Kuhusu Zanzibar Mpendwa Rais Amekosea

...Magufuli mjanja sana,kila nikisikiliza hotuba zake atasema msema kweli mpenzi wa Mungu,atarudia hiyo hata mara sabini.
Ila kwenye issue ya zanzibar kimyaaa..!!
 
Hivi kama sheria zipo wazi na zinamzuia mtu yoyote (hata mwenyekiti wa ZEC) kufuta uchaguzi, KWA NINI CUF hawafungui kesi mahakamani?

At least inaweza kuchelewesha kwanza huu uchaguzi Jecha alioutisha tarehe 20 March.Otherwise CCM wataendelea nao, Shein "atashinda" na CUF watapotezwa. Then Magufuri atapeleka wanajeshi kumtandika yeyote atakayeleta fujo kupinga serikali "iliyoshinda uchaguzi"

Busara kidogo na logic ibabidi itumike hapa. Sometimes misimamo mikali haileti tija
 
"Ujinga ni kuendelea na Uchaguzi kwa Tume ileile na namna ileile huku ukitegemea matokeo tofauti"
- Albeit Einstein

Shark;

Msimamo wangu hapa jukwaani ni kuwaunga mkono CUF na msimamo wao wa kuwaachia CCM waendelee na marudio ya uchaguzi wao chini ya Jecha wao;

Au, kama ni kushiriki uchaguzi mwingine basi, kwanza kwa hii ZEC chini Jecha kupigwa chini kisha awepo msimamizi huru wa uchaguzi utakaorudiwa. Hili liko ndani ya uwezo wa JPM na mwenzie Dr. Shein!

Ila hapa tunajadili kauli ya Rais wa JMT bwana JPM ya "nitaendelea kukaa kimya kuhusu kile kinachoendelea Zanzibar".

Ndo nikasema si afadhali hata angesema serikali za JMT na SMZ zinaendelea kulifanyia kazi ikiwemo kushauriana na CUF kukubali kushiriki wa uchaguzi wa marudio japo tunatambua na tunajua hawezi kuwashawishi kushiriki hiki kiitwacho na Jecha "uchaguzi wa marudio" kwa sbb ambazo ziko wazi!!
 
Nimekupata Mkuu wangu, uko sahihi sana 100%.
Uchaguzi uliharibika kwa makosa yaliyoko chini ya Tume, kuurudia kwa Tume ilele huku kukiwepo hakuna aliewajibishwa ndani ya Tume ni Usanii.

Ila kwa upande mwengine naona kama Bwana Magu uwezo wake ni mdogo sana compare to level ya huu Mgogoro wa Zanzibar. Ikitokea Uchaguzi ukarudiwa basi ni faida kubwa kwa CCM ambayo yeye Magu hana hata cheo cha ukatibu tarafa pale Chamani. Wenye chama chao ambao yeye yuko chini yao ndio wanaotaka uchaguzi urudiwe, yeye pale hawezi kwenda kinyume na matakwa ya Chama.
 
sasa huo usuluhisho unakujaje ikiwa maalim seif 'ameweka mpira kwapani, na kutoka uwanjani'? hataki mazungumzo ameshajitoa, wakisema uchaguz urudiwe hataki pia, hv unafikir kwa situation kama hyo, unataka maguful afanyaje?
 
Hana uwezo wa kuingilia mgogoro ila ana uwezo wa kuleta majeshi kutuliza mgogoro huo?ok fine sasa tunamwambia magu na ccm wenzake tanganyika wauweni wazanzibar wote ila kwa hili wala hawatorudi nyuma.
 

..Anaweza kufanya jambo moja ambalo mimi naamini liko ndani ya uwezo wake hata bila kushirikisha chama chake.

..Dr. Shein ni mjumbe ktk baraza la mawaziri katika serikali ya JMT na ndiye kinara (central figure) ya mgogoro huu.

...Aweza kumwita na kukaa naye na kumshauri njia bora za kufanya kuikoa Zanzibar kuingia ktk machafuko ikiwemo akubali yeye kama yeye kushindwa au atumie mamlaka yake kama Rais wa SMZ kuiamuru ZEC kuendelea na kukamilisha kazi ya kutangaza matokeo

...Hili sidhani kama linahitaji maamuzi ya chama japo bado kinaweza kuwaingilia na pengine hata kuwachukulia hatua ikiwepo kuwanyang'anya kadi zao japo pia ni hatua ngumu na ya hatari zaidi kwa chama!

...I still believe JPM na Dr Shein kwa mamlaka ya kikatiba waliyonayo (nje ya yale ya kichama) wanaweza kufanya kitu ili kufikia peaceful resolution ya mgogoro huu pasipo kusababisha umwagaji damu au kuumiza raia wasio na hatia yoyote!

...Pia wanaweza kuagiza kubadilishwa haraka kwa baadhi ya sheria ambazo wanaziona ni kikwazo kwao hata kukipa chama "supremacy" ktk maamuzi ya baadhi ya mambo ya kitaifa kama haya!

...Kiukweli watu waliwachagua JPM na Dr Shein na siyo vyama vyao. Wabebe dhamana hii muhimu kutumikia wananchi na sio chama!!
 
Mi
Binafsi namuunga mkono JPM kwa mambo mengi anayofanya. Kama ni kumpa ranking kati ya 1 na 10 amnapo 10 ni alama ya juu kabisa na 1 ya chini ningempa 9. Ila kwa jinsi anavyoshughulikia suala la Znz ningempa 1!
 
Hayo unasema weww, yeye hakjsema hivyo.
 
Halafu kulikua na sababu gani yeye kama Amiri jeshi mkuu kutoa vitisho vya wazi kabisa ??? Kama aliamua kukaa kimya si angekaa kimya mpaka mwisho wake ?? Halafu sina tatizo na vitisho hiyo ni njia ya kawaida kabisa inayotumika kwenye serikali duniani ila zinapitia idara husika sio kwa raisi moja kwa moja ,angewaachia kazi hiyo vijana wake wa usalama wa taifa
 
Keep it up!

Andiko lako limemaliza kila kitu.

Waliamua kuwa wanafiki na ndumila kuwili kwa sasa unafiki wao unawatafuna.

Nimejadili sana kwenye hii thread;
 
Mie ningeshauri uchaguzi usimamiwe na tume ingine cuf. Hawana imani na tume hii ni vizuri maridhiano yakafanyika bio ndio njia nzuri itakayo jenga UMOJA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…