Kuhusu Robotics & microcontroller programming

Ngoja kwanza nitafute Digital Potentiometer nikupe gharama za module, nikizipata nitakujulisha. Vifaa vingine vyote vipo. @wicalumtata
 
Wakuu alpha1 hii ni nini, ni mnataka kuunda kiwanda cha kutengeneza subwoofer tuache kuagiza china au ni kitu gani,nimeishia kuona macodes baaasi,ehe ni vitu gani hivyo mnatengeneza?
 
wakuu alpha1 hii ni nini, ni mnataka kuunda kiwanda cha kutengeneza subwoofer tuache kuagiza china au ni kitu gani,nimeishia kuona macodes baaasi,ehe ni vitu gani hivyo mnatengeneza?

Mkuu,hiyo ni project ya kuunda Audio Signal Level Digital Control System, ambayo inaweza kutumika kwenye subwoofer au music system yeyote, ku-set aina na kiwango cha sauti kwa kutumia push buttons (Tactile Switch) na kwa baadaye IR remote controller.

Hizi ni DIY projects ndogo ndogo ambazo ni kama mwanzo tu na baadaye tunaweza kufika uliko-focus (kuunda kiwanda) iwapo utaalamu na mtaji vitaruhusu,tutengeneze bidhaa zetu za electronics hapa nchini, japo kuna ushindani mkubwa toka kwa bidhaa zitokazo nje ya Tanzania, kwa upande wa bei na ubora.

Hao Wachina nao walikuwa kama sisi, lakini kwa kuwa wabunifu na muda mwingi ku-copy na ku-paste kazi za wenzao eg USA etc, leo hii wako juu kiteknolojia hadi kiuchumi na wanadiriki hata kuyauzia bidhaa mataifa makubwa ambayo ndo vinara wa teknolojia duniani.

KAMA WAO WAMEWEZA HATA SISI TWAWEZA, japo ni sawa na kuotesha mmea mchanga kwenye shamba lenye mimea mikubwa. Mrejee Charles Darwin concept yake ya STRUGGLE FOR EXISTENCE/SURVIVAL FOR THE FITTEST
 
Mkuu wicalumtata, gharama za digital potentiometer ni majanga. Ni kama sh 20,000/- kwa moja ya stereo. Sound System ya 5.1 inahitaji zitumike tatu(FR + FL, SR + SL, Center + SW), jumla sh 60,000/-, Programmed MCU (PIC16F877A) sh 50,000/-, 16 x 2 Character LCD sh 25,000/- na module PCB fabrication plus accessories zingine sh 20,000/- jumla 155,000/-

Gharama inakuwa juu sana kwa kuwa tunanunua kifaa kimoja kimoja halafu kwa retailers, na hii huwezi kufanyia biashara, maana hutapata soko au faida ukipata soko. Tukiwa na mtaji vifaa vikanunuliwa kiwandani au kwa wholesaler kwa kiasi kikubwa, gharama inakuwa ndogo sana.

Kwa kuwa nilikuwa na nia ya kujifunza,nilinunua hizo component toka kwenye hiyo online store ili tu nipate vifaa vya kufanyia mazoezi, sikujali gharama.

Kwa upande wa project yako, ambayo mimi naiona kama pilot project, nashauri ni-design system ya 2.1 kwa kutumia potentiometer moja ambayo channel moja ita-control subwoofer na nyingine tweeter (1.1 in reality) pamoja na LCD. Una-control aina ya sauti kwa kujitegemea(SW or Tweeter independently).

Status na signal level(selectable via option button) zinaonyeshwa kwenye LCD. Buttons zingine baada ya option button ni Vol- & Vol+, hivyo inakuwa na jumla ya buttons tatu. Wewe unaingiza tu sauti toka kwenye preamp na kutoa sauti kwenda kwenye power amp.

Kwa kuwa nilinunua vifaa kwa gharama kubwa(only for educational purpose,not for business), na kwa kuwa nimeshakata kiu yangu ya kutaka kuona kama nitafanikiwa au la, utagharimia 75% tu ya vifaa, 25% bure na labour charge bure, ili nawe ukate kiu yako ya kutaka kujua kama inawezekana au la.

Unanipa sh 60,000/- kwa functional module nzima yenye preprogrammed PIC16F877A, Digital Potentiometer moja, 16 x2 Character LCD na accessories zingine. Ila hiyo MCU itakuwa na Code Protection Fuse Enabled ili kuzuia ku-copy kazi yangu, ukilazimisha ku-copy firmware iliyoko kwenye ROM(Flash memory), kila kitu kinafutika, MCU inabaki empty.

Tafakari unipe jibu. Kama ukiridhia, nijulishe nitafute Digital potentiometer, maana hiyo sina.

NB: Ili kuweza kuunda bidhaa ambazo zitauzika(affordable price), nalazimika kujifunza jinsi ya ku-interface Audio Digital Signal Processors kama PT2313,PT2322,PT2323 etc na MCU. Hili lazima niilifanyie kazi ingawaje linahitaji muda.
 
alpha1,

Fanyeni mambo wakuu, kuna watu tunasikia wamegraduate electronics pale udsm na dit ila hatujui wanafanya nini na nini wamefanya kimeonekana, hasa kwenye maswala ya sound systems.
 
Last edited by a moderator:
Kaka hapo nmekupata ,ila vifaa vya electronics ni garama sana au kwasabu vinatoka nje ya nchi? yan kama nataka nifanye za biashara ni kazi ya ziada sana hapa, maana components ni bei juu kuliko hata bei ya kuja kuuzia.
 
Pia na ss tunahitaj support kubwa kutoka kwenu nyie, maana tunaweza unda musik system afu tukapewa sifa nyingi sana, then no support ili tuweze kwenda beyond,mfano tumeunda musik system ya TSH 250000 lakin mwisho wa siku inaishia kuto nunuliwa @ hii ndo Tanzania.
 
fanyeni mambo wakuu, kuna watu tunasikia wamegraduate electronics pale udsm na dit ila hatujui wanafanya nini na nini wamefanya kimeonekana, hasa kwenye maswala ya sound systems

Mkuu,usiwashangae,maana baada ya ku-graduate na kuingia kwenye ajira,wanakuwa busy na ajira zao. Kuyafanya haya baada ya ku-graduate mpaka awe na hobby ya haya mambo na anafanya kama leisure. Na katika mazingira ya ajira zao, unakuta mambo kama haya hayatumiki, hivyo hawalazimiki kuyafanya.

kaka hapo nmekupata ,ila vifaa vya electronics ni garama sana au kwasabu vinatoka nje ya nchi? yan kama nataka nifanye za biashara ni kazi ya ziada sana hapa, maana components ni bei juu kuliko hata bei ya kuja kuuzia
Hiyo ni kweli. Kama unataka kufanyia biashara, inabidi kununua components kwa wauzaji wa jumla au kiwandani na ununue nyingi.

kuhusu iyo 75% wala usiwe na shaka, ntakujulisha nikiwa tayari
Hakuna shida Mkuu. Jipange.


Kwa product ya kwanza, usiwazie kuiuza, bali itumike kama sample kwa wateja ili kama ni nzuri, iwashawishi wateja watoe order ya kutengenezewa nyingine kama hiyo.

Hivyo inabidi kugharimika mwenyewe ili kubadili concept kuwa product ambayo ni valuable ili mtu ashawishike kununua. Wateja wengi hawako tayari kugharimia concept ila product iliyotokana na hiyo concept.
 
kaka hapo nmekupata ,ila vifaa vya electronics ni garama sana au kwasabu vinatoka nje ya nchi? yan kama nataka nifanye za biashara ni kazi ya ziada sana hapa, maana components ni bei juu kuliko hata bei ya kuja kuuzia
Hili suala la ku-interface PT2313 na MCU ili kupunguza gharama za uzalishaj, nalishughulikia, nikikamilisha mapema kabla ya kupata digital potentiometer, nitakujulisha.
Ila kutumia PT2313 pekee, huwezi kutengeneza system ya 5.1 (6-outputs),kila channel ikiwa controlled independently, bali utapata system ya 3.1 (4-outputs), ila unaweza kuzifanya tweeter amps ku-share output toka kwenye PT2313.
 
ndio unaweza kuzifanya zitumie muundo wa 3.1 badala ya 5.1 .ambapo hapa katika mgawanyo kati ya FR, SR,FL,SL naziweka pamoja.lakin mkuu kuna IC PT2258 nilishaona wameitumia wachina katika 5.1 ila sijawah kuifuatilia
 
ndio unaweza kuzifanya zitumie muundo wa 3.1 badala ya 5.1 .ambapo hapa katika mgawanyo kati ya FR, SR,FL,SL naziweka pamoja.lakin mkuu kuna IC PT2258 nilishaona wameitumia wachina katika 5.1 ila sijawah kuifuatilia
PT2258 ni 6-channel Electronic volume controller tu, haina feature ya input signal multiplexing (haina multiplexer) hivyo huwezi itumia kuchagua zaidi ya input moja kati ya MP3, CD, DVD etc na ndo maana huwa inatumika pamoja na PT2323 6- channels Audio Signal Processor ambayo haina volume controller ndani yake.

PT2313 ina input signal multiplexer, tone controller(bass & treble),pia loudness na volume controller features, ila ina stereo inputs 3 na stereo outputs 2.
 

mkuu naona uko fiti sana kwenye haya mambo,napata shida sana unaposema unafanyia hobby, mkuu ninachoona hii ndio mahali pako,na ungejikita zaidi ungefanya mambo makubwa,sijajua tatizo ni nini kwa upande wako, labda inaona ukifanya serious hailipi,hailipi ontime,hamna support kwa maana ya costs, soko halipo la bithaa hizi za electronics?

Mfumo wa biashara na utawala bongo hauruhusu au urasimu mwingi? mkuu hebu kuwa kama kina mzee ford mwasisi wa ford au aliyeanzisha hyundai. mkuu hata kama umesomea kitu tofauti sio ishu, mbona Mr bean ni electrical eng lakini lakini kajikita kwenye uchekeshaji profshn kaweka penben?

the same to Master J ni electrucal eng kaamua kuwa producer, bill gates hakuwa anasomea it lakini ndicho aliamua kudeal nacho baada ya kuona uwezo na roho yake ipo huko akaamua na kuacha shule kabisa. tafakaru mkuu what God has given you,kama kweli hujasomea hii makitu ukijikita serious utafanya mambo makubwa.

Sijui kama mpaka sasa kuna bidhaa yoyote ya sound system tunayotengeneza wenyewe.hata redio ya mkulima ilishatushinda wakati mwanzoni mambo yalifanyika hapa hapa bongo kiwanda cha matshuta/ panasonic pale nyerere road. tungekuwa na subwoofer, ampl,tv,dvd deck etc lakini iko wapi kila kitu chinaaaaa. ni jambo la kipuuzi saaaaaana badala ya kwenda mbele tumerudi nyuma

NB: Tanzanzania ni nchi inayouwa vipaji badala ya kuviendeleza.
 
Pamoja tunaweza ,nikimaanisha kuwe na ushirikiano baina ya wananchi na viongoz wetu ili waweze kuweka vipaumbele ktk masuala kama haya,ila ninachoona ni survival for the fittest.
 
nduu/mamaya,

Mkuu, najua inalipa ndo maana nikaamua kijikita huko baada ya kuona kuna hii fursa katika nchi yetu. Nakuwa nafanya kidogo kidogo huku naendelea kujifua hasa kwa kujisomea na kufanya practicals mi mwenyewe, ila inagharimu muda, pesa na pia inahitaji concetration sana ya akili.

Nami nafuata nyayo za hao jamaa ulowataja na pia hizo changamoto ulozitaja zipo, ila inabidi kukabiliana na kila moja kwa wakati wake.

Kwa upande wa bidhaa, si sound systems tu ambazo nashughulika nazo, bali najifunza Embedded Systems kwa ujumla kiasi kwamba nikiiva, niwe na uwezo wa ku-design chochote kutokana na concept yangu au ya mteja, niunde kitu ambacho ni operational kwa upande wa electronics, kwa kutumia digital technology.

Nashukuru sana kwa kunipa moyo wa kusonga mbele na kuonyesha mtazamo chanya kuhusu hii fani, kwani asilimia kubwa ya watu wanakuwa na mtazamo hasi, wenye malengo ya muda mfupi(Panda-vuna papo kwa papo), wakati kwa upande wangu ni kinyume.

Nashukuru serikali imeanza kutambua kwamba ukuaji wa sayansi na teknolojia unasukumwa mbele kwa ubunifu, ambao ni chachu kubwa katika maendeleo na uchumi wa nchi kwa ujumla, wakaanzishta taasisi/tume kama COSTECH, TANZICT na BUNI Hub. Hilo ni jambo jema, ila tatizo ni CENTRALIZATION: Huduma ni Dar tu basi, mikoani hakuna kitu.
 
Last edited by a moderator:

Hizo taasis zinatoa huduma dar peke ake? Basi kuna haja ya kuhamia dar maana mm mipango yako kama yangu, siangalii garama za practical nataka kuwa na skils ya kutosha.
 
Habari wakuu

Nataka kuanza ku fabricate PCB ntakazo design nahitaji kujua ni wapi materials hizi zinapatikana,

Copper board
Muriatic acid
Hydrogen peroxide (hii nadhani hata maduka ya dawa zipo)

Kwa anayejua tafadhali njuze wapi napata hivyo vitu hapo juu.

Ntaanza na haka ka simple circuit







Natumia design spark, EAGLE, Kicad na Cwizard ku-design.
 
mjomba fujo,

Mkuu, uliza maduka wanapouza vifaa vya maabara una weza kupata.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…