Rapunzel kwanza napenda kukupa pongezi kwa kuwa muwazi, hili ni jambo zuri sana nalo humweka mtu huru na kumwepusha na dhambi kubwa ya unafiki,
pili napenda nizungumzie hili swala la kujichua,tena si kwa wanawake pekee bali kwa wote yaani wanawake na wanaume pia,: sijawahai kufanya utafiti sana kuhusu kujichua lakini kutokana na maongezi ya hapa na pale nimekuja kujua kuwa kujichua kuna madhara tena makubwa tu kama vile
1.kukosa hamu ya tendo halisi kwa wote wanawake na wanaume hasa mtu akishazoea na kuwa addicted na hiyo kitu,
na pengine mume wako hajawahi kukukuta au hajui ikiwa una zoea hilo, lakini kuchua
2.huleta hali ya mfadhaiko au ya kutoaminiana ikiwa mwenzi mmojawapo atagundua kuwa mwezi wake ana zoea la kujichua.
hayo ni kwa upande wa kibinadamu tu lakini tukija kwa upande wa kiMungu
jambo hilo halifai na wala halipendezi machoni pa Mungu nalo ni kinyume na mipangilio aliyoiweka Mungu ya kuitosheleza tamaa ya mume na mke,kwa nini ni kinyume? ni kwa sabau Mungu alijua kuwa mume na mke wanaweza kutoshelezana tamaa zao za mwili lakini hakuwahi kuwaruhusu au kuwapa maagizo ya mume au mke kujitosheleza kibinafsi, kama angetaka kila mmoja awe na uwezo wa kujitosheleza nadhani asingewaweka pamoja ili kila mmoja ajitosheleze kivyake mpaka pale watakapohitaji watoto ndo awaweke pamoja, na siku zote mtu akienda kinyume na asili aliyoiweka Mungu basi madhara huwa hayakosekani(mf ushoga,usagaji,mchina,na carolyte vyote hivi si asili yake muumba na nadhani sote tunajua madhara yatokanayo na hayo yote) kwa hiyo kwa misingi hiyo ni vyema ukifikiria mara mbilimbili kile ambacho umezoea kukifanya pindi mume wako akiwa hayupo ili kujiridisha kimwili.
pia bado nakupa pongezi kwamba hautaki kumsaliti mume wako hongera kwa hilo hongera kwa kuwa mwaminifu kwa mume wako lakini nafikiri unapaswa kujitahidi kuacha zoea hilo kwani lina madhara na mbele za Mungu ni dhambi halafu hakuna mbadala wa dhambi kwamba kwa kuwa hutaki kufanya uasherati basi ujichue yaani uache dhambi hii kwa mbadala wa dhambi fulani,kama wengine wanasema nataka kuepuka uasherati kwa hiyo bora nilewe no hakuanga mbadala wa dhambi dhambi ni dhambi tu.
ni hayo mkuu
Rapunzel.