Kujinufaisha kupitia bank technical holes. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujinufaisha kupitia bank technical holes.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Developer, Feb 11, 2011.

 1. D

  Developer JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 285
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Wakuu mi nna ka account kangu kwenye benki ya makabwela, NMB. Nakumbuka miezi ka minne hivi iliyopita nilikuwa nna sh alfu 40 , na nilikuwa nimepoteza kadi so nikaenda ndani kwenye counter nikadraw pesa yote(40) halafu ndani ka ya dakika tano baada ya kupewa pesa nikafikiri hawa watakuwa hawaja update database zao. Nikachukua simu yangu ya mkononi nikabofya kupitia NMB Mobile nikafanikiwa kununua vocha za sh 40. Nikajua watanipigia au ntakuta na negative elfu 40 waki upadate system au tu watakata nikiweka pesa. La tofauti na matarajio yangu kuna pesa niliwekewa baada kama ya mwezi na hawajakata chochote mpaka sasa? Swali langu je hii ina madhara gani kisheria za kibiashara incase naongeza ongeza kakiwango na kuzitoa kila mara kwa kamchezo haka? Ukizingatia hatuna mkataba wa kukopeshwa pesa kutoka kwenye hizi akaunti za kawaida?
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  lazima utakatwa tuu
   
 3. D

  Developer JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 285
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  toka mwaka jana mwezi wa nane mpaka leo hawakata, so huoni naweza kula bata kimtindo mpaka waje washtuke, labda uniambie madhara yake kisheria za kibiashara
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu... bank transactions zinafanyiwa auditing and re auditing ... ...auditors wa ndani na nje ..... tena na makampuni yanayokodishwa na makubwa hata miaka mitatu watakata tuu
   
 5. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  kuna jamaa yangu alijikuta anakatwa laki sita alikuwa na kamchezo hako....... siku walipoupdata wakalmba hiyo deni... nusure awe chizi.. chukua kilicho halali yako.
   
 6. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  NMB wateja wengi ,na systems zao haziko makini sana,inategemea sana human interactions otherwise ,report alerts zingekwisha kukamata muda mrefu.ila kumbuka benki na wewe mna mkataba wa kufanya kazi in a good will/faith,
  hivyo bora urekebishe hili swala lako else siku ya kuitwa kuijeleza itakuwa aibu ukizingatia ni elfu 40 tu.
   
 7. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,197
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Thats a very old trick, huwezi kukimbia

  Wadau tupeni new ones
   
 8. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Hapo ujue itakuja kula kwako. Mie niliwahi kuingiziwa mshahara wa mwezi mmoja mara mbili, na nikawa sijui, ila baada ya miezi 7 nikashangaa nilipokwenda kucheck kama mshahara umeingia nikakuta umeingia na kutoka na akiba iliyokuwepo. Kwenda benki kuuliza kulikoni, waka-print statement ya mwaka mzima, ndo nikadundua kuwa kuna mwezi mmoja niliingiziwa mshahara double. Kwa hiyo ikawa maumivu, sikuwa na jinsi, bali kukubaliana na hali halisi. Kosa lilikuwa lao, ila mimi sikujua.
   
 9. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  huo ni wizi. omba waamue kutoenda polisi. utakatwa tena kwa interest.
   
 10. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Toka kadi ilivyopotea ulikaa muda gani ndo ukaenda bank?, cause kwa uelewa wangu kama kadi ikipotea na HUDUMA, ya NMB mobile huwezi kuaccess endapo utakuwa umeriport kuwa kadi yako, imepotea, hii ni kutokana ATM ina connection na NMB MOBILE, usije ukawa unatuingiza chaka kaka, au unataka utumie ujanja huo, cause mi nachojua endapo kama ulifanikiwa kutokana na system misbehave , baada ya siku kadhaa akaunti yako ingeoverdraw, na kama ingeoverdraw, ela yoyote ingewekwa kwenye akaunti yako, ingeclear hiyo OVERDRAW(NEGATIVE BALANCE)
   
Loading...