Kuhusu scanner ya KIA

Kuhusu scanner ya KIA

STINGER

Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
41
Reaction score
11
Jana kwenye gazeti la gardian septemba 19, 2019, nilisoma habari za kusikitisha na za kupotosha ambazo zinaweza kuathiri si utalii tu bali na hata usalama wa nchi yetu.

Habari hizi zilihusu kutokuwepo kwa huduma ya skana, ambacho ni chombo muhimu kwa uwanja wa ndege wowote duniani.

Habari hizi hazina ukweli wowote na zililenga kupotosha umma na kumharibia naibu waziri wa utalii na katibu mkuu wa wizara yake waliokuwa kwenye mkutano na wadau wa utalii pale moshi.

Nasema ni za kuwa haribia hawa wawili maana naibu waziri alinukuliwa kuwa aliyasema maneno hayo kuwa hakuna skana kwa miaka mitatu.

Pia kwenye habari hiyo ananukuliwa mkurugenzi mkuu wa kadco kuwa alikiri kuwepo na tatizo hilo jambo ambalo si kweli na pia amenukuliwa mwenyekiti wetu wa chama cha wamiliki wa makampuni ya watalii tato bw. molel kutoa malalamiko yanayohusiana na skana hiyo wakati si kweli.

Ukweli ni kuwa tulikwenda kwenye mkutano huo mzuri tukiwa na lenmgo jema huku tukiongozwa na mwenyekiti wetu. baada ya utambulisho mwenyekiti wa kikao alitoa fursa kwa wadau kuchangia kwa kueleza changamoto ambazo tunakumbana nazo wakati tukifanya kazi zetu pale kia na ndipo tukawasilisha moja baada ya nyingine kwa zamu.

Alichosema mwenyekiti wetu ni kuwa kukosekana kwa ubao wa taarifa za mwendendo wa muda wa ndege kwa miaka mitatu sasa ni changamoto kwa wageni na sisi tunaofanya huduma zetu pale. sasa kinachoshangaza ni wapi taarifa za kutokuwepo wka huduma za skana zilitokea wakati hata neno skana lenyewe sikumbuki kusikia likitajwa.

Taarifa hii ya gardian ilinipelkea kulitafuta gazeti la dailynews la jana hiyo hiyo ambalo niliambiwa lilikuwa na habari kuhusiana na mkutano ule na kukutanana taarifa tofauti kabisa na ile iliyotolewa na gardian, taarifa iliyokuwa kwenye dailynews ilielezea kwa usahihi kabisa swala linalohusiana na yale yaliyozungumzwa kuhusiana na huduma ambayo haiko pale kia kwa miaka mitatu ambayo ni ile ya kukosekana kwa ubao wa matangazo ya safari za ndege pamoja na kukosekana dawati la taarifa yaani information desk.

Kwa kweli taarifa ya gardian imenisikitisha na naamini iwapa wakati mgumu naibu waziri kanyaso na mkurugenzi wa kadco mukoma, nadhani kitakachowaokoa ni taarifa sahihi zilizoko kwenye dailynews na wale wote tuliohudhuria kwenye kikao hicho.

Taarifa ya gardian imekuja wakati mbaya kwa vile ni muda mfupi tu rais alizindua rada ya kimataifa na leo mtu anatokeza na kusema nchi haiko salama kwa uwanja wa ndege wa kimataifa kukosa skana. mimi najiuliza hata mhariri mwenyewe wa gardian hakuweza kuitathimni taarifa yenye mahusiano makubwa na usalama wa nchi kabla ya kuiidhinisha itoke tena kama taarifa kubwa ya gazeti?

Mimi nitoe rai kwa wanahabari wawe makini pamoja na wahariri wao, jana taifa lilitikisika kwa taarifa hiyo nzito, watu walimtafakari naibu waziri mara mbili mbili kama anawezaji kutoa taarifa yenye mashaka ambayo inagusa usalama wa nchi na kama siyo gazeti la dailynews kutoa habari iliyosahihi sambamba na ukweli tuliozungumza pale kwenye kikao bw. kanyaso angetakiwa kujitathmini kwa taarifa ambayo hakuitoa, ni wazi mhariri wagardian hana budi atafute gazeti la dailynews la jana asome habari ile halafu afanye tathmini ya ile aliyoletewa na mwakilishi wake.

Niwapongeze dailynews kwa maana wamemuokoa hata na mwenyekiti wangu molel ambaye angetafsiriwa kuwa anatoa taarifa za kupotosha umma.
 
jana kwenye gazeti la gardian septemba 19, 2019, nilisoma habari za kusikitisha na za kupotosha ambazo zinaweza kuathiri si utalii tu bali na hata usalama wa nchi yetu.

habari hizi zilihusu kutokuwepo kwa huduma ya skana, ambacho ni chombo muhimu kwa uwanja wa ndege wowote duniani.

habari hizi hazina ukweli wowote na zililenga kupotosha umma na kumharibia naibu waziri wa utalii na katibu mkuu wa wizara yake waliokuwa kwenye mkutano na wadau wa utalii pale moshi

nasema ni za kuwa haribia hawa wawili maana naibu waziri alinukuliwa kuwa aliyasema maneno hayo kuwa hakuna skana kwa miaka mitatu

pia kwenye habari hiyo ananukuliwa mkurugenzi mkuu wa kadco kuwa alikiri kuwepo na tatizo hilo jambo ambalo si kweli na pia amenukuliwa mwenyekiti wetu wa chama cha wamiliki wa makampuni ya watalii tato bw. molel kutoa malalamiko yanayohusiana na skana hiyo wakati si kweli

ukweli ni kuwa tulikwenda kwenye mkutano huo mzuri tukiwa na lenmgo jema huku tukiongozwa na mwenyekiti wetu. baada ya utambulisho mwenyekiti wa kikao alitoa fursa kwa wadau kuchangia kwa kueleza changamoto ambazo tunakumbana nazo wakati tukifanya kazi zetu pale kia na ndipo tukawasilisha moja baada ya nyingine kwa zamu

alichosema mwenyekiti wetu ni kuwa kukosekana kwa ubao wa taarifa za mwendendo wa muda wa ndege kwa miaka mitatu sasa ni changamoto kwa wageni na sisi tunaofanya huduma zetu pale. sasa kinachoshangaza ni wapi taarifa za kutokuwepo wka huduma za skana zilitokea wakati hata neno skana lenyewe sikumbuki kusikia likitajwa

taarifa hii ya gardian ilinipelkea kulitafuta gazeti la dailynews la jana hiyo hiyo ambalo niliambiwa lilikuwa na habari kuhusiana na mkutano ule na kukutanana taarifa tofauti kabisa na ile iliyotolewa na gardian, taarifa iliyokuwa kwenye dailynews ilielezea kwa usahihi kabisa swala linalohusiana na yale yaliyozungumzwa kuhusiana na huduma ambayo haiko pale kia kwa miaka mitatu ambayo ni ile ya kukosekana kwa ubao wa matangazo ya safari za ndege pamoja na kukosekana dawati la taarifa yaani information desk

kwa kweli taarifa ya gardian imenisikitisha na naamini iwapa wakati mgumu naibu waziri kanyaso na mkurugenzi wa kadco mukoma, nadhani kitakachowaokoa ni taarifa sahihi zilizoko kwenye dailynews na wale wote tuliohudhuria kwenye kikao hicho

taarifa ya gardian imekuja wakati mbaya kwa vile ni muda mfupi tu rais alizindua rada ya kimataifa na leo mtu anatokeza na kusema nchi haiko salama kwa uwanja wa ndege wa kimataifa kukosa skana. mimi najiuliza hata mhariri mwenyewe wa gardian hakuweza kuitathimni taarifa yenye mahusiano makubwa na usalama wa nchi kabla ya kuiidhinisha itoke tena kama taarifa kubwa ya gazeti?

mimi nitoe rai kwa wanahabari wawe makini pamoja na wahariri wao, jana taifa lilitikisika kwa taarifa hiyo nzito, watu walimtafakari naibu waziri mara mbili mbili kama anawezaji kutoa taarifa yenye mashaka ambayo inagusa usalama wa nchi na kama siyo gazeti la dailynews kutoa habari iliyosahihi sambamba na ukweli tuliozungumza pale kwenye kikao bw. kanyaso angetakiwa kujitathmini kwa taarifa ambayo hakuitoa, ni wazi mhariri wagardian hana budi atafute gazeti la dailynews la jana asome habari ile halafu afanye tathmini ya ile aliyoletewa na mwakilishi wake

niwapongeze dailynews kwa maana wamemuokoa hata na mwenyekiti wangu molel ambaye angetafsiriwa kuwa anatoa taarifa za kupotosha umma
Jamani si tumeomba "RADHI" kwani hamjatusamehe tu..!!!!
IMG_20190920_132222_627.JPG
 
Back
Top Bottom