Kuhusu vocha za simu,hii inakuwaje??

Kuhusu vocha za simu,hii inakuwaje??

Mrimi

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
1,691
Reaction score
641
Wakuu nasikia hizi kampuni za mitandao ya simu zinaprovide tu network lakini hazihusiki na utengenezaji wa vocha za airtime,hii inakuwaje?

Na ni makampuni gani kwa hapa kwetu yanahusika na utengenezaji wa hizo vocha?

Na je kampuni moja inaweza kutengeza vocha kwa makampuni ya simu zaidi ya moja,kwa mfano ikawa inatengeneza vocha kwa ajili ya voda na tigo kwa wakati mmoja?
 
Wakuu naon mnapita kimya kimya,hakuna mwenye ufahamu na hili?!
 
Kuna mambo mawili hapa. 1. kutengeneza vocha 2. kusimamia vocha. Sina hakika kama kampuni hazihusiki moja kwa moja na utengenezaji wa vocha. Hata kama hazihusiki katika utengenezaji basi zitahusika katika usimamizi mambo fulanifulani. Mfano kuna kampuni inaitwa Shivacom hii inafanya kazi upande wa Voda kwa miaka mingi sasa ingawa sina hakika kama inashughulikia utengenezaji au ni usambazaji pekee.
 
Hilo ni kweli kiongozi. Ni kama ticket za mabasi, si lazima mwenye basi awe na kiwanda cha kutengeneza ticket. Kampuni za simu zote zina wazalishaji wao ambapo haikatazwi kuzalisha vocha za kampuni zaidi ya moja, mfano Airtel na tiGo. Kinachozalishwa inhouse (yaani na kampuni za simu) ni data (mtaani mnaita pin). Hizo outsourced company zinazalisha makaratasi kwa brand na data specification walizopewa na wateja wao.

Mfano kuna kampuni moja hapa Tanzania (sitoitaja jina kwa sababu za kibiashara) ambayo inafanya kazi ya printing ya vocha za simu, kadi za ATM, vitambulisho vya smart card etc etc.

Ni kama kwenye magazeti, kuna kampuni za printing ambapo wenye magazeti mbali mbali wanapeleka magazeti yao kwa ajili ya kuprint, so sio lazima kila gazeti liwe na printing facility zake.

So hiyo ni kawaida tu mkuu, hata kampuni kubwa kama Apple ambao ndo watengenezaji wa bidhaa kama iphone, ipad etc etc hawatengenezi kila kitu wenyewe (zaidi wao wana deal na kudesign na kutengeneza software basi, hardware prod wanafanya outsourced companies huko China).

Pia Tanzania kwa sasa, makampuni ya simu sio lazima wawe na site (minara) kila sehemu wanapotaka kuweka huduma zao. Mfano tiGo sasa hivi hawamiliki mitambo yoyote kwani wameiuzia kampuni fulani (jina kapuni) ambayo inafanya biashara ya minara.
 
Mkuu nimekuelewa vizuri kabisa,ila hujanijibu swali la pili,kwamba hapa kwetu ni makampuni gani yanayotengeneza hizo vocha?

Na je hizo vocha zikishatengenezwa,mambo ya uuzaji kwa wateja ni nani anahusika?Kwa mfano,vocha voda au airtel zikiwa tayari,zinawafikiaje wholesellers/agents?
 
Mkuu majibu ni kama ifuatavyo;

1. kampuni mojawapo ni MGT Tanzania Ltd na wengineo (wengine wanaagiza toka China, India, Dubai, Kenya etc)

2. Kwa kampuni za simu za hapa nchini, usambazaji wa vocha unafanywa na kampuni zenyewe kwa kutumia outsourced transporters

3. Wateja wao zinawafikia kupitia wateja wakubwa wa haya makampuni (yaani Super Dealers) ambao wholesalers wa mitaani wanaenda kununua vocha kwao then wao (wholesalers) ndo wanauza kwa retailers (ambako mteja mmoja mmoja ndo anakonunua vocha akitaka ku recharge simu yake).

Naamini nimekujibu maswali yako mkuu.
 
Back
Top Bottom