Kujamiiana Siasa za Ujamaa na Kujitegemea - Serikari JPM

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,168
1,071
Nadiriki kusema kwa unyenyekevu mkubwa ya kuwa Hayati Mwalimu JK Nyerere alikuwa sahihi sana kuingiza mfumo wa kijamaa ktk misingi ya kufinyanga CCM na Serikari ya Tanganyika kisha Tanzania {baada ya Muungano wa Tanganyika na Visiwa vya Unguja na Pemba}..Lakini pia Azimio la Arusha lilikuwa kitovu cha mpevuko wa utekelezaji sera husika katika jamii yetu.

Ujamaa ndio mzizi wa usawa,uadirifu,uzalendo,utu,ubinadamu,udugu,upendo,uchapakazi,maono endelevu na maendeleo dhidi ya maadui ufisadi,ujinga,maradhi,njaa,ubinafsi,kujiinua,uchoyo,kujitajirisha,unyonyaji,ukabaila,ubeberu,udumedume na utajiri wa wachache dhidi ya maskini walio wengi.

Kwa Jicho la nne namwona Mh. Rais JPM akibeba maono ya kijamaa katika utekelezaji wa majukumu,ilani ya chama CCM alie mtoto wa TANU na ASP..Wengi wenye mitazamo ya kufanikiwa kinyume na misingi ya kijamaa lazima waendee kumkosoa,kumkejeri,kumvunja moyo na kumuombea mabaya ili asizidi kuharibu ndoto za mifumo yao ,nia zao,matarajio yao na mikakati yao ya kibeberu.
 
Kila kitu kina zama ndugu yangu. Tumetoka huko na hatuwezi kurudi kwenye ujamaa leo na tena tukirudi kwenye ujamaa hata dunia itatushangaa na sijui tutakuwa mgeni wa nani., nadhani kwa mtu asiependa kujishughulisha na kuchapa kazi ndio anautamani huo ujamaa.
Leo nchi zote duniani wapo kwenye ubepari wewe useme watz turudi kwenye ujamaa nonsense
 
Ujamaa na kujitegema ni kama maji na mafuta, havichangamani.

Ukiwa mjamaa halisi, kujitegemea ni kitu kibaya, kwani unaweka kipaumbele kwenye kutegemeana.

Ukijitegemea, ujamaa ni kitu kibaya, kwani unaweka kipaumbele kwenye kila myu kujitegemea.

Moja ya sababu "Ujamaa na Kujitegemea" ulishindwa ni ukweli kwamba hii ni dhana ya kufikirika zaidi ambayo haijajikita katika kuwezekana kutekelezeka.

"Ujamaa na Kujitegemea" is self contradictory.
 
Ujamaa uliofanyiwa Tohara with kind reference to China social economic success ...story/facts/testimony...
 
JPM amekuja na cash budget, lengo ni lile lile, fedha nyingi iwafikie walengwa kwa maana ya uchumi wa nchi kuzigusa zile sekta zenye kuhusiana na umasikini wa mwananchi wa kawaida.Hata hili la sukari kutoagizwa kutoka nje na lenyewe ni suala la kizalendo sana. Wazalishaji wa ndani washindwe wenyewe kuitumia fursa waliyopewa. JPM ni kiongozi wa nchi aliye mtekelezaji, sio mrasimu mwenye kufurahia hulka za urasimu, ambazo zinawaongezea walio wengi zile hasira na vinyongo.

Asibadilike, kwani anaombewa na walio wengi. Awakwepe wachumia tumbo wanaoishi katika majiji makubwa.
 
Kila kitu kina zama ndugu yangu. Tumetoka huko na hatuwezi kurudi kwenye ujamaa leo na tena tukirudi kwenye ujamaa hata dunia itatushangaa na sijui tutakuwa mgeni wa nani., nadhani kwa mtu asiependa kujishughulisha na kuchapa kazi ndio anautamani huo ujamaa.
Leo nchi zote duniani wapo kwenye ubepari wewe useme watz turudi kwenye ujamaa nonsense


Kwa hali yetu, sidhani kama ina tija sana. China wana sera hizo na wako strict kuitekeleza, hapa kwetu hata Nyerere(Baba Wa Taifa-R.I.P) inaonekana aliminywa na IMF na World Bank akabidi asalimu amri na kujikuta anapelekwa kwenye mrengo wautakao. Hata hivyo nadhan wachunguz wa mambo enzi hizo wanadai zilichangia yeye Kung'atuka( ingawa ushahidi wa hilo haujawa proved). Hivyo kusimamia ujamaa siyo kitu chepesi,na wazungu hawapendi hilo kabisa, sema China yuko imara hayumbishwi, ila kwa nchi zetu hizi inabidi kupambana hasa!
 
Back
Top Bottom