Kuitwa Mama Fulani na Baba Fulani

Kuitwa Mama Fulani na Baba Fulani

mjasiria

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2011
Posts
4,155
Reaction score
1,866
WanaJF habari za ninyi. Ninaamini kwa wengi wetu sikukuu zilikuwa mswano tu, full bataaz na mambao kama hayo. Kwa wale ambao mambo yalikuwa arijojo, napenda kuchukua fursa hii kuwafikishia pole za dhati kutoka kunako mtimani.

Turudi kwenye mada sasa. Imezoeleka katika jamii zetu za kitanzania kwa mtu mwenye mtoto/watoto kuitwa kwa kutumia jina la mtoto wake. Utasikia mama Semeniiiii, njoo huku muuza mboga anataka kuondoka, hapo snowhite anaitiwa mchicha au mama Dullah mwanao anatuletea usiku, sisi tunakuheshimu ila akizidisha kuna siku tutamtia ndimu ujue, huyu ni Kongosho mwenye mtoto mtukutu haswaa. Kwa upande wa wanaume hali ni hiyo hiyo. James anakuwa Baba V, watu8 anakuwa baba Magimbi, basi alimradi kila mtu aitwa kwa jina la mtotowe.

Tabia hii ipo hata kwa wanandoa wenyewe. Unakuta mtu kaoa basi mkewe akishatotoa tu, jina la mke linakufa na tangia hapo anakuwa mama fulani, na yeye pia hataki kusikia anaitwa jina lake isipokuwa baba fulani tu!!!. Tena wengine utasikia akiulizwa wewe iina lako nani mwenzetu, naitwa mama Ana au naitwa baba Mwaipenye, na ukisisitizia jina, mtu hataki kabisa anakwambia we niite hivyo hivyo tu.

Tuje kwenye hoja sasa. Japokuwa si jambo baya kutumia huu utaratibu lakini mimi naona kama unawanyanyapaa sana wale wasio na watoto, hususan wale wanaohitaji watoto lakini hawakujaaliwa kuwa nao. Fikiria kila wakisikia mama/baba fulani huko mitaani wanapata mawazo kiasi gani? Nadhani imefika mahali tuache huu utaratibu kwa sababu unawaumiza sana wenzetu ambao hawajajaaliwa. Wengi humu tunajua kuwa ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu kukosa mtoto linaangaliwa kama tatizo kubwa. Inabidi ifike mahali tutambue kuwa watoto ni majaaliwa tu kutoka kwa muumba. Yaani saa nyingine unakuta watu tunajisiiifu kwa kuwa na watoto kama vile kuna chochote kikubwa tumefanya zaidi ya ngono. Kabla sijapaluliwa naomba niseme kuwa natambua malezi ni kazi ya ziada, kwa hiyo hongera zao wote waliokuza.
 
Last edited by a moderator:
Zaa nawe uitwe baba Zaituni, mama yako huwa namwita '' wee Tupilike,nakuomba mara moja mama Bhooke'' thus all
 
Mkuu nmekusoma nikahis kuna sku ata utalaumu wanaotembelea magari kuwa wanajidai na kuwanyanyapaa wasio nacho.
ni hayo tu.

Kwani mkuu ukiwa na gari huwa unawaambia watu wakuite kwa kutumia gari lako? Kwa mfano huwa unasikia watu wakiitwa we mwenye toyota au we mwenye subaru, kimsingi hakuna. Sasa linganisha na watoto, kuna haja gani ya wewe James kuwa baba John, kwani hilo jina lako ulipewa la kazi gani??
 
huwa tunafanya hivyo kuchochea mtoto wako akiwa na shda kukuita jina mathalani kukuita james! james kwaiyo hiyo kidogo inasaidia ktk ilo, kuhusu mfano wa gari mkuu nilisemea kuwa kuitwa baba flani sio kuwanyanyapaa wasio na watoto, kama ni hivyo basi hata wenye magari basi watakuwa wanawanyanyasa wasio nayo, ingawaje jamii yetu pia sasa iamke kuwa sio kila ndoa ina mtoto mengine huwa ni majaaliwa ya mwenezi mungu.
 
niite jina langu bana mambo ya mama fulani yanipitie kushoto kuzeeshana tu na tabia za kifala.
Mie mpaka leo mama yangu anaitwa jina lake.
I prefer that.
Ila ukikakaa na miswahili utakoma nakuambia litakuita kwa sauti kubwaaa "we baba matatizoooooo hujambo"
 
amu punguza jazba bana, ila nimependa mchango wako!
 
Mbona unarudia hoja ile ile. Hebu nisome vizuri, mimi sisemi kuwa na watoto ni kuwanyanyapaa wasio na watoto kama ambavyo kuwa na gari si kuwanyanyapaa wasio nayo. Hoja hapa sio kuwa na watoto bali ni kuwaita wazazi kwa majina ya watoto wao, ndio nikakupa mfano kuwa kwani ukiwa na gari huwa unaitwa kwa jina la gari lako huko mitaani?!!!
 
amu punguza jazba bana, ila nimependa mchango wako!

jazba iko wapi??
Wewe utakuwa waichukulia jf serious sana na inakupa tabu.Wakati mwenzio niliandika meno 32 yote nje we wasema jazba!
Wancheksha!!!
 
tuntofautiana kama vidole hakuna siku tutafanana labda yesu aje ,chukua changamoto kama msingi wa maendeleo wako sio kulaumu tu haisaidiiii
 
Inategemea na utamaduni wa jamii au familia husika mm mpk leo mama namsikia akiitwa kwa jiba lake na baba na kinyume pia,except cc watoto ndo tunaita baba na mama
 
Inategemea na malezi na mapendekezo yenu sababu mimi mamayetu tuna muita Aunty,na Dad pia anamuita mkewe Aunty
wanangu wanamuita babu yao Dady nadhani nimazowea, sema mbaya ni pale wanapokuwepo wote mume wangu na Dad
ndio inakua Dad wa Mama na Dad wa Aunty ....
 
Hiki kizazi cha mama fulani enzi za wazazi wetu haikuwepo. Mimi ntapenda kuitwa jina langu na mwenzangu hivyo mambo ya mama/baba fulan i don't like hata kumwita mumwita mume wangu ba fulani haileti sense hadi watoto wanashindwa kujua majina ya wazazi wao kwangu huo ni upuuzi na hauna logic na wapi hii inaaply kama si uswahilini na wengine tumeiga mambo ya kiswahili tuu kule kijijini kwetu kulikuwa hakuna hayo mambo lakini kuanzia kizazi cha 90 ndo yameingia haya makitu. I like kuitwa jina langu Catherine na siyo eti ma pascal means what. Ni mawazo yangu
 
Ukiwa na zaidi ya mtoto mmoja pia ni shida! Watoto ambao majina yao hayatumiki (kuwaita wazazi wao) wanaweza kujisikia duni.
 
hiki kizazi cha mama fulani enzi za wazazi wetu haikuwepo. Mimi ntapenda kuitwa jina langu na mwenzangu hivyo mambo ya mama/baba fulan i don't like hata kumwita mumwita mume wangu ba fulani haileti sense hadi watoto wanashindwa kujua majina ya wazazi wao kwangu huo ni upuuzi na hauna logic na wapi hii inaaply kama si uswahilini na wengine tumeiga mambo ya kiswahili tuu kule kijijini kwetu kulikuwa hakuna hayo mambo lakini kuanzia kizazi cha 90 ndo yameingia haya makitu. I like kuitwa jina langu catherine na siyo eti ma pascal means what. Ni mawazo yangu

naunga mkono hoja kwa %100 hiyonimeipenda.
 
WanaJF habari za ninyi. Ninaamini kwa wengi wetu sikukuu zilikuwa mswano tu, full bataaz na mambao kama hayo. Kwa wale ambao mambo yalikuwa arijojo, napenda kuchukua fursa hii kuwafikishia pole za dhati kutoka kunako mtimani.

Turudi kwenye mada sasa. Imezoeleka katika jamii zetu za kitanzania kwa mtu mwenye mtoto/watoto kuitwa kwa kutumia jina la mtoto wake. Utasikia mama Semeniiiii, njoo huku muuza mboga anataka kuondoka, hapo snowhite anaitiwa mchicha au mama Dullah mwanao anatuletea usiku, sisi tunakuheshimu ila akizidisha kuna siku tutamtia ndimu ujue, huyu ni Kongosho mwenye mtoto mtukutu haswaa. Kwa upande wa wanaume hali ni hiyo hiyo. James anakuwa Baba V, watu8 anakuwa baba Magimbi, basi alimradi kila mtu aitwa kwa jina la mtotowe.

Tabia hii ipo hata kwa wanandoa wenyewe. Unakuta mtu kaoa basi mkewe akishatotoa tu, jina la mke linakufa na tangia hapo anakuwa mama fulani, na yeye pia hataki kusikia anaitwa jina lake isipokuwa baba fulani tu!!!. Tena wengine utasikia akiulizwa wewe iina lako nani mwenzetu, naitwa mama Ana au naitwa baba Mwaipenye, na ukisisitizia jina, mtu hataki kabisa anakwambia we niite hivyo hivyo tu.

Tuje kwenye hoja sasa. Japokuwa si jambo baya kutumia huu utaratibu lakini mimi naona kama unawanyanyapaa sana wale wasio na watoto, hususan wale wanaohitaji watoto lakini hawakujaaliwa kuwa nao. Fikiria kila wakisikia mama/baba fulani huko mitaani wanapata mawazo kiasi gani? Nadhani imefika mahali tuache huu utaratibu kwa sababu unawaumiza sana wenzetu ambao hawajajaaliwa. Wengi humu tunajua kuwa ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu kukosa mtoto linaangaliwa kama tatizo kubwa. Inabidi ifike mahali tutambue kuwa watoto ni majaaliwa tu kutoka kwa muumba. Yaani saa nyingine unakuta watu tunajisiiifu kwa kuwa na watoto kama vile kuna chochote kikubwa tumefanya zaidi ya ngono. Kabla sijapaluliwa naomba niseme kuwa natambua malezi ni kazi ya ziada, kwa hiyo hongera zao wote waliokuza.
though nimetoka nje ya mada kidogo kuna mtu mmoja yeye alioa akapata mtoto mmoja na mkewe kwa sasa mtoto ana miaka 22 , ndugu wa mwanaume wakawa wanamsakama mama wa watu oho sijui nii , asa kwa vile mwanamume alikuwa na hela ya kutosha akawa videmu vingi tu wasichana wa daslam walivyo wajanja wakawa wanamsakizia watoto karibu watoto wa nne kasakiziwa hili amaligundua baada ya kwenda kufanyiwa uchunguzi marekani mwaka jana akaambiwa kuwa ana tezi , wataalam wakamwambia for all those 20 years you were unable to impregnant any woman , alivyorudi tanzania akawaita wale wanawake akawauliza hawa watoto ni wa kwangu kweli? waleteni tukapime dna wakatoka baru, mke wake kajifungua january mwaka huu baada ya miaka 22 ila ndoa kazi na vitimbi
 
niite jina langu bana mambo ya mama fulani yanipitie kushoto kuzeeshana tu na tabia za kifala.
Mie mpaka leo mama yangu anaitwa jina lake.
I prefer that.
Ila ukikakaa na miswahili utakoma nakuambia litakuita kwa sauti kubwaaa "we baba matatizoooooo hujambo"

Mswahili ni nani?je wewe si mswahili? je unajua maana ya ubaguzi?
 
Back
Top Bottom