'Kujipenda' kwako ina maana gani?

'Kujipenda' kwako ina maana gani?

kwakina itafakari

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2018
Posts
739
Reaction score
1,657
Amani kwenu wadau.

Moja kwa moja kwenye hoja kuu, kuna baadhi ya watu wangu wa karibu wamekuwa wakinilalamikia kwamba mimi sijipendi kwa sababu ya vitu kama hivi.

*Kutokunyoa nywele mara kwa mara (napenda kufuga nywele ingawa sio zile za makwapani na sehemu za siri)

*Kutokunyoa ndevu mara kwa mara(sioni tofauti nikiwa na ndevu nyingi,kidogo au nisipokuwa nazo kabisa)

*Kutokuvaa saa (watch)

*Kutokuvaa pamba za bei mbaya especially suti (suits, jumba) siku zote napenda kuvaa simple tu.

Vitu ambavyo me huwa sioni kama vina uhusiano wowote na kutokujipenda zaidi ya kwamba ni "life style " tu ya mtu

Lakini binafsi naamini najipenda sana ndio maana nazingatia mambo kama.

*Kutokuvuta sigara kabisa

*Kutokunywa pombe kulikopitiliza

*Kufanya mazoezi mara kwa mara

*Kutokuwa na mademu wengi (ni aina fulani ya kutokujipenda kwa upande wangu) ingawa uwezo huo ninao

Sasa huwa nashangazwa sana na hawa watu wanaosema eti sijipendi,

Kwani Kujipenda kunafananaje wakuu?

Ndio maana nikaona nijaribu kuwashirikisha wadau hapa juu ya hii kitu Kujipenda,

Kwako wewe binafsi,mwanaume au mwanamke,mkaka au mdada,

Kujipenda inajumuisha vitu kama vipi au mambo kama yapi?

Ili mtu kwako awe kweli anajipenda,inabidi awe namna gani? /afanye mambo gani?
 
Bango nene, watakuja inbobo mkuu, kachil tu pm
 
Bango nene, watakuja inbobo mkuu, kachil tu pm

Duuuh!!!
Hayo mambo sijui ya kusoma between the lines kusema kweli me siyawezi kabisa,maana sometimes yanatia UCHIZI tu

Yeyote aliyeelewa hapo juu,anisaidie na me tafadhari!!
 
Kujipenda kwangu kunamaana ya kuhakikisha naijali akili yangu… akili yangu ikikaa sawa sawia vyengine nitavijali tu maana nakuwa najitambua na kujitambua huanzia kwenye akili so nisipoijali nitajijali vipi..??
 
Je unaijali akili yako kwa namna ipi?
Mambo gani ukiyafanya huwa na maana ya kujali akili yako,kuwa na masaa ya kutosha kwenye kulala?
kufanya mazoezi?ama nini?
 
Ina maana mkuu hata kunukia pia hunukii?
Anyway mwanaume anayenukia ana nafasi ya pekee kabisa mbinguni.
Awe ananukia vizuri kistaarabu.

Sio mtu wa kunukia kwa sana,kisela tu.
Manukato makali huwa yananisumbua sana pua!!
 
Ina maana mkuu hata kunukia pia hunukii?
Anyway mwanaume anayenukia ana nafasi ya pekee kabisa mbinguni.
Awe ananukia vizuri kistaarabu.
mwanaume kunukia?
au ulimaanisha KUNUKA!
 
Ina maana mkuu hata kunukia pia hunukii?
Anyway mwanaume anayenukia ana nafasi ya pekee kabisa mbinguni.
Awe ananukia vizuri kistaarabu.

Tulio sensitive na harufu hiyo mbingu ndo tuisahau sio 😩
 
Ina maana mkuu hata kunukia pia hunukii?
Anyway mwanaume anayenukia ana nafasi ya pekee kabisa mbinguni.
Awe ananukia vizuri kistaarabu.
Mi pia napenda sana kunukia, Nimejikuta nina perfumes kibao na nyingi huwa sizimalizi watu wananiomba naamua kuwaletea nachukua chuma kingine.

most of the times nikifika sehemu lazima wadada waulize ( hasa barbershops) utafikiri nina duka aseee.
 
Back
Top Bottom