Kuhusu tendo la ndoa/ngono

fakalava

JF-Expert Member
Jul 16, 2015
4,459
6,027
74579390-african-couple-cuddling-in-bed-gettyimages-jpg.317209


Tendo la ndoa ni kitu cha muhimu sana kuimarisha mahusianao hasa kwa wanandoa, pia hata wapenzi ambao hawajaoana suala la tendo la ngono kwa wengi eso huwa ni la kipaumbele sana.

Kuna baadhi ya makosa madogo madogo huwa yanafanyika kwenye mahusiano lakini yakiachwa bila kuyashughulikia gharama ya kuyarekebisha huwa ni kubwa.

Leo ningependa kwa uchache tuongelee tendo la ndoa (ngono kwa wasiyo wanandoa).
082df188652354233bdd03d01af8e240.jpg


f2649f4759b83792a6e7ebbadb9272d5.jpg


Madhumuni ya tendo la ndoa kwa wanandoa, pamoja na kupata watoto (majaliwa ya mwenyezi Mungu) ni kufurahishana, kila mmoja anapashwa kulifurahia tendo hili ili kuleta maana halisi ya tendo la ndoa.

Kuna makosa kadha wa kadha ambayo wanandoa huyafanya na kusababisha tendo hili lisiwe na maana sahihi kwenye ndoa yao.

Baadhi ya makosa.

  1. Kufanya tendo la ndoa kumridhisha mwenzako.
f303ada980907e681aaab8d05a956f02.jpg

Kuna baadhi ya wanandoa/wapenzi hupitia kwenye kipindi ambacho kwa sababu mbalimbali huwa hawajisikii kushiriki tendo, lakini hufanya tu kwa kuwaridhisha wenza wao, kadhia hii huwakumba hasa wanawake maana wamefundishwa kuwa wakati wowote mwanaume akitaka mpe, (kwa sababu ya utandawazi hii hali imeanza kupungua).

Kuna idadi kubwa ya wanawake wanaolazimishwa kufanya tendo la ndoa bila wao kulidhia, ambayo kwa sasa inaitwa ubakaji ndani ya ndoa, japo hili neno "ubakaji kwenye ndoa" wanaume hawakubaliani nalo.

Inapotokea hali ya mpenzi/mwenza kutokuwa tayari kufanya tendo, unashauriwa huwe na subira ya kumpa mwenzako nafasi mpaka atakapokuwa tayari kushiriki hili tendo hasa kwa kuongea naye kujua ni nini kimemsibu.

2. Kukataa makusudi kushiriki tendo hili kukomoa mwenza wako.
d02bee07f781318bd721691ba3432e44.jpg

ba1521c247e83bdce0d992d496bc97a0.jpg


Kuna baadhi ya wanandoa/wapenzi hasa wanawake ambao hudhani kuwa njia hii ni sahihi kuwaadhibu Waume/wapenzi wao.Binafsi hii njia siiungi mkono maana kuna wanawake walioitumia ikashindwa kuleta matokeo waliyoyategemea, badala yake imeleta vilio.
Kama nilivyosema hapo awali, njia sahihi ya kumaliza migogoro kwenye mahusiano ni mazungumzo/maongezi wala si kufungiana vioo na kuwekeana mipaka ambayo inawezakuwa ndilo kaburi la mahusiano yenu.

Mwisho nitoe rai kwa wanandoa/wapenzi.

Ni vyema kuzijua tabia za mwenzako na kuzihimili na zaidi kusaidi abadilike kutoka kwenye tabia ambazo hazikupendezi.

Wanaume kumbukeni hili siyo mara zote mwanamke akikwambia hakupi "K" huwa anamaanisha lah.... wakati mwingine huwa anakupima, ni kwa kiasi gani yeye anathamani kwako, na pengine labda hujambembeleza au kumwambia maneno matamu muda mrefu sasa anatumia njia hii hili apate anachokiitaji. Ndiyo maana mwanamke anaweza asubuhi akakwambia, sikupi tena, lakini jioni ukala nzigo na kufuli akafungua mwenyewe.
5fabf52bc522cc41a73233ee0fc2d9ee.jpg

361c0aec7c6fe600ca72fba4feef5b75.jpg


Kumbuka mwanamke anaamini kuwa mwanaume anazijua hisia zake hata pasipo yeye kuzisema.

Tendo la ndoa ni tendo la kufurahishana.


Niwatakie weekend njema,

Mzee wa Vimwana a.k.a fakalava.
 

Attachments

  • 74579390-african-couple-cuddling-in-bed-gettyimages.jpg
    74579390-african-couple-cuddling-in-bed-gettyimages.jpg
    15.4 KB · Views: 1,330
  • 1-valentine-day-photography.preview.jpg
    1-valentine-day-photography.preview.jpg
    28 KB · Views: 199
  • 19-couple-photography.preview.jpg
    19-couple-photography.preview.jpg
    23.8 KB · Views: 175
Last edited by a moderator:
USHAURI MZURI ILA MDA MWINGINE MNAUDHI MTU ANAONA BORA AKUNYIME TU. WANAUME WENGI WANAJIJALI WENYEWE TU HAWANA MDA WA KUJUA MWENZAKE AMERIDHIKA AMA VIPI
 
USHAURI MZURI ILA MDA MWINGINE MNAUDHI MTU ANAONA BORA AKUNYIME TU. WANAUME WENGI WANAJIJALI WENYEWE TU HAWANA MDA WA KUJUA MWENZAKE AMERIDHIKA AMA VIPI
Kwa wenza wanaoridhiana na kuridhishana, hakuna anayetamani kumnyima mwenzake, bahati mbaya ni wanaume wachache waliofanikiwa kuzitambua hisia za wenza wao wa kike.
 
Back
Top Bottom