Kuhusu Sala ya Eid Al Fitr; Ukweli mchungu: BAKWATA wako sahihi kabisa

vipi siku hiyo ya muandamo wa mwezi kukawa na mawingu?

vipi Kwa wale wasioona (vipofu) na mwezi hawauoni?

mipaka ya uonaji mwezi ipo kimikoa,nchi, kanda , bara or?

Kwako shekh mtoa mada.
 
UPUUZI MTUPU! JIONGEZE kwenye elimu dunia ili kujua kwamba duniani kuna mwezi mmoja tu na si miezi elfu kumi hivyo kokote kule utakapoonekana basi waislamu kote duniani watasherehekea Eid na haya mambo ya kutazama mwezi ni ya mwaka 47 siku hizi nchi nyingi Uarabuni wanafuata kalenda ambayo ipo 110% accurate.
mbona jua linapochomoza kokote watu hawaanzi kwenda kazini!
 
Habari wana jukwaa, nimejaribu kufuatilia maoni mengi kuhusu tangazo la Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania, Shekh Zuberi bin Ally, nakugundua watu wengi kama hawajakubaliana na tangazo lake alilosema mwezi haujaandama hivyo siku ya Alhamisi haitakuwa sikukuu baadala yake tutafunga na kutimiza siku 30 na sikukuu kuwa Ijumaa.

Kwa upande mwingine ukuaji wa technology hasa ya habari na mawasiliano imesaidia watu kupata taarifa za nchi kadhaa duniani zilizotangaza kusali Eid Al Fitr kesho Alhamisi kuanzia nchi za kiarabu hadi huku kwetu East Africa. Kwa mfano majirani zetu Rwanda, Malawi na kwingineko nimeona barua za Baraza yao ya Kiislamu yakisema Eid ni kesho.

ILa kitu cha ajabu ukiangalia nchi zote hizo hasa za ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na kati hakuna Baraza la Kiislamu la nchi yoyote ile iliyosema kuwa mwezi umeonekana sehemu fulani, mkoa, fulani au eneo fulani zaidi ya kutoa matangazo tu ya kusema Eid ni Keaho!

Hii ni kinyume kabisa na mafundisho ya dini yetu ya Kiislamu hasa kuhusu kusherekea kwa Eid kwani mafundisho yanasema fungeni (Ramadhan) kwa kuuona mwezi na funguueni (Eid Al Fitr) kwa kuuona mwezi au kama hamjauona basi malizieni siku 30. Kwa mutadha huo, BAKWATA wako sahihi kabisa na usiangalie nchi ngapi zinasali kesho maana nchi zote hizo hakuna nukuu ya kusema mwezi umeonekana zaidi ya kusema kesho ni Eid.

Huu ndio ukweli ndugu zangu BAKWATA wako sahihi kabisa. Wasalam
Hivi wewe umashawahi kujiuliza miaka hiyo watu walikuwa wanaishi vipi? walikuwa mabedui wamesambaa kila sehemu kusafiri mji mmoja kwenda mwingine ilikuwa ni masiku. Wakati huo hakukuwa hata na mipaka kujuwa hii nchi fulani hii nchi fulani. Binadamu tumepata maarifa elimu imekuwa kwa tafsiri yako hio ikiwa mimi niko Mwanza hatujauwona na Dar wameona sina haki ya kuwafuata Dar sababu mimi niko sijauowona tech imeongezeka njia za mawasiliano zimekuwa bora kabisa tukio linaweza kunaswa life na binadamu kujiongeza tu yako mambo mengi yalishushwa wakati ule kutokana na mazingira ya wakati ule. Miaka ya 80 tulikuwa na tabia watu wanasikiliza radio wakisikia nchi za kiarabu wana swali Eid sisi tunasema kwetu kesho kutokana na mazingira ya wakati ule kupiga simu Dar to Iringa tu mfano ilikuwa ni kasheshe habari zilikuwa haziendi kabisa. Jiongezeni waislamu tutabaki tunadharauliwa kila siku kwa mambo madogo kama haya yasio kuwa natija ndio maana miaka ile tulikuwa tunaswali sote pamoja leo ni kama kuna dini mbili wamevuruga hata furaha ya Eid. ingeundwa kamati huru sio ya Bakwata wala jumuia ingine wao na jukumu hilo bila kuingiliwa na taasisi yoyote ndio solution turudi ziku za furaha kama zamani. Bakwata siasa nyingi viongozi wa serikali lazima wafit ratiba zao hatuwezi kwenda hivyo. leo utakuta maelfu ya watu wameswali na kesho utaona. Nchi za EA tu majority leo kama sio zote.
 
mbona jua linapochomoza kokote watu hawaanzi kwenda kazini!
Wewe nawe punguza ujinga watu wanaenda kazini kwa saa sio kwa jua. Kuna nchi jua linatoka saa 4 asubuhi watu wanaenda saa moja bado giza kama usiku. Toka lini hata hizo shule umesikia miezi hii watoto wanenda shule saa 1 miezi mingine saa 2. Kazini ni muda labda itokee nchi fulani saa tofauti na nchi fulani.
 
vipi siku hiyo ya muandamo wa mwezi kukawa na mawingu?

vipi Kwa wale wasioona (vipofu) na mwezi hawauoni?

mipaka ya uonaji mwezi ipo kimikoa,nchi, kanda , bara or?

Kwako shekh mtoa mada.
Jana mawingu kila sehemu saa 2 wamejirishisha hakuna mwezi nchi nzima hata kufanya subira tu kuhakikisha hata kwa nchi jirani na leo wataona aibu mwezi utaonekana na watu wote sababu utakuwa mkubwa utashangaa. na ukionekana na watu wote basi juwa sio wa leo wa jana huo. siku ya kwanza kuona kwa mbinde unaweza kuoneshwa ule ule na usione.
 
Kuna miaka ya nyuma bakwata waliaibika sana.Limwezi la siku2 sie ndo tumakula Idd.Yani tulifunga siku ya Idd na tukala idd2.
Anaewaamini bakwaya hajui historia yao ya kutangaza mwezi.
Hata hii ya 2021 ni dhahiri tumeingia chaka naamini, ngoja jioni ifike tuone mwezi ww wa siku mbili tena
 
Uislamu ni ule ule dunia nzima, mwezi ni ule ule dunia nzima, kwanini tule sikukuu siku mbili tofauti.
Mwezi umeandama Saudia Arabia, Ulaya, Rwanda, Uganda nk. Halafu Bakwata wanasema bado haujaandama Tanzania! Kwanini Tz tuna mwezi wetu? Nchi imejaa makafir kibao, huo mwezi kuna watu watakuwa na muda wa kuufuatilia kama umeandama?
 
Nyakati nyengine Bakwata are plain stupid. Kuheshimu tamaduni za dini isiwe sababu ya kukana maendeleo ya sayansi hasa hili la muandamo wa mwezi. Siyo bure dini kuhimiza kuitafuta elimu hadi "uchina".
 
Hivi wewe umashawahi kujiuliza miaka hiyo watu walikuwa wanaishi vipi? walikuwa mabedui wamesambaa kila sehemu kusafiri mji mmoja kwenda mwingine ilikuwa ni masiku. Wakati huo hakukuwa hata na mipaka kujuwa hii nchi fulani hii nchi fulani. Binadamu tumepata maarifa elimu imekuwa kwa tafsiri yako hio ikiwa mimi niko Mwanza hatujauwona na Dar wameona sina haki ya kuwafuata Dar sababu mimi niko sijauowona tech imeongezeka njia za mawasiliano zimekuwa bora kabisa tukio linaweza kunaswa life na binadamu kujiongeza tu yako mambo mengi yalishushwa wakati ule kutokana na mazingira ya wakati ule. Miaka ya 80 tulikuwa na tabia watu wanasikiliza radio wakisikia nchi za kiarabu wana swali Eid sisi tunasema kwetu kesho kutokana na mazingira ya wakati ule kupiga simu Dar to Iringa tu mfano ilikuwa ni kasheshe habari zilikuwa haziendi kabisa. Jiongezeni waislamu tutabaki tunadharauliwa kila siku kwa mambo madogo kama haya yasio kuwa natija ndio maana miaka ile tulikuwa tunaswali sote pamoja leo ni kama kuna dini mbili wamevuruga hata furaha ya Eid. ingeundwa kamati huru sio ya Bakwata wala jumuia ingine wao na jukumu hilo bila kuingiliwa na taasisi yoyote ndio solution turudi ziku za furaha kama zamani. Bakwata siasa nyingi viongozi wa serikali lazima wafit ratiba zao hatuwezi kwenda hivyo. leo utakuta maelfu ya watu wameswali na kesho utaona. Nchi za EA tu majority leo kama sio zote.
Wote wameshajiongeza bado wabongo tu
 
Kwanini viongozi wa Dini wasiwe na Lugha Moja?
Wakae mezani wakakubaliana
Wakapeleka maombi serikalini tuwe na Eid mbili.

Watu tuvunje mifupa mara mbili
 
Tff hawafai kabisa hadi IDD wamesogeza Muda? Sie waislam tunafata msimamo wa yanga so IDD tunakula Leo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom