Kuita na kuhoji mashahidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuita na kuhoji mashahidi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Oct 25, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,612
  Likes Received: 4,603
  Trophy Points: 280
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=+2]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Na Dkt. Abdallah J. Saffari[/SIZE][/FONT]

  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]MSHITAKIWA ana haki ya kuita na kuwahoji mashahidi. Kwa kawaida ataita wale mashahidi ambao watatoa maelezo mbele ya mahakama ambayo yataunga mkono madai yake ya utetezi. Mahakama, na kila mtu mwenye akili timamu wanatarajia kuwa shahidi aliyeitwa na mshitakiwa atatoa ushahidi wa kumtetea mshitakiwa. Hali kadhalika ndivyo ilivyo hata kwa upande wa mashitaka. Hivyo iwapo shahidi aliyeitwa atatoa ushahidi dhidi ya mshitakiwa ushahidi huo utatiliwa maanani sana dhidi yake.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kuita mashahidi ni tofauti na kuwahoji mashahidi. Kwa kawaida mshitakiwa atatoa mahakamani orodha ya mashahidi ambao anataka waitwe shaurini kwa niaba yake. Mahakama yatatoa hati za kuitwa shaurini mashahidi hao (F.142(1), Sheria ya Mwenendo wa Jinai, Na. 1, 1985).[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Lakini sio lazima kuwe na hati hizo. Iwapo mshitakiwa atakubaliana na shahidi au mashahidi wake wafike mahakamani saa na tarehe iliyopangwa kutoa ushahidi basi itatosha. Tatizo la utaratibu huu wa pili ni pale shahidi anapoacha kufika mahakamani, kwa makusudi au la. Mahakama yatakuwa hayana taarifa na ushahidi kamili mbali na kauli ya mshitakiwa kwamba mashahidi wanaohusika, kwa kweli, waliahidi kufika mahakamani saa na siku iliyohitajika.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Katika hali kama hizo kwa kawaida mahakama hutoa fursa ya mshitakiwa kuwaita tena mashahidi wake hususan kwa kuyataja majina na anuani zao kamili. Baadaye mahakama hutoa hati za kuwaita shaurini mashahidi hao. Kwa hivyo hati ya kuwaita shaurini mashahidi ni njia bora zaidi kuliko ile ya pili. Maana kwanza hati hiyo ni ushahidi madhubuti kwamba shahidi ameitwa shaurini muradi iwe aliipokea. Pili ni amri ambayo adhabu hutolewa inapovunjwa na shahidi (F.247(1), Sheria ya Mwenendo wa Jinai, i.h.j).[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kuhoji mashahidi hukamilisha maana ya kuwaita shaurini. Kwa kutumia njia ya kuhoji mahakama hupata wasaa wa kuelezwa na kunakili ushahidi unaodaiwa katika shauri linalohusika. Hivyo ni haki ya mshitakiwa kupewa fursa hii adhimu ya kuhoji mashahidi.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Ziko namna tatu kuu za kuhoji mashahidi kama tulivyokwishaona huko nyuma. Mshitakiwa halidhalika anayo haki ya kuzitumia namna zote hizo ama kwa mashahidi wake au dhidi ya wale wa upande wa mashitaka.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Mahojiano ya awali yatatumiwa na mshitakiwa mintaarafu ya mashahidi wake yaani wale aliowaita kumtetea. Atawauliza maswali ambayo majibu yake yatakuwa ushahidi wa utetezi wake. Inatarajiwa kuwa sehemu kubwa ya ushahidi muhimu unapatikana katika mahojiano ya awali. Ni wajibu wa mshitakiwa kuhakikisha anauliza na kupata majibu sahihi na ya maana kwa utetezi wake. Maswali yasiyo kuwa na maana hayasaidii upande wowote, hivyo hayatamsaidia mshitakiwa pia. Kuhoji mashahidi vizuri hutegemea mbinu, wepesi na maarifa na uzoefu wa uendeshaji mashauri mahakamani. Ni vigumu kumfundisha mshitakiwa namna na jinsi ya kumhoji shahidi wake katika hatua hii ya awali. La muhimu ni kuuliza maswali ya maana mintaarafu ya utetezi wake, yaani maswali ambayo majibu yake yataupiku au kuudhofisha ushahidi uliotolewa awali na upande wa mashitaka.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Mahojiano ya awali hufuatiwa na mahojiano kinzani yanayofanywa na upande wa mashitaka ili kuutikisa ushahidi wa mshitakiwa. Bada ya mtikiso huo wa ushahidi kunaweza kuwa na athari nyingi sana juu ya ushahidi wa utetezi uliotolewa na mshitakiwa au shahidi wake. Pengine anaweza kuwa ametetemeka tu, akasahau kitu, hivyo akasema jambo tofauti na alilosema mwanzo na kadhalika. Kunaweza kukawa na tofauti za msingi na nyingine ndogo ndogo tu kutokana na ushahidi aliotoa awali. Kwa hali hiyo mshitakiwa hupewa fursa ya kusahihisha athari zozote zinazotokana na mahojiano kinzani. Atafanya hivyo kwa mahojiano msawazo.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kwa hiyo mahojiano ya msawazo humpa nafasi mshitakiwa kusahihisha athari ambazo zimetiwa na upande wa mashitaka kwenye ushahidi uliotolewa na mashahidi wa mashitaka.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Pengine mahojiano muhimu mno kupita yote kwa mshitakiwa, ni mahojiano kinzani (F.148, Sheria ya Ushahidi, Na. 6, 1967). Kama ilivyoonekana kwa upande wa mashitaka, mahojiano haya humpa mshitakiwa nafasi muhimu ya kuwauliza mashahidi wa mashitaka maswali yote ambayo majibu yake yatamsaidia katika utetezi wake. Mshitakiwa anaweza hata akahoji mambo ambayo shahidi hakuwahi kuyasema katika mahojiano ya awali yaliyoongozwa na upande wa mashitaka. Kwa vile haja ya mahojiano haya ni kuchimbua kweli hakuna mipaka iliyowekwa na sheria juu ya maswali ya kuuliza ila matusi dhahiri. Uongo mwingi hufichuliwa katika mahojiano haya.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Na mahakama yanalielewa jambo hili vizuri kiasi kwamba kumnyima nafasi hii kumesababisha kubatilishwa hukumu za awali dhidi ya washitakiwa. Katika shauri la R. v. John Bosco (Shari la Jinai la Masahihisho No. 6, 1979, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mbeya) mshitakiwa hakupewa nafasi ya kuwahoji mashahidi wa mashitaka wawili wa nne na wa tano. Hata hivyo hatimaye mshitakiwa huyo alipatikana na hatia ya kumnajisi msichana wa umri mdogo. Hukumu hiyo ilibatilishwa na Mahakama Kuu baadaye kwa vile kutokumpa mshitakiwa huyo fursa ya kuwahoji mashahidi wawili muhimu wa mashtaka kulisababisha haki kutotendeka maana ushahidi wao haukutikiswa kuona kiasi gani ulikuwa sahihi.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Ushahidi wa mshtakiwa[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Baada ya ya upande wa mashitaka kumaliza kuwaita mashahidi wake mahakamani lazima yaamue iwapo mshitakiwa anastahili kujibu mashitaka au la (F.230, Sheria ya Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Endapo mahakama yataona kwamba mshitakiwa hastahili kufanya hivyo yatamwachia huru mara moja na hataweza tena baadaye kushtakiwa kwa kosa hilo (F.231, Sheria ya Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Lakini mahakama yakiridhika kuwa mashitakiwa anastahili kujibu shataka yatampa mshitakiwa huyo fursa ya kujitetea.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kuna namna mbili ambazo kwazo mshitakiwa anaweza kuzitumia kabla ya kutoa utetezi wake. Ni wajibu wa mahakama kumfahamisha mshitakiwa njia zote hizo mbili. Kwanza mshitakiwa anaweza kutoa ushahidi kwa kiapo au bila kiapo na kuita mashahidi wake. Au anaweza kukaa kimya isipokuwa mahakama na upande wa mashitaka yatatafsiri kimya hicho dhidi yake (F.231(3), Sheria ya Mwenendo wa Jinai, i.h.j). Kabla ya Novemba 1, 1985 mshitakiwa aliweza kutoa ushahidi bila kiapo ambapo asingeweza kuhojiwa na upande wa mashitaka wala mahakama. Athari ya jambo hilo ilikuwa ni kuficha ushahidi muhimu. Lakini sasa hata kama mshitakiwa hatatoa ushahidi wake bila kiapo wala kuita mashahidi bado atahojiwa na upande wa mashitaka au mahakama (231(2), Sheria ya Mwenendo ya Jinai, i.h.j).[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Aina ya utetezi[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kuna aina nyingi za makosa ya jinai. Idadi yake kubwa kama vile wizi, kughushi maandishi, mauaji, kubaka, uhaini na kadhalika yameorodheshwa na kufafanuliwa vizuri katika Kanuni ya Adhabu ( Sura ya 16, Sheria za Tanzania). Hata hivyo yako makosa mengine ya jinai kwa mujibu wa sheria kadha wa kadha. Makosa ya kutoa rushwa, kwa mfano, husimamiwa na Sheria ya Rushwa (Na. 16, 1971), makosa dhidi ya matumizi ya fedha za kigeni hushughulikiwa na Sheria ya Kudhibiti Fedha za Kigeni (Sura ya 294). Aidha, kuna sheria ya Usalama Barabarani (F.8, Kanuni za Adhabu, Sura ya 16, Sheria za Tanzania) ambayo hushughulikia makosa yote ya uvunjaji wa sheria hizo kama vile kuendesha gari kwa njia ya hatari na kusababisha kifo.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Ufafanuzi mzuri wa makosa yote ya jinai hupatikana katika uamuzi wa mashauri mbalimbali ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ambayo sio muhimu mno kuyarejea hapa.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kila kosa la jinai lina utetezi wake. Takriban kuna aina kumi kuu ya utetezi dhidi ya makosa mbalimbali ya jinai. Nazo ni kama zifuatazo:[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1. Kutojua sheria[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kutojua sheria sio utetezi wa kosa lolote lile la jinai isipokuwa tu inapoelezwa (F.8, Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Sheria za Tanzania). Inadaiwa kwamba endapo kutoijua sheria kungekuwa ni utetezi watu wengi mno wangefanya makosa kwa kisingizio hicho. Kwa bahati mbaya idadi kubwa ya Watanzania na watu wengine wengi ulimwenguni hawajui kusoma na kuandika. Wale wanaojua kusoma hapa Tanzania hufanya hivyo na kuelewa kwa lugha ya Kiswahili pengine na Lugha ya makabila yao. Lakini miswada na sheria zote kuu hadi sasa huandikwa kwa Kiingereza, lugha ya kigeni inayoeleweka vyema na watu wachache sana. Yaani asiyejua kusoma na kuelewa lugha ambayo kwayo sheria zimeandikwa ni shauri yake.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Tatizo jingine dhahiri ni uchache wa usambazaji wa sheria zenyewe. Taasisi chache tu huwa na nakala za sheria kuu,kama vile maktaba za sheria katika vyuo na mahakama. Hata baadhi ya mahakama ya wilaya na Mahakimu Wakazi hayana sheria muhimu. Kutokana na uchache huo wakorofi hushawishika kuziiba kwa matumizi yao binafsi. Ndiyo kusema tatizo hili huweza kuathiri, kwa namna ndogo au hata kubwa, utekelezaji wa utoaji wa haki haraka na kwa usahihi.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]2. Itibari[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Imani ya kweli kwamba mtu ana haki au itibari ya milki ya mali au kitu chochote kile ni utetezi wa kutosha dhidi ya mashitaka yote ya aina ya wizi (F.9, Kanuni ya Adhabu, i.h.j). Kwa mfano mtu anapanda na kuondoka na baiskeli moja kati ya kumi ambazo zimeegeshwa akiamini kuwa baiskeli hiyo ni yake, hana hatia ya wizi. Msingi wa utetezi huo ni kukosekana kwa nia mbaya mintaarafu ya mshitakiwa katika kutenda tendo analoshitakiwa nalo. Watu hufanana, itakuwa vitu? Hivyo huweza kutokea mtu akakosea na kuchukua kitu ambacho kimefanana mno na mali yake kwa imani ya kweli kwamba kitu hicho ni chake. Utetezi hu ni mintaarafu ya vitu au mali tu.[/SIZE][/FONT]
   
 2. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu kwa elimu hii kuhusu mashahidi, pamoja na kwamba font imekuwa ndogo na inauumiza macho.
  Article ni ndefu hivyo font ingekuwa kubwa kidogo.
   
Loading...