Kuhusu ujinsi wa binadamu: Lisemavyo gazeti la Kiongozi kuhusu wanawake, wanaume na mahunta

Kuhusu ujinsi wa binadamu: Lisemavyo gazeti la Kiongozi kuhusu wanawake, wanaume na mahunta

Doctor Mama Amon

Platinum Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
2,311
Reaction score
3,490
Wajibu wa kisheria na kijamii kulingana na jinsi

Na Raphael Kamuli

(Chanzo: Kiongozi, Toleo Na. 32, Tarehe 09-15 Agosti 2019, ukurasa wa 12, ISSN 0856-2563.)



1568536657681.png

Popes in the History of AMECEA

Wanaharakati wa vuguvugu la [mapenzi ya jinsi moja] wamekuwa wakitumia njia mbili kuhalalisha mapenzi [hayo] kikatiba na kisheria.

Kwanza wamekuwa wakishinikiza au kushawishi watunga Katiba au sharia kuweka “mwelekeo wa kimapenzi” kama mojawapo ya misingi ya usawa. Walifanikiwa kufanya hivyo nchini Afrika kusini na kufanya nchi hiyo kuwa ya kwanza duniani kutambua usawa kwa msingi wa “mwelekeo wa kimapenzi.”

Pili, wamekuwa wakijenga hoja potofu kuwa “jinsi” na “mwelekeo wa kimapenzi” ni dhana moja. Mwelekeo wa kimapenzi ukiwa ni msingi wa usawa kikatiba au dhana ya [jinsi] na mwelekeo wa kimapenzi vikihesabiwa kuwa ni dhana moja, sheria zote zinazopinga [mapenzi ya jinsi moja] zinakuwa batili.

[Makala hii inakusudia kuonyesha kwamba mikakati yote miwili kwa ajili ya kuhalalisha mapenzi ya jinsi moja kikatiba na kisheria inapingana na kanuni za haki na majukumu asilia yanayotambuliwa na Katiba ya Tanzania.]

Jinsi hubeba wajibu, na hapo ndipo neno “jinsia” huzaliwa. Jinsia ni wajibu wa kijamii wa binadamu kulingana na jinsi. Kwa hiyo, wakati “jinsi” ni suala la kibayolojia, “jinsia” hubeba matazamio ya jamii juu ya jinsi. Wajibu wa msingi kwa binadamu kulingana na viungo vya uzazi ni kuzaliana, kwa lugha ya Kiingereza “procreation.”

Viungo na maumbile ya binadamu kulingana na jinsi vimetengenezwa kwa sababu hiyo [ya kuzaliana]. Hivyo, maumbile ya binadamu yanatakiwa kutumika kulingana na mpangilio na utaratibu uliokusudiwa [na Mungu wa maumbile]. Ni ukweli usiopingika kuwa kujamiiana kumekuwa kukifanyika kwa sababu zaidi ya kuzaana.

[Kulingana na maandiko ya Padre Bernard Joinet, sababu nyingine ni pamoja na kuonyesha ukarimu, kutoa shukrani, kutafuta kipato, na kuburudishana.]

Hata hivyo, kujamiiana kukifanyika kinyume cha utaratibu na mpangilio wa maumbile huo ni ubatili [kwa kuwa hiyo ni haki batili].

Jamii zilizostaarabika zimejemga utamaduni wa kutambua na kudumisha wajibu wa binadamu kulingana na jinsi. Jamii hizo pia zimejenga matarajio kuwa binadamu anapaswa kutambua na kuuishi utamaduni huo.

Wajibu huo unakwenda mbali zaidi ya kazi na umuhimu wa viungo vya [jinsi] na kujumuisha wajibu wa binadamu wa jinsia moja kwa watu wa jinsia nyingine na kwa jamii.

Kwa mfano, sheria ya ndoa ya Tanzania imemwekea mwanamume wajibu wa kumtunza mkewe. Kwa hiyo, jinsia sio jambo binafsi, ni jambo la kijamii na kisheria.

Kwa utamaduni wa Magharibi maisha ni jambo binafsi. Mtazamo wa kijamii hautiliwi maanani sana.

Barani Afrika na Asia mtazamo juu ya maisha ni tofauti. Kwa sehemu hizo, maisha ni jambo la kijamii. Kwa hiyo, haki batili ya kuchagua mwelekeo wa kimapenzi imebeba mtazamo wa kimagharibu.

Kijinsia mtazamo huo wa kimagharibi sio sahihi kwa sababu jinsi ni jambo asilia na tofauti inayotokana na jinsi ni ya kudumu. Hvyo, mtu hawezi kujichagulia mwelekeo [wa kimapenzi] kadiri atakavyo.

Kwa hiyo, jinsi ni alama yenye kuonesha tofauti kati ya mwanamke na mwanamume na ni kitu cha kudumu. Hivyo basi, binadamu hawezi kujichagulia mwelekeo wa kimapenzi kwa kadiri atakavyo. Mwelekeo pekee sahihi wa kimapenzi ni kujamiiana na [m]wenza wa jinsi tofauti.

Mwelekeo huo [wa uheterofilia] unatokana na asili ya binadamu [walio wengi], utaratibu na mfumo wa viungo vya mwili vya mwanadamu na majukumu ya kijamii ya mwanadamu kulingana na jinsi. Huo ndio ustaarabu [kwa muibu wa haki na majukumu asilia ya binadamu walio wengi.]

Suala la mwelekeo wa kimapenzi kikatiba na kisheria.

Sheria huakisi maisha, mtazamo, ustaarabu na matarajio ya jamii au nchi husika. Sheria pia hubainisha matendo halali na haramu. Msingi wa sheria ni katiba [ya nchi]. Katiba [ya nchi] ndio sharia “mama.” Kila sheria inapaswa kufuata misingi ya Katiba [ya nchi]. Sheria yoyote inayopingana na Katiba [ya nchi] ni batili.

Katiba hulinda makundi ya watu kwa kukataza ubaguzi kwa makundi hayo kwa misingi Fulani. Lengo la katiba kukataza ubaguzi kwa misingi Fulani ni kulinda makundi dhaifu au kulinda misingi ya utu, ustaarabu na demokrasia.

Kwa mfano, Katiba hulinda utu kwa kukataza ubaguzi kwa misingi ya hadhi ya kijamii, katiba hulinda wanawake kwa kukataza ubaguzi kwa misingi ya jinsi, na katiba hulinda demokrasia kwa kukataza ubaguzi kwa misingi ya maoni ya kisiasa.

Katiba ya Tanzania inakataza ubaguzi kwa misingi ya utafifa, kabila, mahali mtu anapotokea, maoni ya kisiasa, rangi, dini, jinsi [na] hali au hadhi ya mtu katika jamii. Misingi hii ya ubaguzi hufanya watu wa aina Fulani kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni. Kwa hiyo, kwa kukataza ubaguzi Katiba inajenga usawa mbele ya sheria katika mambo halali [yanayotambuliwa kama haki za kikatiba].

Katiba ya Tanzania haitambui usawa kwa msingi wa mwelekeo wa kimapenzi. Hii ni tofauti na Katiba ya Afrika Kusini, kwa mfano, ambayo inatambua wazi usawa katika msingi wa mwelekeo wa kimapenzi. Kwa hiyo, nchini Afrika Kusini ni haki ya kikatiba kwa mtu kujichagulia mwelekeo wa kimapenzi. Haki hiyo inalindwa kisheria nchini humo kwa sababu msingi wake ni Katiba, japo haki hiyo imejengwa juu ya msingi potofu kama ilivyoelezwa awali.

Katiba ya Tanzania inalinda usawa kwa msingi wa jinsi. Kama ilivyoelezwa kwa kirefu hapo awali tafsiri halisi ya jinsi haipelekei haki ya kujichagulia mwelekeo wa kimapenzi. Kwa hiyo, kwa kuwa Katiba ya Tanzania haijataja wazi haki ya usawa kwa msingi wa mwelekeo wa kimapenzi haki hiyo haiwezi kuhesabika kuwa ni sehemu ya usawa kwa msingi wa jinsi.

Kuna tafsiri potofu kuwa neno jinsi linamaanisha pia mwelekeo wa kimapenzi. Tafsiri hii haina ukweli na ni upotoshaji mkubwa na wa makusudi. Maneno jinsi na mwelekeo wa kimapenzi yana tofauti. Kimsingi, hata neno jinsi na jinsia yana tofauti. Ndiyo maana hata katiba ya Afrika Kusini imeyaweka tofauti.

Katiba hiyo, pamoja na misingi mingine, inakataza ubaguzi kwa misingi ya jinsi, jinsia, na mwelekeo wa kimapenzi. Kama maneno haya yangekuwa na maana moja lingewekwa neno moja kuwakilisha misingi hiyo mitatu.

Kwa hiyo, ni sahihi kwa sheria za Tanzania kuharamisha mwelekeo wa kimapenzi ambao unahusisha mapenzi ya jinsia moja. Msingi wa sheria hizo ni Katiba.

Iwapo sheria za nchi zingeruhusu mapenzi ya jinsi moja, zingekuwa zinakiuka Katiba na hivyo sheria hizo zingekuwa batili [kwa mujibu wa katiba].

Angalizo:

Makala hii imehakikiwa na Mama Amon kwenye jukwaa hili mahali hapa: https://www.jamiiforums.com/threads...aka-ya-kusanifu-fasili-ya-kitu-hicho.1630455/
 

Attachments

  • 1568460009025.png
    1568460009025.png
    31.3 KB · Views: 37
Back
Top Bottom