Kuhusu rufaa: Yanga yanyimwa alama 3 za bure

the muter

JF-Expert Member
Oct 31, 2012
1,330
1,799
Venance Ludovick amesimamishwa kucheza VPL mpaka suala lake litakapokamilika kusikilizwa, mpaka sasa imebainika ni kweli ana leseni mbili zilizotolewa na TFF ambazo ni za kuchezea Mbao na African lyon,

kwenye usajili wa mtandao TMS jina la Ludovick kule Mbao linasomeka Ludovick lakini African Lyon linasomeka Ludovic huku herufi K ikiwa imeondolewa, imeagizwa katika kikao kijacho wote kwa maana ya Mbao Fc ,

African Lyon pamoja na mchezaji wafike na vielelezo vyao vyote ili wafikie tamati, suala la African Lyon kupokwa point halitakuwepo kwa kua mpaka mchezaji anacheza tayali alipewa leseni na mmlaka halali TFF hivyo kosa linakua kwa TFF kumpa mtu leseni bila ya kikao cha kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kukaa means atakayeadhibiwa ni officer wa TFF aliyetoa leseni
 
chura churani wa jangwani walikuwa wanagojea point za bure imekula kwenu
 
Mlisema TFF ndiyo Yanga yenyewe sasa hapa imekaaje wakuu?
Matopeni wamewahi kupewa point za mezani na CAF.
Walikosa raha kuhisi Yanga watapata point za mezani.
Mpira una kanuni zake. Mwisho wa msimu kitaeleweka
 
Matopeni wamewahi kupewa point za mezani na CAF.
Walikosa raha kuhisi Yanga watapata point za mezani.
Mpira una kanuni zake. Mwisho wa msimu kitaeleweka


Hii habari nimechelewa kuipata.. kwanini lakini?? Ila hakijaharibika kitu.

We muhudumu uliovaa tshirt ya kijani, jeans ya njano na raba nyeusi, niongeze kinywaji tafadhali.
 
Timu imegeuka "Matonya FC" chezeni mpira hamna fadhila za kibure bure.Ushindi unapatikana uwanjani .Ushindi wa mezani badisheni timu iwe ya table tennis.
 
Venance Ludovick amesimamishwa kucheza VPL mpaka suala lake litakapokamilika kusikilizwa, mpaka sasa imebainika ni kweli ana leseni mbili zilizotolewa na TFF ambazo ni za kuchezea Mbao na African lyon, kwenye usajili wa mtandao TMS jina la Ludovick kule Mbao linasomeka Ludovick lakini African Lyon linasomeka Ludovic huku herufi K ikiwa imeondolewa, imeagizwa katika kikao kijacho wote kwa maana ya Mbao Fc ,African Lyon pamoja na mchezaji wafike na vielelezo vyao vyote ili wafikie tamati, suala la African Lyon kupokwa point halitakuwepo kwa kua mpaka mchezaji anacheza tayali alipewa leseni na mmlaka halali TFF hivyo kosa linakua kwa TFF kumpa mtu leseni bila ya kikao cha kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kukaa means atakayeadhibiwa ni officer wa TFF aliyetoa leseni
Moderator, Mhariri TFF wamekanusha hizi habari zilizoletwa hapa kuwa ni upotoshaji

"Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewataka wadau wa mpira wa miguu nchini wapuuze taarifa za kwenye mitandao kuhusu mchezaji Venance Ludovick.

Suala la mchezaji huyo linaendelea kufanyiwa kazi na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji. Tunawahakikishia umma wa wapenda soka nchini kuwa haki itatendeka kwa mujibu wa kanuni zinazoendesha mashindano husika.

..………….……….…………………………………………………………………..............

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) "

Source: KUHUSU MCHEZAJI VENANCE LUDOVICK
 
Back
Top Bottom