demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,288
- 15,238
Ndani ya saa 24 yatatoka Majibu ya Rufaa iliyokatwa na Mabingwa wa kihistoria wa LigiKuu Tanzania bara yaani Dar es Salaam Young Africans SC.
Kamati hiyo ndiyo yenyejukumu la kuamua kama Yanga inastahili alama mbili au kuendelea kuwa nyuma kwa alama nne kama ilivyokuwa sasa.
Klabu ya Yanga SC inaweza kupunguza gepu la alama 2 kati yake na wale waliowashikia nafasi yao, endapo tu itashinda rufaa yake iliyoikatia timu ya African Lyon, kwa kumchezesha mchezaji Venance Ludovic, huku akiwa hajakamilisha taratibu zake za uhamisho kutoka Mbao FC ya Mwanza.
Meneja wa Yanga Hafidhi, Salehe ameviambia vyombo vya habari, baada ya kupata taaarifa sahihi kuhusiana na mchezaji huyo waliamua kuwasilisha malalamiko yao kwa kamati ya rufaa iliyochini ya TFF, ili haki iweze kutendeka kama ambavyo sheria zinavyosema.
“Tulipata maelekezo ya kutosha na mchezaji huyo aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Awadhi Juma, na ndiyo alifunga bao la Lyon kabla ya sisi kusawazisha mchezaji huyo hajakamilisha taratibu zake za usajili kutoka Mbao na hata Mbao wenye wamemkatia rufaa,”amesema Hafidhi Afisa wa Yanga SC.
YANGA inaweza kukomboa pointi mbili ilizopoteza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya African Lyon baada ya sare ya 1-1 Desemba 23, mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kamati ya Saa 72, ambayo ndiyo inayosimamia ligi ya Vodacom inakutana leo na moja ya kesi ambazo itazisikiliza na kuzitolea maamuzi ni hiyo ya Yanga dhidi ya Lyon, kuhusiana na kumchezesha mchezaji huyo.
Lyon inadaiwa kukiuka taratibu za kumsajili mchezaji huyo kutoka timu ya Mwanza na rufaa mbili zimegongana mezani, moja ya Yanga na nyingine ya Mbao.
Klabu zote mbili Mbao na Yanga zinapinga Ludivic kuichezea Lyon akiwa mchezaji halali ya Mbao aliyoichezea mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Vodacom Tanzania.
Kwa mujibu wa vielelezo vilivyowasilishwa na Mbao, inaonekana kabisa Ludovic alihamia Mbao kimakosa na akatumika kimakosa pia, hivyo Yanga inaweza kushinda rufaa hiyo na kuvuna pointi mbili zaidi.
Katika mchezo huo uliopigwa Desemba 23, kwenye uwanja wa Uhuru, timu hizi zilimaliza dakika 90, zikitoka sare kwa kufungana bao 1-1, na kupoteza malengo ya Yanga katika kuwafukuzia wapinzani wao Simba ambao walikuwa wanapishana kwa pointi mbili.
Endapo Yanga itashinda rufaa hiyo basi itafikisha pointi 42 na kupunguza gepu la pointi kati yao na Simba kutoka nne hadi mbili kama ilivyokuwa awali.
-nawasilisha

Mleta Uzi Nadhani Hutaleta Mrejesho Kuhusu Rufaa Yenu ....
Je points zenu munazozingojea Za Mezani Zimepaa anga gani?
Munafikiri Vya Bure Vinapatikana tu Kirahisirahisi Hivyo??
Tafuteni Njia Nyengine Ya Kupata Points lakini Siyo Hiyo Ya Ubwete....
Sasa Ninawashauri tu Nyie Mbeleko FC kuwa Muende FIFA moja kwa moja Mukakate rufaa ya Kuzidai Hizo Points! Lakini Kwa TZ hamna chenu...
Kuhusu rufaa:Yanga yanyimwa alama 3 za bure
cc: demigod