Kujenga barabara bila pavement kumefanya DSM kuwa mbayaa

Kujenga barabara bila pavement kumefanya DSM kuwa mbayaa

instagram

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,118
Reaction score
4,880
Mji wa dar barabara zake nyingi zimewekwa lami kisha huku pembeni zimeachwa kwenye majani au vumbi kupelekea waenda kwa miguu kupita kwenye majani au vumbi jambo linalochangia muonekano wa ki 3rd world na soli za watu kujaa uchafu.
Ni vema barabara ikijengwa basi kuwe na pavement kwa ajili ya waenda kwa miguu kama ilivyo kwa barabara za kigali zinazoleta muonekano wa ki ulaya ulaya.
Ndo mana ulaya utazani hakuna vumbi kwani barabara zao ziko paved ndo mana mtu anaweza toka home na kurudi hajakanyaga vumbi na anaweza kulala na viatu na shuka lisichafuke.

Muonekano wa kigali kama ulaya
FB_IMG_1580519761784.jpeg
FB_IMG_1580519776241.jpeg
FB_IMG_1580519755395.jpeg
FB_IMG_1580519801239.jpeg
FB_IMG_1580519790754.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakuja barabara imewekwa lami, pembezoni si tu kwamba hakuna pavement kwa waenda kwa miguu, bali hakuna kingo, na mvua ikinyesha, udongo wa pembeni wote unaingia barabarani, ikiwemo uchafu. Mbaya zaidi hata mitaro unakuta hakuna, maji kutoka maeneo mbalimbsli yanaingia barabarani, na muda si mrefu, mashimo yanaanza, na Value for Money haionekani. Barabara mpya zilizowekwa lami kama kutoka mbezi hadi Goba, kuna maeneo mvua iikinyesha, udongo wa pembeni unajaa barabarani. Laiti kama wangekuwa wanaweka pavement pembeni, mitaro ya maji, na kufanya landscaping maeneo ya pembeni kuzuia udongo kuingia barabarani, gharama za kuweka watu wa kuzifagia zingepungua na zingedumu zaidi. Barabara za Rwanda chini ya NPD (Tanroad-Tz) wanazingatia hilo, wameenda mbali zaidi kuweka vitofali pembeni mwa barabara na kuweka maua, mji unavutia sana, na si kigali tu, hata maeneo kama Remera, Kicukiro nk.
 
Na hizo zenye pavement basi wamewekwa Wamachinga. Watu wanatembea kwenye barabara pamoja na gari!
 
Barabara ya Mwenge Tegeta imejengwa vizuri ina sehemu za watembea kwa miguu lakini sehemu hizo zimegeuzwa za kufanyia biashara hasa maeneo ya Tangibovu hivyo kuhatarisha maisha ya watembea kwa miguu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajiuliza inakuaje CBD tena pale city center kuna nyumba mabati yake yana kutu na yamechoka kishenzi nyumba hazijapakwa rangi miaka kibao kwenye prime area kama ile ni kuweka sheria ndogo ndogo tu za kuwabana,mfano yeyeto anayetazamana na barabara kubwa mita 100 anawajibika kuwa na pavement,kila barabara iwe na standard yake na design ya block zake ziwepo kampuni mahususi kwa ajili ya kazi hizi zipewe hata subsidies kwenye material na misamaha midogo midogo kwny kodi ili kupunguza gharama kwa wananchi pia.Hivi viwanda vya cement na rangi haviwezi kuungana vikachagua barabara moja ya mfano?!,na kuwa na campaign like blah blah blah.
 
Wazo zuri kabisa. Ati unakuta lami imepita kwenye mtaa, halafu kutoka lami hadi nyumba za watu kama mita 5-10, na ni udongo tu, kwa nini wenye nyumba wasigharamie kuweka hata zege au pavement kuunganisha na lami?? Kuna barabara nzuri mfano wa mwendokasi, imejengwa kutoka kimara korogwe hadi maji ya chumvi ubungo, wameweka na pavement, shida kutoka kwenye pavement hadi nyumba za watu udongo, na kipindi hiki cha mvua ukipita, udongo unaingia kwenye barabara. Laiti wenye hizo nyumba wangelazimishwa kumwaga zege au kuweka pavement hadi lami, ingependeza sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom