Kuhusu Sala ya Eid Al Fitr; Ukweli mchungu: BAKWATA wako sahihi kabisa

Jamani Tanzania mwezi haujaonekana. Kaman kuna aliyeuona aseme kauona wapi. Acheni mihemko na papara za kutaka kufanya maovu mliyojipangia tangu mwezi uanze, alaaaa
 
Dah...mkuu...Mwezi (Moon) una maana kubwa kiimani... Umewahi kujiuliza kwanini tarehe ya Pasaka hubadilika badilika?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu bado pasaka inajulikana itakuwa tarehe ngapi na lini, haya mambo yanaleta sintofahamu sana kwenye jamii,kwa maana utasikia wengine wanaanzwa kuswali na wengine wanakuwa bado.
 
Mkuu bado pasaka inajulikana itakuwa tarehe ngapi na lini, haya mambo yanaleta sintofahamu sana kwenye jamii,kwa maana utasikia wengine wanaanzwa kuswali na wengine wanakuwa bado.
Mkuu...tofauti ya Pasaka na Ramadhani....Pasaka wanaangalia mwezi mn'gaavu (Full moon) ambao ni rahisi kuuona.... Waislam huangalia mwezi muundamo ambao hubadilika badilika kutokana na mizunguko ya Jua, Dunia na Mwezi. (Rejea: Kupatwa kwa Mwezi - Sayansi darasa la tatu la zamani)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana jukwaa, nimejaribu kufuatilia maoni mengi kuhusu tangazo la Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania, Shekh Zuberi bin Ally, nakugundua watu wengi kama hawajakubaliana na tangazo lake alilosema mwezi haujaandama hivyo siku ya Alhamisi haitakuwa sikukuu baadala yake tutafunga na kutimiza siku 30 na sikukuu kuwa Ijumaa.

Kwa upande mwingine ukuaji wa technology hasa ya habari na mawasiliano imesaidia watu kupata taarifa za nchi kadhaa duniani zilizotangaza kusali Eid Al Fitr kesho Alhamisi kuanzia nchi za kiarabu hadi huku kwetu East Africa. Kwa mfano majirani zetu Rwanda, Malawi na kwingineko nimeona barua za Baraza yao ya Kiislamu yakisema Eid ni kesho.

ILa kitu cha ajabu ukiangalia nchi zote hizo hasa za ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na kati hakuna Baraza la Kiislamu la nchi yoyote ile iliyosema kuwa mwezi umeonekana sehemu fulani, mkoa, fulani au eneo fulani zaidi ya kutoa matangazo tu ya kusema Eid ni Keaho!

Hii ni kinyume kabisa na mafundisho ya dini yetu ya Kiislamu hasa kuhusu kusherekea kwa Eid kwani mafundisho yanasema fungeni (Ramadhan) kwa kuuona mwezi na funguueni (Eid Al Fitr) kwa kuuona mwezi au kama hamjauona basi malizieni siku 30. Kwa mutadha huo, BAKWATA wako sahihi kabisa na usiangalie nchi ngapi zinasali kesho maana nchi zote hizo hakuna nukuu ya kusema mwezi umeonekana zaidi ya kusema kesho ni Eid.

Huu ndio ukweli ndugu zangu BAKWATA wako sahihi kabisa. Wasalam
 
WINGER_TEREZA njoo utetee na hili la mwaka huu.
Kadhi wa Kenya jana ametangaza mwezi umeonekana Lamu na leo ni Eid, huku viongozi wetu wa bakwata wanatudanganya kua mwezi haujaonekana Tanzania bara, Zanzibar wala Kenya
Ukweli mchungu ni kwamba Bakwata hawana mamlaka ya kutangaza mwezi mpaka wapewe go ahead na sisiem makao makuu.
Bongo wanasiasa ndio wenye mamlaka ya kutangaza mwezi kwa kuzingatia protocol.
WINGER_TEREZA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom