BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 654
- 1,598
Kama tunavyojua, mara kadhaa tumekuwa tukiwasikia baadhi ya wanasiasa wakidai kuwa wajawazito wanajifungua bure. Kauli hizi zimekuwa zikizua mijadala mikubwa kuhusu uhalisia wake, hasa ikizingatiwa kuwa bado kuna gharama mbalimbali zinazotozwa kwa maelezo kuwa ni michango ya huduma.
Hata hivyo, hali inaonekana kuwa tofauti kabisa kwa wajawazito wanaojifungua kwa upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa kina-mama kuhusu kutozwa gharama kubwa, hali ambayo imekuwa tishio kwa uchumi wa familia nyingi.
Mwishoni mwa mwaka jana (2025), nilipokuwa Muhimbili, nilishuhudia mama mmoja akilalamikia gharama alizotakiwa kulipia kwa ajili ya mdogo wake aliyekuwa amejifungua kwa upasuaji. Hospitali ilihitaji zaidi ya laki sita, ilhali mjamzito huyo alikuwa amepata rufaa kutoka hospitali ya rufaa iliyopo Mkoa wa Dar es Salaam.
Mama huyo alidai alipouliza sababu ya gharama kuwa kubwa, alielezwa kuwa upasuaji unahitaji vifaa maalum na uangalizi wa karibu zaidi. Baada ya maelezo hayo, nilitafakari na kuona kuwa unafuu wa gharama za kujifungua hauwahusu wanaojifungua kwa upasuaji.
Malalamiko ya aina hii yamekuwepo kwa muda mrefu, siyo tu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, bali pia katika hospitali nyingine za rufaa zilizopo Dar es Salaam.
Hali hii inaweza kuwa tishio kwa familia nyingi, hususan wajawazito wasio na uwezo mzuri wa kiuchumi, katika kupata huduma za afya kwa usawa. Endapo kipaumbele cha Serikali ni kutoa huduma bure au kwa gharama nafuu, basi uamuzi huo unapaswa kuwahusu pia wanaojifungua kwa upasuaji.
Kutozwa gharama kubwa kunatoa tafsiri ya haraka kuwa kujifungua kwa upasuaji ni jambo la anasa. Kwa mfano, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, gharama za upasuaji ambazo zimekuwa zikitozwa kwa wamama niliokutana nao ni kati ya laki 4 hadi 8, kutegemeana na hali ya mjamzito.
Wapo watu wengi wanaoingia kwenye madeni kutokana na kugharamia upasuaji wakati wa kujifungua. Siyo wajawazito wote wanaojifungua kwa upasuaji huwa wamejiandaa mapema; wengine hupokea taarifa ya kuhitaji upasuaji baada ya kushindikana kujifungua kwa njia ya kawaida. Hali hii huwafanya wajikute hawajajipanga kifedha kwa gharama kubwa zaidi.
Wito wangu kwa Wizara ya Afya ni kulichunguza kwa kina suala hili na kueleza wazi unafuu wa huduma za kujifungua unagusa wa makundi gani.
Aidha, menejimenti ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili itafakari upya gharama zinazotozwa na iandae utaratibu rafiki zaidi ambao hautaacha jamii ikiwa na maumivu.