Kuhusu ukarabati wa Bombadier zetu

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
501
1,214
Naomba, kwa niaba ya wazalendo wenzangu wa Isansa Mbozi nitoe ufafanuzi kuhusu na kilichoandikwa na gazeti la NIPASHE la leo tarehe 14 January 2019, kwenye kichwa cha habari _"Bil 13.9 kukarabati Bombadier Canada"_

Ni kwamba tarehe 10 mwezi huu, mh waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandidi Isack Kamwele , alialikwa kama mgeni rasmi katika chuo cha usafirishaji( NIT) katika uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege

Katika hotuba yake, alieleza changamoto katika sekta hii ya usafiri wa anga hapa nchini, mojawapo ya changamoto aliosema, ni ukosefu wa karakana( Hanga) za kukarabati ndege zenye ubora na ukubwa wa kutosha hapa nchini

Hivyo akasema kwa mfano mwakani wanapaswa kupeleka ndege zetu 2 za bombadier kwa ajili ya kuzifanyia service( Schedule service), kwa kawaida kila ndege ina muda wake maalumu wa kufanyiwa service kutokana na flying hours, ambapo kwa bombadier Q 400 hufanyiwa service kila baada ya masaa( Flying hours) 600 ya kuwa angani

Na akasema, kama watapeleka ndege hizo nchini Canada kwa ajili ya service itawagharimu serikali takribani $ 3m kwa ndege moja na $ 6m kwa ndege zote mbili

Lakini akasema, baada ya kuambiwa hilo, alimfuata mh Rais na kumuomba apewe fedha kwa ajili ya ukarabati wa hanga yetu, iliyopo katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro( KIA) ambapo kimsingi ombi lake lilikubaliwa na mh Rais, na serikali wameshaanza ukarabati mkubwa katika hanga hiyo na pia wameshaingia mikataba 3, ikiwemo ya kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya ukarabati wa ndege zetu

Na yote hii, inafanyika ili tuweze kuokoa fedha nyingi za kupeleka ndege Canada kwa ajili ya service

Binafsi kama mzalendo nitoe wito, hasa kwa vyombo vya hsbari kama magazeti, kujiepusha kuwa na vichwa vya habari vyenye kuweza kupotosha umma,

Nadhani kwa hili la NIPASHE, nina imani mamlaka husika zitachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo

Mzalendo
_Ngamanya Kitangalala_
 
“Kujipendekeza ni dalili ya kudharau uwezo wako wa akili na kuacha tumbo kuongoza mwili”
By Allency


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom