Habari wana JF?
Inafahamika kua watanzania tuna kasumba ya kuyakuza maneno ya mtaani eidha kwa kujua ukweli wake au kwa kuyadhania tu ili mradi na sisi tuonekane tunajua.
Hili suala la mpaka wa tanganyika na znz linaleta mkanganyiko kwa baadhi ya watanzania kutokana na watu wachache ambao wamekua wakijaribu kuvumisha ni wapi ilipo mipaka ya znz na tanganyika, watu hao hawana ushahidi wowote juu ya wayasemayo kwa watu huku chini chini, cha kusikitisha ni kua baadhi ya wavumishaji hao ni maofsa na watumishi wa serikali kana kwamba hawaelewi madhara wanayoweza kutuletea kama taifa.
Rai yangu ni kwamba, watu wanaovumisha maneno chini chini haswa haya yenye maslahi kwa taifa, waache tabia hiyo kwa kua haitajenga na badala yake itabomoa kutokana na kuwaacha wanajamii njia panda, tanganyika na znz ni wamoja ndio mana tunaishi kama ndugu tangu miaka hiyo.
Ikiwa mtu anadhani anafahamu sana mambo ya nchi asimame hadharani na kuyazungumza na sio kupiga porojo mtaani ili waonekane wanajua wakati mimi kwa mtazamo wangu naona hawajui kitu. mtu anayejua anasimama na kupresent hadharani anachokijua na mwishowe ataukizwa maswali.
Nawasilisha.