Kujinyonga kwa vijana na watoto

Kujinyonga kwa vijana na watoto

twende wote

Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
50
Reaction score
84
Habari wadau,

Niende kwenye mada, Jambo la mtoto au kijana kujinyonga sio Jambo la kumlaumu mtu, Jambo Hilo Ni Jambo linaloenda ki Imani zaidi, (Dini) Jambo hili liko ktk ulimwengu wa roho,

Ninaposema ulimwengu wa roho naomba mnielewe kwa wale wakristo mtanielewa, mwanadamu ameumbwa na vitu 3 ambavyo Ni mwili, (nje) roho, (uhai) na nafsi(mtu wa ndani).

Mwili wa nje hii body yenyewe inaendeshwa na hisia na tamaa za mwili na dunia, lakini nafsi ambae Ni mtu wako wa ndani, yeye anaambatana na Imani ya Mungu, huyu mtu wa ndani ndiye anaekufanya uiamini Dini na uwepo wa Mungu(God existence) Sasa Basi, amini usiamini, shetani yupo.

Kitu anachokifanya shetani Kama mtoto familia yake haijasimama ktk Imani ili awekewe ulinzi wa Mungu, Basi hakika, mtoto huyu anaweza kuibiwa nafsi yake kishetani(kichawi) na akawekewa nafsi ya ki pepo( kijini, kishetani) nafsi ya huyu mtoto itawekwa gerezani, au popote pale, Ali mradi nafsi izuiwe mahali fulani.


Baada ya nafsi kukamatwa pepo mchafu ataingizwa katika body (mwili) hapo Ina maana mtu anakuwa Ni nusu mtu, mtu wa ndani hayumo, hapo ndipo unaweza kuona mtu anafanya tendo moja la ajabu, pasipo kujalisha umri wa mtendaji, maana anaetenda ndani yake, sio ile nafsi, Bali Ni roho ya shetani,

Hapo utasikia mauaji, mtu kuua mpenzi, mtu kaua mzazi, mtu kajinyonga, nk.

Kumbuka roho yoyote Haina umri, roho iwe ya mtoto au mtu mzima, zote Ni roho, cha muhimu ktk maisha Ni hii nafsi, ikishakamatwa na washirikina, wanaweza kuweka kitu chochote ndani ya mtu akawa aidha shoga, msagaji, mvuta bange, mzinzi, mwizi, nk.

Maana unapoenda kutenda uovu kwa yeyote ambae ewahi kufanya, huwa Kuna sauti, inakwambia usifanye, au huwa wanasema roho ilikataa, kinachokataa ndio mtu wako wa ndani au nafsi, yeye Mara nyingi anaongea na Mungu wako, huyo mtu wako wa ndani wapo watu wanaouwezo wa kumchomoa ukabaki kopo, na ukaendeshwa ufanye Jambo lolote ovu watu wakabaki midomo wazi, hili jambo tulikemee majumbani na kulishitaki katika maombi, Dua na Sala, ili hizi roho chafu zituogope.

Mungu awabariki nyoote
 
Hata movie wanazoangalia vijana pia zina sababisha hayo wanaona wanaiga halafu wanajua ni kweli kumbe wenzao wanaigiza tu
 
Nakubaliana na wewe hizo ni roho za kishetani wanapandikiziwa watoto.

Mtoto wa miaka 10 anapata guts wapi za kujinyonga?
 
Back
Top Bottom