Kujilipia mahari imekuwa kawaida

Kujilipia mahari imekuwa kawaida

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,933
Reaction score
11,865
Siku hizi imekuwa kawaida mabinti wanapotaka kuolewa huwapa wachumba wao hasa wasio na kipato mahari ili wakalipe kwao, kuna wanawake kama watano nawajua wote wamejilipia mahari.

Sasa najiuliza hapa mwanaume utakuwa na sauti kweli si ukileta za kuleta unaambiwa ondoka, je, mila zetu zinaruhusu mwanamke kujilipia mahari.

Na nyie wanaume mnaokubali kupewa mahari na wachumba hamuoni mnajidhalilisha hivi wanaume tumekuwa adimu kiasi hiki mpaka mwanamke ajilipie mahari yeye mwenyewe ili tu aolewe.
 
bora akupunguzia mahali lakini sio kukulipia, kulipiwa mahali ni mwanamke ni sawa na kutoa rushwa
 
Chochote anachokupa mwanamke huwa kinarudi kwake mara mbili au tatu.....
wanawake ni 'very very smart'

Si wanawake tu, pia wazee, vilema, wasio na elimu kabisa,,,,yaani ni hawaamin kama wanaweza bila kusaidiwa! Na hawaamin kabisa kama nao wanaweza kukusaidia! Ikitokea ukaomba msaada kwa mtu wa aina hiyo basi jiandae kumlipa fadhila 3times or more!!!
 
inategemea na roho ya mtu watu tumeumbwa tofauti. Kuna mwingne akikulipia mahali ni manyanyaso kwenye ndoa lakini mwingne atakulipia na bado atabaki kutambua kuwa yeye ni mke tu nawe ni mume. Inahtaji mwanamke anaejielewa kujua wajibu na majukumu
 
Mwanaume ukisaidiwa mahari maana yake umeoa mke wa kukopa...
 
Toa kitu upate kitu…. Wanawake tuwaache tu ingawa wengi tunawaona kama wajinga hivi lakini wanajua wanachokitaka. Every gift has power to return to the giver.
 
Kwa kawaida mahari hulipwa na wazazi wa mtoto wa kiume. Hata muuoaji kujilipia mahari siyo utamaduni wetu.

Hii ya muolewaji kujilipia mahari haijakaa sawa kabisa. Kama mzazi wako anashindwa kulipa mahari na wewe mwenyewe umeshindwa kumsaidia mzazi wako kulipa mahari basi bora uka negotiate tu uoe kwa mkopo.
 
Faida za kulipiwa mahari na mwanamke ni kidogo ukilinganisha na hasara.

Ni bora kama mwanaume hujiwezi wazazi wa binti wakalijua hilo ili upangiwe mahari kidogo kulingana na uwezo wako...

Kulipiwa mahari na mchumba wako kutakufanya ukose kujiamini hasa inapitokea mkeo amekukorofisha???
 
Faida za kulipiwa mahari na mwanamke ni kidogo ukilinganisha na hasara.

Ni bora kama mwanaume hujiwezi wazazi wa binti wakalijua hilo ili upangiwe mahari kidogo kulingana na uwezo wako...

Kulipiwa mahari na mchumba wako kutakufanya ukose kujiamini hasa inapitokea mkeo amekukorofisha???

kweli kabisa.
 
kwenye mahari sina uhakika ila kujinunulia shela nadhani ishakua kawaida.... ndoa nyingi sa hizi naona mabibi harusi wanazichanga za shela!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom