Kuimarika kwa CCM ni mwiba kwa Upinzani

Tatizo la Kinana ni kuwa anaongea kana kwamba ccm siyo chama tawala. Kuna maana gani kupanda kwenye jukwaa na kueleza juu ya udhaifu wa serekali wakati wao ndio wenye serekali? Wapainzani watatumia udhaifu huo huo kumwumbua Kinana na serekali ya chama chake. Wananchi hatutaki porojo, tunataka utekelezaji na hilo Kinana hawezi kulitenda

Ni kweli hii ni weakness kubwa sana kwa CCM na ni mbinu ambayo ni very risky. Kama wapinzania wakitumia huu mwanya vizuri CCM watakuwa wameumia. Yaani wewe unataoka kwenda kulalamika kwamba nyumba yako ni chafu, badala ya kuisafisha? Kwani hao watendaji anaowalalamikia wamewekwa na nani?
 
Aliyemteka Mh. Rose Kamili Kipndi cha Kampeni za Uchaguzi Mdogo Jimbo la Kalenga.

Mdudu halisi,
Umewahi kusema haya na wafuasi wako?
Kuhusu Yusuf Kongoroka, nilitaka kujua kama wale mamburula waliomkamata wamemfikisha mahakamani ili akatendewe haki kwani ni dhahiri ya kwamba walimwonea kwa kusubiri ahudhurie mkutano ndo wamtie kwenye mikono ya sheria wakati wanafahamu anapoishi, kwa nini wasiende kumkamata nyumbani kwake?

Na huyo ndg yako aliyewapuuza watu wa Mtwara kwa kuwaita wajinga kwa sababu ya kuomboleza vifo vya ndugu zao, hivi hafahamu kwamba jamii nyingi hapa Tanzania zina viwango tofauti vya ujinga kutokana na tamaduni zao? Jamii za wafugaji hawataki kusoma hata kama serikali inawajengea shule na kuwapelekea walimu. Wewe umeona wapi kwenye tatizo kuhusiana na hizo mada zangu?
 
Mapenzi Yepi kiongozi,ya kitandani ama? Kama ni ya kitandani ni kweli maana huko wapo akina Chemba,Kapuya n.k, Ila kama ni kuwatumikia wananchi basi nawewe umeungana na Kikwete et all kututukana watanganyika. Inasikitisha hali ya kiuchumi Tanzania vilio kila kona wewe unaendelea kuitukuza ccm. Inanipa tabu niamini kama kichwani kwako kuko sawa. Yawezekana unaishi mjini,utakuwa na haki ya kutetea ccm japokuwa hujui maumivu ya jopo kubwa la vijana bila ajira wa mitaji. Kijijini hukoo ndiyo kabisaa wengine kabisa utawaonea huruma maana mbolea kwa ajili ya mazao balaa tupu,ruzuku mnapiga wenyewe juu kwa juu. Jaribu kuwaza mara mbili mbili kabla hujuitukuza ccm na upumba.vu mwingine,na mengine bado sijaandika mfano madawa ya kulevya, kuuwawa kwa Kinana(Tembo) n.k. Tafakari tena katika andiko lako.
Kaka naona umeandika kwa jazba sana. Naomba utambue kwamba watanzania ndo wanaoifanya CCM iendelee kushika hatamu kutokana na UBORA wa sera zake. Hao unaowafikiria kwamba watatuletea maisha mazuri kamwe hawawezi na ndiyo maana watanzania wanahofia kuwapa ridhaa ya kuongoza nchi.
 
CCM hawana mapenzi ya kweli kwa wananchi ndiyo maana wakawaletea serekali inayowaumiza wananchi na hilo Kinana ana lifaham ndiyo maana anazunguka nchi nzima akiinanga serekali ya CCM.
Mbona UKAWA nao wanaizunguka Tanzania mkuu. Lengo lao ni kujijenga kama ilivyo kwa CCM.
 
Kinana ametengeneza CCM ndani ya CCM ndiyo kuimalika huko?Ulishawahi ona wapi chama tawala kinaiponda serekali yake?Hapo hakuna chochote cha maana alichokifanya Kinana.Alichokifanya Kinana ni kuangalia ni kitu gani ambacho kinatumiwa na wapinzani kuwavutia wananchi akagundua kuwa ili uweze kuwapata wananchi ni kuishambulia serekali kwa maovu inayoyafanya wakati maovu hayo ni ya CCM yenyewe na kuendeleza kutoa ahadi nyingi ambazo nyingi zimeshindwa kutekelezwa na hazitekelezeki.Alicho kifanya Kinana ni kufanya yale ambayo wapinzani wanayafanya baada ya kugunduwa kuwa wapinzani wanayatumia hayo kuibomoa CCM.Kwa hiyo Kinana aliona kuwa hakuna jipya ambalo anaweza kulifanya ili wananchi waendelee kuihurumia CCM isipokuwa ni kuunda upinzani ndani ya CCM ili ifanane na wapinzani halisi.

Swaddakta mkuu
 
Hivi wanaosema kwamba wanazunguka huko na huko kuimarisha Chama Cha Mapinduzi, na kwamba kinazidi kuimarika; mbona hawatuelezi pia ni lini Chama chao kilidhoofika, na kwa nini????????
 
Kaka naona umeandika kwa jazba sana. Naomba utambue kwamba watanzania ndo wanaoifanya CCM iendelee kushika hatamu kutokana na UBORA wa sera zake. Hao unaowafikiria kwamba watatuletea maisha mazuri kamwe hawawezi na ndiyo maana watanzania wanahofia kuwapa ridhaa ya kuongoza nchi.

CCM ninayoifahamu mimi haina ridhaa ya wananchi kwa miaka 10 sasa bara. Ni Bahati mbaya tu kuwa ccm ilifanikiwa kuwateka fikra watanzania kuwa wao ni chama tawala na kuwajengea imani kuwa hakuna zaidi nje ya CCM. Kwa kuwa mrefu watanzania waliamini hivyo lakini sasa hali imebadilika. Watanzania wameamka na wameona utumwa waliouishi chini ya CCM ndio maana 'hamkani hali si shwari tena' CCM.

Kinana na boya Nape kiguu na njia mikoani kunusuru chama. Waliobaki CCM ama ni mamluki wanaoona haya kujikomboa au mateka wa siasa za sumu zq CCM.
 
Ni kweli hii ni weakness kubwa sana kwa CCM na ni mbinu ambayo ni very risky. Kama wapinzania wakitumia huu mwanya vizuri CCM watakuwa wameumia. Yaani wewe unataoka kwenda kulalamika kwamba nyumba yako ni chafu, badala ya kuisafisha? Kwani hao watendaji anaowalalamikia wamewekwa na nani?

Kukiri madhaifu uliyo nayo ni tabia ya mtu muungwana sana. Kwa hakika ndugu zangu mimi naahidi kumpa Tsh 5,000 mtu yeyote atakayeonesha hutuba yeyote (video) ya kiongozi wa Chadema akikiri kuwa kuna mapungufu fulani ndani ya chama hicho. Lakini kitaalamu tunajua kuwa hakuna chama kisichokuwa na mapungufu kokote Duniani. sasa hawa cdm ni malaika?
 
Kaka naona umeandika kwa jazba sana. Naomba utambue kwamba watanzania ndo wanaoifanya CCM iendelee kushika hatamu kutokana na UBORA wa sera zake. Hao unaowafikiria kwamba watatuletea maisha mazuri kamwe hawawezi na ndiyo maana watanzania wanahofia kuwapa ridhaa ya kuongoza nchi.
Hii comment haitofautiani na kinyesi.
Ccm=shimo la choo
 
Mkuu uwezekano wa CHADEMA na UKAWA kuchomoka ni mdogo mno, ni sawa na ngamia kupenya katika tundu la sindano.
 
Utakuwa umetoka kunywa gongo na KINANA wewe sio bure.

AKILI NYINGINE ni kama maziwa mgando.
 
Ndg zangu wana JF,

Natumaini nyote ni wazima wa afya njema.

Naomba nitumie nafasi hii kuwafahamisha watanzania wenzangu kwamba kwa mwenendo huu wanaouonesha Chama Cha Mapinduzi katika kipindi hiki cha cha Awamu ya Nne, ni dhahiri ya kwamba Wapinzani wana safari ndefu ya kuhakikisha wanaingia Ikulu. Katika uhalisia wake CCM imeendelea kukubalika vijijini na mijini hasa kutokana na utekelezaji usio wa kubabaisha wa ilani yake ya uchaguzi.

Mifano halisi ya hivi karibuni inayoonesha ni jinsi gani wananchi wamejenga moyo wa matumaini kwa chama hiki ni vile kilivyoweza kujizolea kura lukuki katika chaguzi za Madiwani katika kata 27 pamoja na chaguzi ndogo za wabunge zilizofanyika katika jimbo la Kalenga na Chalinze.

Lakini kama hiyo haitoshi, wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi katika mikutano mbalimbali ya CCM inayoendelea kote nchini, mfano mzuri ni mikutano ambayo Katibu Mkuu, Comrade Abdulrahiman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Mh. Nape Nnauye wameifanya katika mikoa ya Tabora na Singida ilivyohudhuriwa na wananchi wengi wapenda maendeleo

. Mahudhurio haya ni yamethibitisha kwamba watanzania wengi wana imani na Chama Cha Mapinduzi na kwamba ndicho kitakachowakomboa toka kwenye lindi la umaskini.

Comrade Kinana na Nape walikuwa katika ziara ya kukagua uhai wa chama pamoja na kukagua utekekelezaji wa ilani ya uchaguzi ambapo wamekagua utekelekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya za mikoa Tabora na Singida.

Si vibaya pia tukajikumbusha mafanikio haya yaliyopatikana chini ya utawala huu makini wa Chama Cha Mapinduzi;

Kwanza ni ujenzi wa misingi imara ya kiuchumi. Hapa, watanzania wamejionea ubora na uimara wa miundo mbinu, kwa mfano barabara zimeboreshwa kiasi ambacho wafanyabiashara wanauwezo wa kusafirisha bidhaa zao kutoka na kwenda kokote hapa Tanzania bila usumbufu wowote unaosababishwa na ubovu wa barabara hivyo unaweza kujipatia bidhaa yoyote ukiwa popote Tanzania hata kama ni kule kijijini Mbaha, kando kando ya ziwa Nyasa.

Reli nayo imeimarishwa kwa kufanyiwa ukarabati na sasa unaweza kusafiri kwa treni toka Dar kwenda Kigoma kwa muda wa siku mbili tu tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ilichukua muda wa siku tatu kutoka Dar kwenda Kigoma. Viwanja vya ndege vya Kigoma na Mtwara vimefanyiwa ukarabati mkubwa ikiwa ni katika kuhakikisha usafiri wa anga unaimarika.

Mafanikio mengine ya CCM ni pamoja na kuondoa kero ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi wa maeneo mbalimbali nchini, na hapa tumeshuhudia uanzishwaji wa mradi mkubwa wa maji wa ziwa Victoria ili kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa. Katika sekta ya Elimu, serikali ya Chama Cha Mapinduzi imefanikiwa sana kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na ule uliohusisha Elimu ya Sekondari (MMES).

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2002 watoto wengi waliohitimu elimu ya msingi wameweza kujiunga na elimu ya sekondari na hivyo kuhakikisha kwamba suala la kupata elimu ni haki ya kila mtoto. Pia kumekuwa na ongezeko la vijana wanaojiunga na Elimu ya Juu, huku Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ikibeba jukumu kubwa la kutoa mikopo kwa ajili ya kugharimia mafunzo na kuhakikisha kwamba vijana wote wanaojiunga na kiwango hicho cha elimu wanahitimu masomo yao.

Pia CCM imefanikiwa kuimarisha utawala bora kwa kuweka na kujenga misingi imara ya kiuongozi na kiutawala kwa kuhakikisha viongozi wanawajibika ipasavyo kwa wananchi. Kiongozi anapokosea huchukuliwa hatua za kinidhamu ama zile za kisheria na pale anapofanya vizuri hupongezwa. Katika kulitekeleza hili, tumeshuhudia viongozi mbalimbali wakipongezwa na huku wengine wakiwajibishwa kutokana na makosa mbalimbali waliyofanya.

Mfano, kuna kesi zinaendelea mahakamani kuhusiana na matumizi mabaya ya madaraka na ambapo wahusika wake ni vigogo kadhaa waliopata kuhudumu kwenye serikali ya Chama Cha Mapinduzi.

Lakini kuimarika kwa miundo mbinu kama vile majengo mbalimbali kwa ajili ya makazi ya watu na ofisi mbalimbali za idara za serikali na mashirika ya umma ni mafanikio mengine ambayo CCM wamejipatia katika kipindi chote cha utawala wao.

Ingekua naamini kwamba umeandika hii kutoka akilini mwako mwenyeweningejibu ufukarea wako wa ubongo na matumaini yako ya kupona ugonjwa wa cancer ya mapafu ya ccm . Ila naamini kabisa umetumwa tu kutest chumvi ya mwenendo wenu wa mikutano ya mikoani ambayo mmejifanya na nyie ni wapinzania wa kulaani uetendaji mmbovu usioridhisha wa wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi wao kana kwamba watendaji hao ni wa chama cha CUIF!!! shame on you, mmebakiwa na karata moja tu kwa sasa kama ccm, ambayo ndio turufu yenu UJINGA WA WATANZANIA baaaas, ukiondoa hilo hamna loloy=te jata asilimia 2% ya kura hamwezi kupata.

Ushauri wa bure, enddeleni na sera zenu za shule za kata na kuimarisha ujinga kwa watanzania kwani ndio mtaji wenu pekee uliobakia. maneno yako haya "Katika uhalisia wake CCM imeendelea kukubalika vijijini na mijini hasa kutokana na utekelezaji usio wa kubabaisha wa ilani yake ya uchaguzi"
Ni kama litums paper ya kutest watu wanaonje mwenendo wa chama chenu kinachoelekea ukingoni mwa siaasa!!!

Shame on you for being slave willingly!!!!
 
BELIEVE or NOT, CCM ilikuwepo, ipo na itaendelea KUWEPO kwa miaka nenda, miaka rudi kwani SERA zake zimeimarika na zinaendelea kuimarika tofauti na vyama vyenu vilivyojaa wazandiki na wanafiki. UKAWA is going to collapse very soon.
 
Back
Top Bottom