuwa na sehemu maalum ya kuweka baiskeli ya kufanya mazoezi- Japo haishauriwi mfanyakazi kufanya mazoezi mpaka kutoka jasho awapo kazini lakini dakika chache za kuendesha baiskeli ambayo inaweza kuwekwa mahali popote au ndani ya chumba cha mkutano inasaidia kwa afya.
Panda ngazi- weka utamaduni wak kupanda na kushuka ngazi hata viwango vichache ni bora kuliko kupanda lifti kila siku. “Kama unaenda jengo la 5 panda ngazi mpaka jengo la tatu kisha panda lifti hizo chache zitasaidia kufanya mapigo ya moyo kwenda kasi na kuunguza insulini katika mwili wako”
Kwa wale wafanyakazi waliopo kwenye maeneo ambayo hawawezi kupata kila kitu ni muda mzuri kutumia mitandao ya kijamii na kufanya mazoezi ndani ya maeneo yao, yale ambayo yatasaidia kutembea na kupunguza muda mrefu wa kukaa.
kufanya kazi ofisini inaweza kuwa kumbukumbu ya zamani katika ulimwengu wa baada ya COVID-19

UN Photo/Marvin Bolotsky
kufanya kazi ofisini inaweza kuwa kumbukumbu ya zamani katika ulimwengu wa baada ya COVID-19

Wadawati ya kusimama ndio suluhisho?​

Dr. Diazi amesema kwa sasa baadhi ya ofisi zimekuwa na madawati yanayoruhusu wafanyakazi kusimama wanapofanya kazi. Hata hivyo amesema mpaka sasa bado hakuna utafiti uliothibitisha iwapo kuna unafuu kwa wale wanaosimama ikilinganishwa na wanaoketi chini muda mrefu. “Madawati ya kusimama yamekuwa yakipigiwa chepuo na wafanyabiashara wanayoyauza na sio wanasayansi hivyo hivyo wafanyakazi wasijielekeze kwenye kusimama pekee kama suluhisho la kuketi muda mrefu.”
Ameeleza kusimama muda mrefu kuna madhara makubwa kwenye mwili wa mwanadamu ndio maana watu wanaofanyakazi inayohitaji kusimama wamekuwa wakikabiliwa na magonjwa mbalimbali.
Kuna aina mbalimbali za madawati , yapo yakusimama pekee na mengine yana baiskeli inayomuwezesha mtu anayetumia pia kuweza kuiendesha huku akifanyakazi na hivyo kusaidia misuli kuzunguka. Hata hivyo amesema mpaka hapo utafiti utakapo tangaza umuhimu wake na faida zake ndio atakapoweza kusema kama inaweza kuwa njia mbadala ya kufanya mazoezi na kuketi muda mfupi.
Cyrille Tchatchet asili yake ni nchini Cameroon akifanya mazoezi katika eneo la mazoezi nchini Uingereza, ni mwanamichezo muinua uzito mkubwa akiwa timu ya wakimbizi

© UNHCR/Béla Szandelszky
Cyrille Tchatchet asili yake ni nchini Cameroon akifanya mazoezi katika eneo la mazoezi nchini Uingereza, ni mwanamichezo muinua uzito mkubwa akiwa timu ya wakimbizi

Kwa wanaotaka kupunguza unene wa mwili​

Kwa wale wanaotaka kupungua Dr amesema wanatakiwa kufanya mazoezi kwa zaidi ya saa 200 kwa wiki au mara moja kwa siku na mazoezi mazuri ni yale yakuongeza mapigo ya moyo kama aerobic.
“Mazoezi ni mazuri kwakuwa pia yanafaida nyingine ambazo mpaka sasa hakuna dawa, mfano afya ya akili, utafiti umeonesha mtu mwenye msongo wa mawazo akifanya mazoezi anaweza kuwa na afya bora ya akili ikilinganishwa na yule mwenye msongo wa mawazo na hafanyi mazoezi.



UN Swahili
 
Inawezekana mkuu, ndo maana wakati mwingine ukinyanyuka kwenye kiti miguu hufa ganzi hasa ukiwa kwenye safari ndefu ya basi.
Ushahidi upo kwa mifugo pia ukimfuatilia kuku wa bandani na yule wa kuishi na binadamu wanatofautiana sana
 
Sawa mkuu, mpaka sasa nimetimiza miezi 3, ninauzito was 87kg, nimepunguza sana ulaji was vyakula vya wanga ikiwemo wali, na ugali nilikuwa na uzito was 94kg.
Mungu mkubwa bado napambana.
 
Back
Top Bottom