Kuiongelea Tanzania bila Mwalimu ni uendawazimu

Feb 9, 2012
58
10
KUIONGEREA Tanzania ya leo bila kumwongelea Mwalimu JK Nyerere ni kujidanganya.

Wengine wanathubutu kusema eti awamu hii imefanya maendeleo makubwa kuliko ya Nyerere, ni kwa vigezo gani?

Mwalimu alisema hatutaki maendeleo ya vitu, majumba, barabara, magari, bali tunataka maendeleo ya watu.

Je, watu wetu wana maendeleo gani, umaskini, ujinga na maradhi, bado yanawasumbua kwa kiasi kikubwa sana.

Tafsiri ya maendeleo kwa Mwalimu JK Nyerere ni maendeleo ya watu na si vitu.

Watanzania tufumbue macho yetu ili tutambue tupo wapi na tunapelekwa wapi na utawala huu wa Awamu ya Nne?

Kuhusu ukabila, ukanda na udini Mwalimu JK Nyerere ambaya sasa ni mtumishi wa Mungu, yaani yumo katika mchakato wa kufanywa Mtakatifu, alionya tangu mwanzoni kwa kusema kwamba: "Ukabila bado upo. Kwa hiyo, ukabila lazima uendelee kupigwa vita.

Hapana kukaa na kusema; Tanzania hatuna ukabila'. Hapana. Watu hatujawa Watanzania bado. Kwa hiyo, lazima tuendelee kuupiga vita. Na watu wana udini dini. Kuna watu kabisa wanatamani nchi hii iwe ya Kikristu, wajinga. Kuna watu wanatamani nchi iwe ya Kiislamu, wajinga. Natumia neno zuri wajinga, sisemi wapumbavu. Wajinga!"

Huyu ndiye rais wa Awamu ya Kwanza na alikuwa anamaanisha kile alichokisema, lakini awamu yetu hii ni awamu ya propaganda na porojo.

Zaidi kuhusu suala la udini na msimamo wa rais wa nchi Mwalimu Nyerere alitoa msimamo huu: "Tunataka rais wetu, akiwa Mkristu, ajue hatumchagui kwa sababu ya Ukiistu wake. Akiwa Mwislamu, ajue hatukumchagua kwa sababu ya Uislamu wake. Hatumchagui awe rais wa Wakristu wala awe wa Uislamu, na tunataka hilo alijue na alikubali kwa dhati na alisimamie na ndiye kiongozi wetu. Alisimamie kwa dhati bila woga, ndiye kiongozi wetu. Katika nchi changa namna hii, ambayo watu haraka sana hukimbilia ukabila, haraka sana hukimbilia udini, tunataka kiongozi awe imara kabisa katika mambo kasma haya."

Leo siku ya Jumatano ya majivu tunapoanza kutafakari mateso ya Yesu aliyoleta mapinduzi ya kiroho na jamii nzima basi tufikirie juu ya madhara ya udini katika nchi yetu. Huenda ni muda mwafaka kwetu sote kuomba na kufunga katika kipindi hiki cha neema ili Mungu atuepushe na machafuko yatokanayo na viongozi wabovu wa kisiasa na jamii.

Na kila mmoja wetu hasa viongozi Wakristo wajiulize wanafanya nini kutetea haki ya wanyonge, wanafanya nini kujenga Tanzania yenye haki na usawa katika masuala yote?

Kwanini kwa mfano wabunge hawapingi suala la kuiingiza nchi ya Tanzania katika Jumuiya ya nchi za Kiislamu, au kuingiza Mahakama ya Kadhi katika Katiba mpya, wakati tukijua masuala hayo ni hatari sana kwa mshimakamo na amani ya nchi yetu? Watanzania tunahitaji kuomba sana ili Mungu aiepushe nchi yetu na mipango ambayo ninaamini haifanikiwi kamwe, kwa sababu Mungu wetu ni Mungu wa Upendo na ni baba wa wote bila kujali dini, itikadi wala kabila.

Sote tusimame imara, kama unavyosema ujumbe wa maaskofu Katoliki katika kipindi hiki cha kwaresima; pamoja na Mungu wetu tuupige vita ukabila, ukanda na hasa udini katika nchi yetu.

Kwa Wakristo nawatakieni mwanzo mwema wa kipindi hiki cha kwaresima, ambacho ni kipindi cha mabadiliko katika mwenendo wetu kama Wakristo, tubadilike na tudhamirie kutenda matendo mema hasa kwa maskini na wasiojiweza.

Hiki kipindi kituletee neema na kweli na hatimaye tukafufuke na Kristu Mtawala, aliyeshinda maovu yote, ukiwapo ukabila na udini. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

CHANZO: Tanzania Daima | Fr. Mapunda
 
Kwa ccm ya kikwete foleni ya dsm anajivunia ni maendeleo lakini nani wanamiliki magari hajui kazi kweli kweli!!!!!!!!
 
kwa Tanzania hakuna kama Nyerere Julias wanaombeza wote utaona wanazungumzia upande wao. Nyerere Julias ni Jembe halitatokea hapa Tanzania. Alishayasema yote miaka mingi iliyopita si hawa wanaombeza wanarudia tuuu. RIP Kambarage
 
Back
Top Bottom